MABINTI WA CHUO 03
Feedback zimekuwa nyingi kutokana na ule Ujumbe niliouandika wa Kwanza kabisa kuhusu Wadada wa chuoni na Mabadiliko Yao pindi wanapokuwa chuoni. Asilimia kubwa Mabadiliko huwa ni Negative na asilimia chache ni positive.
Ukiacha Miaka Yetu ya Nyuma kidogo angalau ilikuwa Kati ya Mabinti 10 utapata 5 wapo wanapakua na kupika, 3 wanaenda ghetto Ijumaa na wanarudi jumatatu asubuhi, 1 yeye huwa anaenda mara moja moja Sana na 1 ndo unakuta katulia Tu. Lakini kwasasa Hali imezidi kuwa Tete kwasababu Kati ya Wadada 10 utapata Mmoja Tu ambaye hajihusishi na hayo Mambo.
Nimejiuliza Sana kitu gani kinatafutwa Sana na Binti mdogo kuyabeba Majukumu ya Mke akiwa hajui hata ni nini Maana ya Mke. Hiko kitu unachokitafuta cha kuwa Mke sasa Kabla ya wakati nakwambia hata ukisubiri ukaja ukaolewa kiuhalali na Mwanaume sahihi utakikuta Tu kinakusubiri. Kinachokusibu uwahi sasa kinakuharibia destiny yako.
Kwasasa asilimia kubwa ya Wadada wanatafuta unafuu wa Maisha hasa pale anapojikuta Hana boom anasahau kilichompeleka chuoni anasema nikipata Mtu wa kunilisha na kufix Kodi nimemaliza. Anasahau Hatma kubwa iliyopo Mbele yake iliyomtaka kujitunza sasa na kuyaishi Maadili na Utakatifu. Mwingine anatoka kwao wazazi wameokoka na yeye kaokoka wengine wazazi ni wachungaji lakini anakwambia Mchungaji ni Baba siyo Mimi. Kwani ni ngumu kuyaishi uliyofundishwa nyumbani?
2 Timotheo 3:15
[15]na ya kuwa tangu utoto umeyajua maandiko matakatifu, ambayo yaweza kukuhekimisha hata upate wokovu kwa imani iliyo katika Kristo Yesu.
Post iliyopita nilielezea Tu suala la kuzalishwa na kutelekezwa. Kuna haya;
1. Unakunywa P2 ili uzuie Mimba ufanye Uzinzi kwa Raha unasahau effect ya vidonge vya P2 ni kubwa Sana, Unasahau effect ya Kiroho kwenye haya Mambo. Unatoka hapo umefanikiwa kutoka hujabeba Mimba lakini umeondoka na cancer,sijui ugumba vinayoletwa na hayo madawa, Umeondoka na maroho machafu ambayo yatakusumbua Maisha yako Yote. Sasahivi asilimia kubwa ya Wadada wa chuo ukikamata Ile mikoba Yao Lazima ukutane na hivi vidonge.
Imagine Binti wa miaka 20 anapambana na vidonge asishike Mimba huyo mpaka anafikisha Miaka 28 atakuwa kwenye hali gani? Ni ajabu Sana kuona Muda ambao Binti alipaswa apambane na Coursework anapambana na boxer za Kijana ambaye hata hamjui ametokea wapi. Muda alipomaliza shule alitakiwa kuwa anafanya kazi nzuri lakini sasa anapambania Afya yake kwasababu wengine huwa wanatoka tayari wameshaambukizwa Magonjwa ya zinaa n.k
2. Utoaji wa Mimba...
Ni kweli Mtaani wapo wanawake wanaotoa Sana Mimba lakini chuoni hii sasa imekuwa inaenda kwa Kasi Sana. Binti ukishajiona umefanya Maamuzi ya kuwa Mke usisahau kuna kubeba Mimba; sasa na balaa la haya Mimba kunasa huwa haiangalii huyu ni mwanafunzi kwasasa hapa yenyewe unatunga kufuta Mchakato mnaoufanya. Sasa kama hauko tayari kuwa Mama wakati unasoma ebu kaa hostel soma maliza, fuata Mchakato,olewa,beba Mimba ndani ya ndoa hapo huwezi kuitoa na unajua kuwa Malezi ya Mtoto ni uhakika 100%. USITOE MIMBA! Kama ulifanya Maamuzi ya kubinjuka hayo ndo Matokeo.
Yeremia 1:5
[5]Kabla sijakuumba katika tumbo nalikujua, na kabla hujatoka tumboni, nalikutakasa; nimekuweka kuwa nabii wa mataifa.
Mara Kadhaa hata vyombo vya habari vimekuwa vinarusha taarifa unakuta Binti na Kijana waliokuwa wanaishi pamoja Mmoja kamchoma mwenzie kisu na kumuua kwasababu ya wivu wa kimapenzi; mwingine anajinyonga kabisa kwasababu kaachwa. Hatma za Watu Bora zinafia njiani kwasababu ya kutokujielewa na kujua nini kimewapeleka Chuo. Binti usifanye Mistake ya kuishi na Mtu asiyejulikana kwenu,hajakulipia Mahari,hajakuoa kuna siku atakuja kukuulia huko ndani. Na wengine Mpo mnapigwa kabisa na bado unajifanya ni Mama Mjengo Imara.
WITO KWA WAZAZI
Kama hakuna Mtu Amekuja kwako Kutoa Mahari kwaajili ya Binti yako na kumuoa basi Mtoto wako bado hayakua kuanza kujitegemea kwenye kila kitu sasa. Weka juhudi za kumfuatilia kwa kina; Kufuatilia Maendeleo yake ya Kiroho, Anaendele na Mifungo? Anaomba? Anaenda Kanisani? Wakati mwingine Nenda Physically ukute hata anavyovaa kama kuna ndugu Mkoa husika wale jukumu la Kumfuatilia.
Kumuona amefika Chuo ukaona anajitosheleza na afanye kila kitu mwenyewe ndo yanakuja kutokea haya. Na kwasasa Mtu haoni Thamani ya Neno Ndoa anauliza kipya ni nini humo ndani? Maana tayari anajua kila kitu. Lakini mzazi ukiweka juhudi ya kujua kila kinachoendelea kwake kwa kila njia itasaidia kupunguza au kuondoa kabisa haya Mambo.
God Bless You!
Giftrose Joel Amasi
0629786447