Mke HIV+ anahitajika

Mke HIV+ anahitajika

goggles

JF-Expert Member
Joined
Apr 1, 2017
Posts
2,415
Reaction score
2,358
Wanasema hakuna marefu yasiyo na ncha. Ni takribani 5yrs imepita tangu nifiwe na marehemu mke wangu. Mara baada ya mama watoto wangu kufariki nilikuta nimeingia katika mapenzi na mama mmoja ambae nilidumu nae kwa miaka miwili. Mama huyo tuliachana kwa sababu zisizozuilika

Mwaka 2018 niliamua kupima afya ili nioe, ajabu nilibainika kuwa na maambukizi ya virusi vya ukimwi. Nilivyogundulika na ugonjwa huo niliamua nisioe. Lakini kadri siku zinavyoenda nimebaini kuna umuhimu wa kuwa na mke. Na hii imetokana pia na ushauri na Dr ambae ni rafiki yangu wa karibu.

Umri wangu ni miaka 48 hivyo mke atakekuwa tayari kuolewa na mimi pia awe na umri wa miaka 40+ (mtu mzima).

Kwa sasa nimepata uhamisho nahamia mkoa wa Mara mda wowote, ambapo pia na mimi ni mzaliwa wa mkoa wa Mara hivyo nikimpata mke wa mkoa wa Mara itapendeza zaidi.

Masharti ya mke ninaemhitaji pamoja na umri niliyoutaja hapo juu lakini pia awe ni mtumishi wa idara yoyote au awe ni mjasiliamali.

Kwa maongezi zaidi ni-PM tupeane mawasiliano.

Nawasilisha tafadhari
 
KILA LA HERI MKUU NA IMANI UTAMPATA PIA POLE SANA KWA KUONDOKEWA NA MKEO KIPENZI
 
Pole kiongozi Kuna mmoja alikua anatafuta mume HIV+ jaribu kutafuta uzi wake
 
Pole sana bro kwa msiba wa shemeji na pole kwa masahibu yaliyokukuta,Mungu ni mwema kama kweli una nia ya kuowa imani yangu utapata mke mtakaeendana hali.

Kila la heri mkuu.

Sent from my Redmi Note 5 using Tapatalk
 
Kuna binti yupo mpanda ana umri wa miaka 23 ni mjasiriamali
 
Chief bahati njema kwako, lakini umekuwa selective sna mtumishi anaweza kosa itakuwa je....

Sent using Jamii Forums mobile app
Mazoea yana tabu yake ndugu. Xwife wangu alikuwa ni mtumishi na niliona faida ya kuwa na mke mtumishi especially mkiendana kwa tabia na mkakubaliana katika malengo yenu. Hivyo ndiyo maana napenda kumwenzi xmrs wangu. Lakini pia kuna chaguo la pili la mjasiliamali

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom