Mke aliyemuua Mwalimu huko Kilombero apandishwa kizimbani

Yaani, labda huenda alifata show. Ila sasa kaharibu maisha yake yote. Anawaacha watoto, walelewe na ndugu. Ngono inakatisha ndoto zote!!!
Yani ndoto zotee..kwa sbb yy alichukulia simpo tuu..kwamba nitakua na mchepuko wangu boda mr akijua atajijua kila mtu ataishi maisha yake kumbe na shetani nae anamwangalia tuu anasema utajua hujui huyo hutakaa nae na mume hutamuona tena...ukijua ya mbeleni tutaogopa sana...ni bora uwe unaisikiliza ile sauti ya ndani kabisa inayokwambia acha...
 
Kweli sauti ya ndani ndiyo roho Mtakatifu mwenyewe. Hii ya kuendekeza kichwa na chini. Matokeo yake ni haya, ila watu wanaotoa uhai wa wenzao. Ni wamezaliwa hivyo? Ni pepo inawashika? Ama ni kitu gani? Maana mpaka binadamu anakata roho mmh!!!
 
fate
 
Hata hawaoneshi sura za majuto! Ila baada ya kukaa jela kwa muda mrefu, naamini akili zitawakaa tu sawa.

Natamani huyo boda na mwenzake wapelekwe gereza la kilimo Idete ili wakabadilishe mazingira. Halafu huyo mwanamke abakie tu pale Kiberege.
 
Kweli sauti ya ndani ndiyo roho Mtakatifu mwenyewe. Hii ya kuendekeza kichwa na chini. Matokeo yake ni haya, ila watu wanaotoa uhai wa wenzao. Ni wamezaliwa hivyo? Ni pepo inawashika? Ama ni kitu gani? Maana mpaka binadamu anakata roho mmh!!!
Mkuu hua nawaza pia nadhani ufahamu wao hua umekadatwa na ibilisi kwa wakati huop
 
Kuna mambo yanahuzunisha sana! Mwanamke una miaka 33! Tena ni mke wa mwalimu mkuu wa pale S/M Signal (inataamkwa Zignali na wenyeji)! Umezaa watoto wawili na huyo mume wako!

Ila katika hali ya kushangaza, unaamua kutembea na bodaboda mwenye umri wa miaka 28! Na mnafikia mpaka hatua ya kupeana mimba na kuzaa mtoto wa 3 na huyo bodaboda wako!! Umeonywa uachane na huyo bodaboda wako, lakini wapi!!

Na badala yake unaamua kumuua mume wako ili ufaidi vizuri maisha na huyo bodaboda wako! Kwa kutumia akili kisoda mlizojaliwa kwenye vichwa vyenu, mnatekeleza kweli hayo mauaji! Na mwisho wa siku wote mnaishia jela!!
 
Huyu dada na urembo wake kwel akaamua kumuua mkewe kisa bodaboda, haya maisha yana maajabu sana.
 
CCM ina wanachama wauwaji
 
Mkuu hua nawaza pia nadhani ufahamu wao hua umekadatwa na ibilisi kwa wakati huop
Kwa kweli, maana haiingii akilini mtu na akili zake, aamue kuuwa mume,baba wa watoto wake. Kisa mapenzi ya nje. Ni shetani anawashika akili. Now akili zimewarudia watashaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…