Mke ameleta dada wa kazi nyumbani pasipo kumshirikisha mume

Mke ameleta dada wa kazi nyumbani pasipo kumshirikisha mume

Karibu JF mtandao ambao mtu huleta tatizo lake binafsi kwa kupitia mshikaji/jamaa yake
Mi nahisi we unavimelea vya ubishoo....Sioni kama Kuna ubaya,sio lazima tatizo likukute wewe ndio useme hata lamwenzio ni sawa madam kusaidiana kutatua changamoto ,changamoto ni za Kila binadamu zipo tunaishi Nazo azikwepeki...ndio mana kunakushauriana ...
 
Mke amlipe housgirl
Kumlipa housegirl sio issue. Issue ni gharama anazotumia nyumbani kwako ambazo ukizijumlisha zinazidi mshahara wake hata mara tatu (3) kwa mfano:
1. Chumba anacholala kama angepanga angelipa say 50,000 kwa mwezi
2. Umeme anaotumia say kwa mwezi 5,000
3. Maji kwa mwezi 5000
4. Uchakavu wa vitu anavyotumia 5000
5. King'amuzi anachotumia 5000
6. Chakula 6000 x siku 30 = 180,000

Jumla kuu 250,000

Hapo hata kama mshahara atalipa mke bado itakula kwako tu
 
Kisa kiko hivi

Mshikaji wangu kaniomba ushauri wa mawazo,kanihadithia issue nzima ilivyo,ila point ya msingi ni kwamba mkewe ameleta housegal nyumbani pasipo kumshirikisha, anasema hapafahamu kwao na huyo binti wala wazazi wake,na pia yeye jamaa hana budget ya kulipa msichana wa kazi kwa sasa kwani mambo yake hayako vizuri,hivyo anashangaa kuletewa mgeni ndani kwake asiyemtambua.

Maamuzi yake yalikua ni kumchapa makofi mkewe na amtimue huyo binti arudi kwao.

Ila mimi nimemtuliza nimemwambia yeye ajifanye mjinga kama hajui lolote linaloendelea aone mwisho wa mwezi kama ataombwa mshahara wa huyo binti ama vipi,hapo ndio afungue mdomo wake sasa.

Nyie wakuu mna ushauri gani kwenye hili suala?
Adhabu yake mpandishe cheo huyo dada kuwa waziri wa mambo ya ndani wakati ukiandaa utaratibu wa kumpandisha cheo cha Rais wa SMZ😊😊
 
Kumlipa housegirl sio issue. Issue ni gharama anazotumia nyumbani kwako ambazo ukizijumlisha zinazidi mshahara wake hata mara tatu (3) kwa mfano:
1. Chumba anacholala kama angepanga angelipa say 50,000 kwa mwezi
2. Umeme anaotumia say kwa mwezi 5,000
3. Maji kwa mwezi 5000
4. Uchakavu wa vitu anavyotumia 5000
5. King'amuzi anachotumia 5000
6. Chakula 6000 x siku 30 = 180,000

Jumla kuu 250,000

Hapo hata kama mshahara atalipa mke bado itakula kwako tu
Kwa kawaida binti huamka saa 10 alfajiri kutwa yupo kikaangoni kulala around saa tano
Kwa mujibu wa masaa ya kazi, huyu binti ilimpasa aanze kazi saa 1 na nusu amalize kazi saa 9 alasiri. Tupige hayo masaa ya extra time times allowance atapata how much?
NB: Either win-win situation au win-lose(binti) situation.
 
Huyo mwanamke ndo kichwa cha familia... jamaa akikaa kimya ataonekana lofa hasa kama mkewe ni mama wa nyumbani sasa dada wa kazi wa nini??
 
na
Nimekusoma mkuu
na kamtarifu jamaa yako serious aise !!! dawa nzuri sana hii, dunia ya sasa usipambane na mwenza, kuna ustawi wa jamaa utafunguliwa kesi zitakzo kutia hasara tu, pambana na situation na sio mtu
 
Kumlipa housegirl sio issue. Issue ni gharama anazotumia nyumbani kwako ambazo ukizijumlisha zinazidi mshahara wake hata mara tatu (3) kwa mfano:
1. Chumba anacholala kama angepanga angelipa say 50,000 kwa mwezi
2. Umeme anaotumia say kwa mwezi 5,000
3. Maji kwa mwezi 5000
4. Uchakavu wa vitu anavyotumia 5000
5. King'amuzi anachotumia 5000
6. Chakula 6000 x siku 30 = 180,000

Jumla kuu 250,000

Hapo hata kama mshahara atalipa mke bado itakula kwako tu
Acha roho mbaya Hapo labda chakula tu,na maji ya kuoga kidogo,the rest ni cost sharing inahusika
 
Very simple. Kuanzia leo akirudi nyumbani ni mwendo wa kuzunguka na boxer tu. Akihitaji chochote amuite dada wa kazi hata kama mkewe yupo. Ahakikishe anamwaga sifa za kutosha za housegirl juu ya uzuri na uchapakazi wake kwa mkewe. Kama alivyokuja bila kutaarifiwa basi hakika ataondoshwa pasi kujulishwa akifanya hayo.
[emoji419][emoji419][emoji419][emoji419]
 
mwambie jamaa nae awe anakua serious saa zingine, mbona anakua kama sio mtu mzima!? Yaani ameshindwa kucrack code ndogo kama hiyo? Jamaa inaonekana mke wake kamzidi akili.
 
House girl ana umri gani? Mbona kazi rahisi tu hiyo
 
Back
Top Bottom