Mke hataki ndugu wa mume:Msaada please.

Huyo jamaa inabidi asimame kwenye nafasi yake ya ubaba na kamwe asithubutu kukubali mawazo ya mke yaliyojaa uovu na hila, hata hivyo atafute muda wakae na mkewe wajadili suala la malezi ya mtoto huyo na ndugu wengine ambao wanahitaji msaada wao kuwa ni jambo lisiloepukika. ila vikao vyote hivyo avifanye kwa makini na ustaarabu huku akitumia lugha iliyojaa hekima na kumtia moyo mkewe ili akubaliane na huduma hiyo wanayoitoa.
 
Wewe mtoa mada, umekuwa kama vile huna uzoefu na maswala ya kindoa vileee!!
Hizi kesi/ mijadala/ maombi ya ushauri huwa yako ya aina nyingi, kama
- kutafuta solution ya ukweli ( ambapo wote wahusika husikilizwa na kueleweka) ambapo kii kesi yetu haipo
- au kutafuta syompathy (sidhani kama hii inahusika)
- kutafuta kuchangamsha baraza (nadhani tuko hapa)

Nadhani tunachangamsha baraza, na mie kwa upande huo niseme kuwa ndoa nyingi zenye michanganyiko ya misimamo, uelewa, mitazamo ya misingi ya mambo muhimu maishani huwa ni ngumu.
Hasa matamanio ya ngono yanapoongoza wakati wa kutafuta mwenzi.

Kwa kumtazama huyo jamaa yako, inaelekea alivutiwa na vitu vingine wakati wa kuoana, bila kujua mrembo ana mtizamo gani sasa anajutia big time.
Ndo narudia kusema amuache aanze upya. Haswa kama hataki kukaa meza moja kuongea naye.
Ni jambo la kusikitisha lakini it is a fact.

Ndoa nyingi watu huishi nyumba moja lakini waliachana zamani
kila mtu ana agenda zake.
Hayo ni matokeo ya ule wakati vijana walipoanza kukataa maoni ya kuwahusu wanawake wanaofikiria kuwa wanawapenda na wanatamani kuishi nao.

Watoto yatima wengi tu wako boarding na asilimia kubwa wanatoka katika koo za makabila mbali mbali, kwa sababu mbalimbali. mojawapo ikiwa baba au mama mwenye ndugu anashindwa kuwakilisha hoja mezani hadi ipate kibali, (sababu ya kiburi cha pesa, ujinga, woga, majungu nk)
 

Nadhani mume alitaka kuangalia mkewe atare-act namna gani kwani baada ya kumkubalia na huyo kijana kufika, mke hajasema chochote zaidi ya kumuandalia mahali pazuri pa kulala.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…