Mke mjamzito, nataka kukata bima NHIF ushauri

Sawa mkuu nimeelewa
Naomba kuuliza hivi taratibu za kulipa ni kwa pamoja au mtu unaweza kulipa awamu kwa awamu mana naona pesa ni nyingi hasa kwa sisi wa kipato Cha chini
Kabisa ngependa kujua pia
 
Sawa mkuu nimeelewa
Naomba kuuliza hivi taratibu za kulipa ni kwa pamoja au mtu unaweza kulipa awamu kwa awamu mana naona pesa ni nyingi hasa kwa sisi wa kipato Cha chini
Kabisa ngependa kujua pia
 
NHIF ina vifurushi vya aina nyingi ni kama unavyonunua kwenye simu hivyo ni vema kwenda kwenye ofisi za NHIF zilizopo karibu na wewe watakuelewesha
 
Kujifungua si gharama boss. Baada ya kujifungua mkatie bima mama. Mtoto wako atatibiwa bure hospitali yyte ya serikali mpaka miaka mitano. Nashauri bima ichukue atleast mtoto akiwa na miaka mitatu. Then mama ajikatie bima mwenyewe mtoto atakua beneficiary, kwasasa bima haitokusaidia kwa mwaka mzima.
 
Nilikuwa sijaona vizuri, kwahyo kutoka 192,000 mpka 432,000 kweli maisha yanakwenda kasi
Halafu kuna baadhi ya kima humu zilikuwa zinasapoti kauli ya yule rc mpumbavu aliyesema aliyekosa 50 akajifungulie nyumbani.
Eti akisema watu wakate bima, sijyi yule mpumbavu yuko wapi na simkumbuki jina.
Mtu analima, anafamya kibarua cha 5 kwa siku anaweza wapi kuimudu hii laki 4 ya pamoja.

Aje raisi apitishe sheria machawa wote wa kisiasa wahasiwe ama wanyongwe kabisa.
 
Mtoto kutibiwa bure hayo ni maneno ya siasa mkuu..
 
Mtoto kutibiwa bure hayo ni maneno ya siasa mkuu..
Hujawahi kua na mtoto wewe, hunielezi chchte na unaishi hapo hapo bongo. Na kama unae basi hufatilii mambo ya nchi yako, ww ni keyboard learner tu. Tembelea hospitali za serikali ujifunze, uone na huduma zinazotolewa. Tunawashinda hata sisi tulio ughaibuni kufahamu vitu. Au upo ughaibuni pia?.
Eti siasa, seriously?
 
Aliumwa nini mwanao maralia sio!! Haya subiri litokee zito(japo siombei, mungu amuepushe) ndio utaelewa.
Sasa kama mtoto anatibiwa bure unadhani kwanini watu wanahamasishana bima ya afya.
Nina watoto sio mmoja...
Picha linaanza mmoja wapo kazaliwa pale dodoma Benjamin mkapa, alipata manjano, unadhani alitibiwa bure, kitanda tu pekee ni elfu 50.
 
Mtoto wa umri gani?
 
Unaishi wapi? Kama upo hoi hahe kama mimi mambo yasiwe mengi nenda manispaa ustawi wa jamii kuna bima unalipa 40,000 tu lakini hauruhusiwi kutibiwa kwenye national referral hosp. Na ni bima kwa ajili ya hosp za serikali tu. Hilo ulizingatie. Mimi imeniokoa sana wife toka mwanzo wa ujauzito mpaka alipojifungua tar 19/1 na Hadi leo anaitumia hiyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…