Kwanini asitafute hukohuko mtaani?! Tena ndio vizuri sababu anaweza akatarget wasichana wawili au watatu akawa anachunguza taratibu huku anaendelea nao kimahusiano kama akiridhika nao aoe kabisa.
Tena itakusaidia kwenye kuziona na kujua tabia/mapungufu yao na makuzi yao kuliko ukutane na mtu humjui halafu uaminishwe tabia yake nzuri maana wengine sio waaminifu watafanya hivyo kumsaidia mtu wao apate ndoa tu!!
Yote ya yote boss, mwenyezi Mungu awatangulie, kikubwa mfanye sana maombi, musali awaonyeshe chaguo sahihi. Kutafuta mke mwema nayo ni kazi sana sikuhizi.
Nakumbuka kuna jamaa alikuja kutangaza kabisa kanisani kwetu kwamba anatafuta mke. Baada ya matangazo akapewa muda akajasema nia yake. Alipewa hiyo nafasi jumapili mbili na alifanikiwa kupata mke kupitia kanisa!! Mshirikisheni sana Mungu katika hilo!!