Mke ka-'confess' jamaangu kachanganyikiwa...

Mke ka-'confess' jamaangu kachanganyikiwa...

pumbatupu

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2011
Posts
256
Reaction score
82
WanaJF kama kawaida hii ndio kona yetu ya kubadilishana mawazo. Leo kuna jamaa yangu yamemkuta makubwa..Ni hivi: Anaye mke wake mjamzito wameishi pamoja sasa karibu miaka mitano.Mwanzoni mwa ndoa yao kiukweli jamaa yangu alikuwa hajatulia, waliendelea kuzinguana hivyo mpaka juzi kati nadhani mwezi wa nne ambapo jamaa yangu aliamua ku'confess' mabaya yote ambayo aliyafanya na kwa kweli bila kutegemea mke wake alimsamehe na kumuahidi upendo ilimradi tu yasijitokezee tena.Na jamaa yangu alimuombia mkewe ku'confess' kama alishawahi kumtenda..lahaulah..lakwata hapo ndo jamaa kabaki hoi bin taaban. Yaan mke wake huku akilia alimuambia kuwa ..aliamua kutembea na jamaa yake wa zamani baada ya kuona mshkaj anamzingua na hana uhakika kama hata hiyo mimba kama ni yake maana aki-backdate tarehe zinagongana na zile alizodate na Jamaa wa nje??..Amemuomba mume wake wasameheane waendelee kama kawaida..kwamba mbona yy kamsamehe..mshkaj kamuambia subiri....
jamaa kaja kuniomba ushauri..na mimi naomba kuwashirikisha wanaJF tumshaurije huyu mkuu??
 
Yeye alipo-confess si amesamehewa?! Sasa anauliza nini wakati mfano keshaonyeshwa...! Ukijua wewe ni mwepesi wa kutapika/ una kinyaa usimchunguze sana mamantilie... Omba msosi, kandamiza, sepa. Ukimchunguza mama muuza hutakula. Yeye alijua my wife wake ni malaika??? Atulize boli tu, ngoma iko droo hiyo...
 
..wasiwasi wake ni itakapogundulika mimba siyo yake..
 
Kwakweli mume ndio aloanza ufuska wake na amempa mkewe mwanya yakufanya alio yafanya japo kua mke vilevile anamakosa,chamsingi wasamehe yane kwani hakuna binadamu asie tenda makosa,ukizingatia kuna kiumbe wanakitarajia,lakini huyo mwanamke angekua mie hata unishikie Kisu nakwambia mumewangu kama unaniua niue tu lakini sijafanya,hajui kama wanaume wanataka wafanye wao2 wakifanyiwa wanaweza hata kukutoa roho,eti Confess! loh unanini bibi uso ka kimnya.
 
Anapenda kusamehewa na sio kusamehe ehhh?!Mwambie hayo ndio malipo yake...sasa ayakubali au ayakatae ni juu yake.
 
.... kuna jamaa ...alikuwa hajatulia, .....aliamua ku'confess' mabaya yote..mke wake alimsamehe na kumuahidi upendo ilimradi tu yasijitokezee tena....

... mkewe ku'confess' ....aliamua kutembea na jamaa yake wa zamani baada ya kuona mshkaj anamzingua....Amemuomba mume wake wasameheane waendelee kama kawaida..

Kwa haraka haraka matokeo ni 1 - 1 = 0.. yaani ngoma droo... tena kikubwa mimi kama refa naweza kukataa goli la jamaa yako kwani mkewe alifanya dhambi baada ya kushawishiwa na tabia chafu ya mume wake.. naweza kumpa credit mke..

Kikubwa..wakubali maisha ya kitoto yamepita..Sasa..movie ya maisha ya kweli ndio inaanza.. waende Hospital kupima afya zao..kama wazima wakubaliane kufunga kufuri zao.. wakubali kulea mtoto bila kupima DNA.. "kitanda hakizai haramu"

Pia mwambie huyo jamaa yako si vizuri kumtendea mke mambo mabaya halafu ukategemea yeye abaki kama alivyo..mke ni binadamu kama wewe na ana-feelings kama wewe..Alichopata ni mshahara wa dhambi zake..
 
Mwambie hivi amsamehe makosa yake, kama vile yeye alivyosamehewa makosa yake. Ikiwa yeye ni binadamu na anadhani anastahili kusamehewa, basi na huyo mama ni mwanadamu anayestahili kusamehewa pia.
 
Nimekusoma mkuu...
 
Mwambie hivi amsamehe makosa yake, kama vile yeye alivyosamehewa makosa yake. Ikiwa yeye ni binadamu na anadhani anastahili kusamehewa, basi na huyo mama ni mwanadamu anayestahili kusamehewa pia.
Nimekupata dada LD..
 
Anapenda kusamehewa na sio kusamehe ehhh?!Mwambie hayo ndio malipo yake...sasa ayakubali au ayakatae ni juu yake.
Unamaanisha mkuki kwa nguruwe...teh..teh..teh...na wewe bi dada??? Lizzy
 
Haya mambo mengine ni kama kujitakia matatizo,....hivi kama ulikua unafanya makosa na ukaamua kuachana na tabia hiyo ni lazima ukomfess,...mimi naona mtu unaweza ukaachana na upuuzi bila hata kuconfess.....rafiki yako kalikologa na inabidi alinywe hata kama ni ngumu kumeza
 
ameyataka mwenyewe sasa kinachomchanganya ni nini? Hivi kumbe mkuki kwa nguruwe eeh? Mwambie hayo ndo malipo yake. Atulie maisha yaendelee! Na wasirudie tn.
 
I repeat again, Waheshimuni wake zenu kwani wana akili nyingi kuliko hata zetu, mwambie atulie kwani alianza yeye, na zaidi sana mama anamzingua ili ampime msimamo wake. nawakilisha.
 
Back
Top Bottom