Mke hataki ndugu wa mume:Msaada please.

Mke hataki ndugu wa mume:Msaada please.

Kuna jamaa yangu kaniomba ushauri juu ya tatizo linalomkabili. Yeye kaoa mke. Baada ya kufiwa na mdogo wake wa kike, ndugu waligawana watoto wa marehemu na yeye(jamaa) akapewa mtoto m1 ili amtunze na hasa ikizingatiwa kuwa hakuwa na baba. Matatizo ya mke ndo yakaanza. Mara simtaki huyo mtoto kwa kuwa hukunishirikisha. Mara mtoto huyo ameshndikana huko alikotoka kwa kuwa ni mtundu. Mke ameendelea kusistiza kuwa hamtaki huyo mtoto licha ya kupita miaka 3 sasa. Kutokana na presha ya mke wake, jamaa aliamua kutafuta shule ya boarding ya watoto yatima lakini bila ya mafanikio. Pia aliwahi kumchukua ndugu yake mmoja ili amsaidie kwenye biashara zake lakini kelele za kumkataa zikasikika na hatimaye yule kijana akaondoka. Jamaa wiki iliyopita aliombwa na ndugu wa mke ampokee kijana wake akae kwake ili ajiandae kure-sit mtihani wa fm4 mwaka huu. Jamaa hakuwa na hiana akamkubalia bila ya kumshikisha mke wake huku akihofia kelele za mke wake kwa kutomshirikisha. Kijana kafika na hakuna kelele.
Huyo jamaa inabidi asimame kwenye nafasi yake ya ubaba na kamwe asithubutu kukubali mawazo ya mke yaliyojaa uovu na hila, hata hivyo atafute muda wakae na mkewe wajadili suala la malezi ya mtoto huyo na ndugu wengine ambao wanahitaji msaada wao kuwa ni jambo lisiloepukika. ila vikao vyote hivyo avifanye kwa makini na ustaarabu huku akitumia lugha iliyojaa hekima na kumtia moyo mkewe ili akubaliane na huduma hiyo wanayoitoa.
 
Wewe mtoa mada, umekuwa kama vile huna uzoefu na maswala ya kindoa vileee!!
Hizi kesi/ mijadala/ maombi ya ushauri huwa yako ya aina nyingi, kama
- kutafuta solution ya ukweli ( ambapo wote wahusika husikilizwa na kueleweka) ambapo kii kesi yetu haipo
- au kutafuta syompathy (sidhani kama hii inahusika)
- kutafuta kuchangamsha baraza (nadhani tuko hapa)

Nadhani tunachangamsha baraza, na mie kwa upande huo niseme kuwa ndoa nyingi zenye michanganyiko ya misimamo, uelewa, mitazamo ya misingi ya mambo muhimu maishani huwa ni ngumu.
Hasa matamanio ya ngono yanapoongoza wakati wa kutafuta mwenzi.

Kwa kumtazama huyo jamaa yako, inaelekea alivutiwa na vitu vingine wakati wa kuoana, bila kujua mrembo ana mtizamo gani sasa anajutia big time.
Ndo narudia kusema amuache aanze upya. Haswa kama hataki kukaa meza moja kuongea naye.
Ni jambo la kusikitisha lakini it is a fact.

Ndoa nyingi watu huishi nyumba moja lakini waliachana zamani
kila mtu ana agenda zake.
Hayo ni matokeo ya ule wakati vijana walipoanza kukataa maoni ya kuwahusu wanawake wanaofikiria kuwa wanawapenda na wanatamani kuishi nao.

Watoto yatima wengi tu wako boarding na asilimia kubwa wanatoka katika koo za makabila mbali mbali, kwa sababu mbalimbali. mojawapo ikiwa baba au mama mwenye ndugu anashindwa kuwakilisha hoja mezani hadi ipate kibali, (sababu ya kiburi cha pesa, ujinga, woga, majungu nk)
 
Hiyo alikuwa anafahamu sana kuwa ndugu yake anatakiwa kuja but kwa kumheshimu mume wake alimuomba huyo ndugu mwenye mtoto amuombe mume kama mkuu wa familia na hilo pia mume alitakiwa kulifikisha mezani but kwa kichwa chake cha mfume dume akona yeye ni final say. Sasa

Nadhani mume alitaka kuangalia mkewe atare-act namna gani kwani baada ya kumkubalia na huyo kijana kufika, mke hajasema chochote zaidi ya kumuandalia mahali pazuri pa kulala.
 
Back
Top Bottom