Sasa ikiwa huyu bwana yuko hivyo, anaonesha amekuwa sikio la kufa.
Si ajabu hata ukimshauri ataenda kumwambia mkewe kuwa Mtambuzi ameniambia hivi na vile. Hayo mengine yote anayodai "eti kwao mkewe hakuna wa kumkalisha chini, mama ameshindwa na watoto aliozaa mwenyewe", ni visingizio tu vya kuhalalisha upole wake. Atendelea kukulalamikia kwa sababu yamemfika shingoni, lakini nina wasiwasi yeye mwenyewe anamwogopa mkewake.
Kama ana ubavu, mwambie anatakiwa kutawala hapo nyumbani kwa mkono wa chuma mpaka mambo yataporejea katika hali ya kuvumilika.
Talaka sio busara, lakini kama ufumbuzi wa mwisho talaka inaruhusiwa pale ambapo ndoa inakuwa karaha badala ya raha. Kwa ufupi kazi ipo!