Mke aliyemuua Mwalimu huko Kilombero apandishwa kizimbani

Mahakama ya Wilaya ya Kilombero mkoani Morogoro imewapandisha kizimbani na kuwasomea shtaka watu watatu akiwemo Jovina Steven Mwekya (33), mkazi wa Mang'ula ambaye ndiye mke wa marehemu Mwalimu Tungaraza, Musa Amani Mwakyoma (28), mkazi wa Mang'ula, na Tadei Sales Mwinuka (40), mkazi wa Mang'ula, kwa kosa la mauaji.

Wakisomewa shtaka hilo na mwendesha mashtaka wa serikali, Dastan William, mbele ya Hakimu wa Wilaya ya Kilombero, Mhe. Regina Futakamba, amesema mnamo usiku wa Juni 2, 2024, wakati marehemu akiwa amelala chumbani, watuhumiwa hao walipanga njama ya kumvamia chumbani kwake na kumpiga na kitu kizito kichwani, hivyo kusababisha kifo chake.

Aidha, baada ya kusomewa shtaka hilo, watuhumiwa hao wamerudishwa mahabusu mpaka tarehe 25 Juni, 2024, itakapotajwa tena.

PIA SOMA:
- Morogoro: Atuhumiwa kula njama kumuua mumewe ili ale raha na bodaboda

Team kataa ndoa wanazidi kupata points za kugomea kuoa au kuolewa.
Watawaachia tu ili wakalee watoto, maana bila hivyo watoto wataishia mitaani…kama siyo kuwaachia wote basi mmoja wao
 
Daaah,
 
Mke

Bushlawyer katika ubora wako,ithibitike kuwa wamehusika harafu mmoja wao aachiwe kulea watoto?
 
Hata wanapopima DNA lakini wanatoa majibu ya tofauti ni sababu ya Bush Lawyer.
Hata kuachiwa kwa akina Sabaya ni sababu ya Bush lawyer, hata yule aliyeingizwa chupa sehemu ya haja kubwa lakini DPP akafuta kesi ni sababu ya Bush lawyer.

Hongera nyingi sana kwako Town Lawyer
 
Kuna mambo yanahuzunisha sana! Mwanamke una miaka 33! Tena ni mke wa mwalimu mkuu wa pale S/M Signal (inataamkwa Zignali na wenyeji)! Umezaa watoto wawili na huyo mume wako!

Ila katika hali ya kushangaza, unaamua kutembea na bodaboda mwenye umri wa miaka 28! Na mnafikia mpaka hatua ya kupeana mimba na kuzaa mtoto wa 3 na huyo bodaboda wako!! Umeonywa uachane na huyo bodaboda wako, lakini wapi!!

Na badala yake unaamua kumuua mume wako ili ufaidi vizuri maisha na huyo bodaboda wako! Kwa kutumia akili kisoda mlizojaliwa kwenye vichwa vyenu, mnatekeleza kweli hayo mauaji! Na mwisho wa siku wote mnaishia jela!!
Hii sijui ni mental health au ni ukosefu wa elimu na exposure. Very low thinking, inasikitisha sana
 
Ngoja ninunue bunduki kmmmke mama Jovin kila mara anaulizia hati ya nyumba zetu
 
Back
Top Bottom