Mke mlevi na mpenda starehe!

Mke mlevi na mpenda starehe!

Mpe pole sana Na kama kichwa cha family akae chini na mkewe amwambie ni vitu gani hapendelei na kama mwanamama yuko tayari kuacha waendelee na ndoa kama hayuko tayari basi amweleze yuko tayari kutoa talaka .
Akili inaweza kuingia kichwani na akabadilika .

namshangaa huyo mama kwa nini aliolewa

Kuna post nishaituma, jamaa kashafukuza anasubiri mahakama itoe tamko tu. Sina uhakika kama jamaa atamrudia yule dada maana hadi sasa jamaa hajutii kuachana na mkewe! Mie kinachoniuma ni mtoto tu, yani yule mwanamke anampa wakati mgumu mwanae kwa starehe za dunia za kupita tu.
 
hapo kwenye kabila la wapenda pombe ndipo sijapapenda kwani
atu wote wanaopenda pombe hawahusiani na hilo kabila na ingekua
hivyo baa zote zingejegwa huku migombani sahihisha hapo

Mkuu unaonekana ni mtu wa kujistukia sana, i guess sijataja kabila rather nimetumia fasihi, labda nikuulize we unadhani ni kabila gani nilikuwa naliongelea hapa? Maana watu siku hizi mmekuwa mashabiki wa ukabila. Post yote hii ulichoona ni 'watu wa migombani?' anyway waweza kuniambia wewe labda unadhani ni kabila gani?
 
FL1 wamama wengi tu waliolewa wanapenda starehe, tunakutana nao sana tu sema hawa hawafanyi wanaume zao wakiwepo wanakuwa na kaunafiki flani hivi ka kujifanya wema mbele za macho ya waume zao, ila mme akiondoka na yeye ni kula bata tu,tena kwa hawa wanaume wanaosafiri safiri au wanaofanya kazi nje ya nchi pole zao, mama hakuna part anayoikosa
marrykate kwa nini ufiche mama.?
Mie wangu wakati anapata hati miliki alijua kabisa my wife anapenda music ,kutoka out na viji mambo fulani fulani mara moja moja nk nk
kwa hiyo nimeingia ndani sina shida naangalia family kama mama na pia mara moja moja nikitaka kutoka hata kama yuko mbali namwambia naenda na marafiki wa kueleweka..
Hii kujificha ficha mtu unakosa mambo mazuri kisa usijulikane interest zako ni zipi?
 
Last edited by a moderator:
Huyo anajiendekeza mbona mimi niliambiwa niache pombe nikaacha kabisa japo sometimes nakumbuka napiga kareds tu ,narudi hm napulizia domo pafyum .ila sijamuudhi wamoyo.
 
Huyo anajiendekeza mbona mimi niliambiwa niache pombe nikaacha kabisa japo sometimes nakumbuka napiga kareds tu ,narudi hm napulizia domo pafyum .ila sijamuudhi wamoyo.

Thats how marriage works! Ila na wewe kwa nini mpaka alikukataza au nawe ulikuwa pampula?
 
Mh hii nayo chngamoto, Mhusika anatakiwa kuchukua uamuzi mgumu kwani kuendelea kuwa katika hali hii (mazingara ya stress) kwa muda mrefu kutmuathiri yeye pamoja na mtoto kama unavyosema na yeye kaanza kunywa pombe mwisho wa siku atajashindwa kumhudumia mtoto vizuri kinachotokiwa chapa mkofi piga talaka kwao halafu unajipanga namna ya kulea mtoto wako bila stress.
 
marrykate kwa nini ufiche mama.?
Mie wangu wakati anapata hati miliki alijua kabisa my wife anapenda music ,kutoka out na viji mambo fulani fulani mara moja moja nk nk
kwa hiyo nimeingia ndani sina shida naangalia family kama mama na pia mara moja moja nikitaka kutoka hata kama yuko mbali namwambia naenda na marafiki wa kueleweka..
Hii kujificha ficha mtu unakosa mambo mazuri kisa usijulikane interest zako ni zipi?

Ndo yule kakurupuka kwenda kili awards bila ya kumwambia mumewe! Unajua ni bora mwenzio afahamu unachopenda tokamwanzoni then achague kama utamfaa kuwa wife au demu wa kuzugia tu. Sasa unajifanya mtakatifu kumbe pampula? Waswahili husema mficha maradhi kifo humuumbua! Sasa unapiga ze ulabu ukilewa utaumbuka tu!

Halafu na wewe, hao friends wanaoeleweka ndo wakina nani? Maana mie mwenzenu nimechoka kuwaona wanawake watu wazima na matumbo ya vitambi wamejazana pale savannah lounge, wanalewa kama hawana akili nzuri, wanavuta masigara ili waonekane wana confidence, manyama uzembe yamewazunguka kiunoni kwa kunywa mabia na nyama choma! Wake za watu hao! Ah!
 
Last edited by a moderator:
Mh hii nayo chngamoto, Mhusika anatakiwa kuchukua uamuzi mgumu kwani kuendelea kuwa katika hali hii (mazingara ya stress) kwa muda mrefu kutmuathiri yeye pamoja na mtoto kama unavyosema na yeye kaanza kunywa pombe mwisho wa siku atajashindwa kumhudumia mtoto vizuri kinachotokiwa chapa mkofi piga talaka kwao halafu unajipanga namna ya kulea mtoto wako bila stress.

Your wish is his command, and thats what realy happened for sure!
 
Mshauri rafiki yako - ajitahidi kukaa chini na mkewe wazungumze.

mie naona hakuna maana yoyote yakuaa chini wazungumze maana tayari huyo muke amesha halibika kikubwa nikumtema 2 tena angalie asije kumletea magonjwa
 
Good news i may call it ni kwamba binti amekula BAN usiku huu, natoka kwa mshkaji, kamuomba mama yake aje kukaa na mjukuu, bidada amemuvuzishwa. Imeniuma na imenisikitisha kuona wanandoa wamefikia stage hiyo kila nikimuangalia mtoto naumia kama mwanangu vile. Nimepewa jukumu la kupeleka petition ya divorce ili wagawane mali na mambo ya custody of the child na mwanamke asepe zake. The guy seems a bit releaved hata tumechoma samaki kwake na ndio nimeondoka, kiukweli aliyonieleza ni mengi zaidi, yani jamaa ana kifua aisee. Kumbe ameshawahi kumfuma mkewe na njemba akawa halali na mkewe kitanda kimoja. Leo ndo ananionyesha chumbani kwake kulivyo na partition, dah, jamani ndoa hizi. Ila wamezinguana mpaka jamaa kamnyang'anya kila kitu mpaka mahakama itakapotna tamko although wao ni wakatoliki kwa hiyo tunaanza na kusikiliza baraza wanasemaje pamoja walishapelekewa hiyo kesi na wakaisuluhisha.

Its a shame for a marriage to end like that, lakini ni bora kutengana kuliko kuuana kwa magonjwa na kumuacha mtoto ateseke...mpe pole rafiki yako, Mungu ni mwema atampitisha salama kwenye haya mapito
 
Jana nilikuwa napata mbili tatu za baridi na jamaa yangu, katika maongezi akaniambia hana furaha ya ndoa yake. Mke wake ni anapenda pombe, analewa na watu mbalimbali anawaita 'friends', hana muda hata wa kutandika kitanda wanacholalia. Chumba chao dada wa kazi ndo anafagia, anafua, kupika na hata kutunza mtoto kwani mama hurudi mtoto akiwa amelala.

Pia kila sherehe anataka kwenda, amediriki kwenda hata kwenye Kili Awards bila ya kumshirikisha mumewe. Alipomuuliza anasema alikuwa na kaka yake, tatizo yote hayo hata ukoo wao wanapenda pombe sana. Kabila la wapenda pombe nadhani mnawajua wale wazee wa migombani walivyo!

Tatizo ni kwamba jamaa amechoka, mwanamke hashauriki, kaomba msaada hata kwao waongee na binti ila haijasaidia. Wana mtoto mmoja, jamaa ndio anahangaika kuwahi nyumbani japo akae na mtoto. Amefikia maamuzi ya kutaka kuachana na mkewe, jamaa ni msomi mzuri na ana kipato cha kujitosheleza, mke pia pamoja hana elimu ila ameweza kuendesha biashara ambayo mumewe alimuanzishia na inaendelea vizuri.

Tatizo mke ni mtu wa starehe za kulimbukia kwani wakati wanakutana hakuwa hivyo tena walikuwa na muda wa kukaa pamoja na kushauriana.

Nimeshindwa cha kumueleza japo nami nikaona labda mnaweza kutoa mchango wowote.

Nikusahihishe kidogo sio wachaga wote wanapenda pombe!!
 
Dah! hatimaye yamekuwa hayo...............Ukiolewa/oa jua upo kwenye hatua nyingine za maisha kabisa, usi-behave kama sharobaro au malaya...lazima uonyeshe tofauti.

Inasikitisha lakini maadam mume kavumilia na kuchukua hatua stahiki za mwanzo kuzuia ndoa kuporomoka dhamira yake sasa ni safi (angalau kwa taarifa tuliyopewa).

Hizi ndoa zina mambo ndio maana nafikiria mara mbilimbili kuoa!
 
Ni kweli mazee, ukioa au kuolewa lazima uonyeshe tofauti katika mfumo wa maisha yako, maana umeshavuka stage ya kwanza na umeingia stage ya muhimu katika maisha ya mwanadamu kwani hapo ndipo watoto huzaliwa ambao wao huwa wanajamii. Usipoonyesha kupevuka, kuna hatari ya kutengeneza jamii yenye maadili mabaya. Jamii yenye kupenda ulevi, ukahaba, kuzaa hovyo na kulekeza watoto, kupiga wanawake, jamii ambayo wanawake hawatafurahia uzao wao! Ni muhimu kubadilika sio kuvaa pete tu! Its more than that. Hata uvaaji, maongezi, marafiki, places you use to hang out sasa mme au mke wa mtu kila siku anakunya bia kona bar au jolly's tukueleweje na pete yako? Ah ndoa hizi.
 
Nikusahihishe kidogo sio wachaga wote wanapenda pombe!!

He! Mkuu umetoka wapi mbona fasta hivyo? Kuna sehemu nimemention kabila kwa jina? Au kwa kanda kuwa ni wale wa migombani kusi, kaskazi, mashari au magharibi? Mbona we unakuwa mtu mwingine tena kujihisi? Hebu pitia vizuri hiyo post then uniambie wapi na uthibitishe kuwa ni wachaga ndo wazee wa migombani pekee? **** wanyakyusa, wahaya etc etc etc! Lakini waweza kutoa ufafanuzi kwa nini umejihisi kuwa we mchaga ndo mpenda pombe! Labda utoe ufafanuzi kidogo although the main point hapa ni tabia ya huyo dada, kabila sio ishu hapa mkuu ndo maana sikuiweka hadharani.
 
  • Thanks
Reactions: Sal
Lazima kuna tatizo kubwa tuuuu, Either Jamaa hajui kutomba vizuri, au mke anapepo la ngono, Nashauri amwite waongee, awashirikishe wengine na awe makini hao marafiki wasije wakawa nyumba ndogo na wakamletea UKIMWI
 
Kwanza lugha umeitumia kali kidogo, lakini labda nikuulize; hivi kwa nini kila mwanamke akigombana na mumewe mnakimbilia kusema jamaa hachapi vizuri? Laiti mngekuwa mnaona hawa wanawake wanavyopindwaga hata mngewaonea huruma. Tatizo wakishatemwa ili aweze kujustfy ukahaba wake ndo hujisingizia eti hakuwa ananiridhisha kwani ukae miaka yote hiyo leo ndo useme? Hawa watu huwa wanapindwa mpaka unadhani atavunjika na harudii tena, ila utashangaa na kesho anataka! Ishu hapo sio kupinda mie nadhani ni tabia mbaya ya mwanamke.
 
shida ni kama mtu anaumwa, au ukata umetawala nyumbani, sio mtu unapombeka mpaka mausiku with so called "friends" halafu unaseme shida na raha... bull shit...
piga makofi ya kutosha, kesho atajua ana mume na mtoto na atajua kazi zake na zipi na za house girl ni zipi. mwanamke gani umeolewa halafu kutwa unarudi unanuka mipombe kitandani wakati mwenzio yuko sober.
apeleke umigombani wake huko kama yeye starehe kaziona ukubwani. hana haya hata kidogo.

Aliapa kanisani siku ya ndoa yao kwa shida na raha,ndo shida zenyewe hizo..pole yake!
 
Ndo yule kakurupuka kwenda kili awards bila ya kumwambia mumewe! Unajua ni bora mwenzio afahamu unachopenda tokamwanzoni then achague kama utamfaa kuwa wife au demu wa kuzugia tu. Sasa unajifanya mtakatifu kumbe pampula? Waswahili husema mficha maradhi kifo humuumbua! Sasa unapiga ze ulabu ukilewa utaumbuka tu!

Halafu na wewe, hao friends wanaoeleweka ndo wakina nani? Maana mie mwenzenu nimechoka kuwaona wanawake watu wazima na matumbo ya vitambi wamejazana pale savannah lounge, wanalewa kama hawana akili nzuri, wanavuta masigara ili waonekane wana confidence, manyama uzembe yamewazunguka kiunoni kwa kunywa mabia na nyama choma! Wake za watu hao! Ah!

marafiki wa kueleweka si ndo hao hao jamani
hata ukimwambia mwenzio niko na fulani na fulani hana hofu..
Sio ukimtajia niko na Carina anachanganyikiwa huko alipo na kukosa amani
 
Hizi ndoa..!!! hadi mwili umenisisimka! acha saa 4 au 5 usiku, mke wa mtu saa 2 usiku hujarudi nyumbani bila sababu ya msingi..!!! hata kama ni foleni za Dar, wenye upendo huwa wanasubiriana. hata kama kila mmoja ana gari lake, mnangojeana mahali wote mwende nyumbani pamoja. labda kama mnatoka wrong direction lakini mtu utajua kua mke wangu kazi yake inamchelewesha na mume ataelewa.
hivi wanawake wanaolewa ili wavae shela au waonekana na zile pete mbili kwenye kidole japo nafsi inakataa?? mke wa mtu ana nyumba ndogo...!!! halafu inakuleta hadi mlangoni kwa mumeo. hata hao wanaume wanaowachukua nao wana roho ya chuma.

Tatizo hili limewahi kunikumba. Tena hivyohivyo kama ulivyoeleza. Akilewa anasema alikuwa na ndugu. Tukawa tunagombana sana, nampiga. Nikimpiga kosa linageuka kuwa la kwangu. Naulizwa kwa nini nimempiga nikawa nakosa sababu ya maana. siku moja nikaamua kwa dhamira kabisa, sitampiga tena. Akaongeza muda wa kutorudi nyumbani mapema. alikuwa anarudi saa 4-5 usiku sasa ikawa saa 6-7. Nikaa kimya kabisa, nilikuwa nimedhamiria hasa. Siku moja akarudi saa 7 usiku nikamfukuza chumbani. Kwa taratibu za kwetu ukimfukuza mwanamke chumbani na msipoyamaliza wenyewe, usipomrudusha anatakiwa kukushtaki kwa ndugu au familia ili uulizwe sababu ya kumfukuza. Bila kumpiga. Hakuenda popote kwa miezi 3 akawa analala chumba cha pili. Siku moja wakati narudi zangu home nikamkuta kaletwa hadi home getini anakula denda saa 6 usiku. Waliponiona akateremka kutoka kwenye gari lililomleta. Nikampeleka kwa dada yake jirani na mimi nikitumaini kuwa safari hii kesi itakuwa nzuri kweli kwangu. Nikasuburi siku ya kwanza .... mpaka leo mwaka wa sita hajasema sababu iliyofanya nikampeleka kwa dada yake.
Maoni yangu kwako, hana maana huyo, mtafutie sababu umfumanie umfukuze, hiyo ndio sababu kubwa. Ulevi na satarehe sio sababu tosha. Huenda na wewe unastarehe.
 
Back
Top Bottom