@mtambuzi
Unajua unapoteza mapato na hizi story zako
Ungana na Shigongo kwenye riwaya au anzisha viarida vya stori fupi fupi hata ukiuza sh.2000 utapata faida kubwa.
Hebu wana JF fungukeni hapa, nimshauri nini huyu mwenzetu mbaye ndoa yake inaonekana kumuelemea?
Si ana biashara bwana, haina haja kuumizana vichwa..Chukua watoto peleka boarding, alaf home kila mtu ajitegemee kwa mahitaji, kuanzia misoc n evrthn! OVER...
Mbona pole zake!
Sasa tukifunguka si ndio rafiki yako atajinyonga maana ataona kapata laana!
Ila cha kuuliza - kwani alimpatia wapi huyo mke? Hakumchunguza kujua hulka zake?
Sitaki kuamini huyo mdada/mmama amekuja kubadilika ghafla.Kama kabadilika ghafla, ni kwanini?
Anadai mabadiliko yalianza taratibu mwendo kama kinyonga, na ghafla graph ikapanda....................
Nimeeleza wazi kwamba alimpa mimba kiwa form four na ndipo akalazimishwa kumuoa na baab wa binti.
@mtambuzi
Unajua unapoteza mapato na hizi story zako
Ungana na Shigongo kwenye riwaya au anzisha viarida vya stori fupi fupi hata ukiuza sh.2000 utapata faida kubwa.
mkuu hapo ndipo tatizo lilipoanza kwani naamini mwanamke amejiweka kwenye nafasi ya kutokufanywa lolote na inawezekana ameshajielewa ni kiasi gani mapenzi aliyonayo kwa mwenzake.. kingine ile dhana ya kwamba ndoa ililazimishwa kutokana na ujauzito nalo linachangia ..
kifupi ndoa inapokuwa na sababu ya tatu katika kufungwa huwa inakuwa ni tatizo tayari
Kumbeeee eh!........... nishapata pa kuanzia sasa.......................
pia hata mwanaume inawezekana alipata athari kisaikologia na alikuwa anaamini si chaguo lake na inawezekana pia akawa ndo chanzo cha tatizo .. pia anaweza kuwa amepata mtu (mwanamke) mwingine kwake anaamini ndo chaguo lake hivyo kapata sehemu cha kulinganishia , na kwa kuwa alikuwa tayari anaamini si chaguo lake hivyo amejikuta anatunza madhara badili ya kurekebisha..
Acha masihara bana................. Unajua wewe ni mtu mzima sasa, au huzioni hizo mvi zako kichwani?
Sasa ikiwa huyu bwana yuko hivyo, anaonesha amekuwa sikio la kufa.Hata mimi hilo tatizo la upole wa mume nimeliona, jamaa ni mpole sana na ana muogopa mkewe kupita kiasi, kwa kifupi naweza kusema ameshikwa hasa.................
Sasa ikiwa huyu bwana yuko hivyo, anaonesha amekuwa sikio la kufa.
Si ajabu hata ukimshauri ataenda kumwambia mkewe kuwa Mtambuzi ameniambia hivi na vile. Hayo mengine yote anayodai "eti kwao mkewe hakuna wa kumkalisha chini, mama ameshindwa na watoto aliozaa mwenyewe", ni visingizio tu vya kuhalalisha upole wake. Atendelea kukulalamikia kwa sababu yamemfika shingoni, lakini nina wasiwasi yeye mwenyewe anamwogopa mkewake.
Kama ana ubavu, mwambie anatakiwa kutawala hapo nyumbani kwa mkono wa chuma mpaka mambo yataporejea katika hali ya kuvumilika.
Talaka sio busara, lakini kama ufumbuzi wa mwisho talaka inaruhusiwa pale ambapo ndoa inakuwa karaha badala ya raha. Kwa ufupi kazi ipo!