Mke na Mama

Aisee kama ni mimi sidhani ningechukua muda mwingi kuumiza kichwa....mama anaumwa na anataka kuja kukaa kwangu....mke hana muda wa kujadili hilo bali ni kuandaa mazingira ya kumpokea mkwe..kama alinipenda mimi atapenda na ndugu zangu pia. imagine angekuwa ni mama yake anaumwa angekataa?
 
1.mama ni muhimu akae nawe kama anavyotaka,ni wakati wa kuvuna baraka.
2.mkeo, nae ni muhimu akubali mama awepo.
Wewe ndio unapaswa kuhakikisha hayo yanatendeka.....changamka mkuu.
 

dah, umeni convince mpaka nimemchukia huyu mke...
sawasawa kaka, nimekuelewa. Huyu mke wa mheshimiwa
kwakweli amekosea.
 
Wanasema´Ukipenda BOGA penda na ua lake´ Mama una mmoja tu.
Hutampata mwingine popote pale, ila mke utampata popote pale na wakati wawote.

Kuwa na Busara mkuu.
Inahitaji uamuzi mgumu ndugu.
Lakini jipe Moyo uyashinde majaribu.
 

dah, umeni convince mpaka nimemchukia huyu mke...
sawasawa kaka,
nimekuelewa. Huyu mke wa mheshimiwa
kwakweli amekosea.

Yap!....hizi porojo na siasa za mapenzi sometimes hazilipi sana,...inakua kama unaidhulumu nafsi i.e unataka mama yako apone at the same time unataka eti mwanamke wako akuone unamjali na kumskiliza_ingawa ni sawa mwanamke anastahili kujaliwa,kusikilizwa,kuheshimiwa n.k lakn sio kwa mambo kama haya kiongozi wangu.
 
Reactions: Mbu
Muombe sana Mungu atakusaidia katika hili...

Mama ni Mungu wa Pili na Mke ni Muhimu saka kwa sababu ni ubavu wako
kaeni muongee muelewane
 
Reactions: Mbu
Mwambie akipenda boga apende na ua lake....
 
Labda mkeo kagundua mama yako anapretend anaumwa, na anataka aje kwako kukugombanisheni muachane. Mie nawajua mama wake tabia zao kwa watoto wao wa kiume. My mother ndio mchezo wake pia kupretend anaumwa ili akafuruge ndoa za watoto wake wa kiume, sababu hajawapenda wake za watoto wake. Hata mie sijaipenda hizi tabia za mama zetu, ndio maisha. wewe kama dume, usimuache mke wala mama hapo, kuwa makini hapo
 

Yawezekana mama yako haumwi kweli na pia huko nyuma alikwisha wahi kukaa kwenu na kumfanyia visa mkeo.Kuna wamama wengine ni washari mno kwa wakwe zao.
 
Igwe usikurupuke namna hiyo kaka. Ukijibiwa hiyo nyumba ni ya mke, utasemaje?Busara zinahitajika zaidi kwenye hili kuliko povu. Kila nyumba inahitaji busara zake.Kuombana ushauri ndio desturi za waungwana.
Kaka hata mimi nilitaka kuingia kichwa kichwa, ulilosema linaukweli sana. Inabidi jamaa utujuze zaidi anaishije na mke wake, lakini ukweli unabaki vile vile Mama ni muhimu sana sasa kama mke hampendi Mkwe hafai kabisa tena ni Sumu kabisa.
 
Jenga hoja ktk uhalisia wa Mada usii-dilute utapoteza maana.
 
Wadau mama anaumwa na anataka kukaa na mimi,mke wangu anasema hana furaha kukaa na mama nyumba moja,nimechanganyikiwa nishaurini,nimuondoe mamam au nikae nae na mke wangu hatakuwa na furaha???

Nisaidieni wajameni.

muuguze mama utakavyo.... heee mwanaume unakosa maamuzi...
 
Mkuu hii story imeanzia mbali inawezekana wana tofauti zao mke na mkwe, we ongea na mkeo mama aje kujiuguzia hapo akipona asepe. Bibie apunguze makali ,mtibishe mgonjwa!
 
acha kuwa na mawazo ya pimbi, unawezaje kumuuliza mama yako sababu za kutaka kuja kwako? Inshort ni kwamba mama yangu ana thamani kubwa sana, mama ndie mtu wa karibu zaidi na mwanae, ukimpenda mama wa mumeo ni sawa kabisa na kuonyesha unamjali mumeo! Ukishaoa mwanamke anakua sehemu ya familia ya mume ndo maana kwao aliagwa na send off na mahari ukatoa hivyo anao wajibu wa kukusaidia kumtibu na kumhudumia mama yako maana mke ni msaidizi wa mume. Pia mama hawezi kuwa na mipaka ya kuja kwa mwanae hata kama haumwi as long as unaouwezo wa kumu accomodate bila shida. Kama unao uwezo wa kumsaidia mama yako na mke anakuwekea pingamizi kwa upande wangu mke atakua hanifai kwanza unatakiwa ujue kuwa moja ya sababu za kuoa ni mke kukusaidia majukumu yako na sio mapenzi tu. Kumtunza mama yako ni wajibu wake kabisa.
 
kwanza unaweza kufindout ,,kwann mkeo ,hataki kukaa na mama yako?,pia kuna baadhi ya wanawake wanakua wanajenga fikra kua wakwe n wabaya kiasi ambacho bila ya mama asinge kua na wewe saiv ,,mama ni muhimu kuliko chochote ,, yaani yeye ni mwanzo, ktk maisha yako yoote usijaribu kumdharau,,mlee mama yako na mfariji kt k shida na ugonjwa,hakuna fadhila yyte ambao utaweza kulipa mama aliyo kutendeaa, nakuomba kaa na mama yako ,, mungu atakufanyia wepesi na kua muangalifu ,na zungumza na mkeo ,muelezeee kama yule ndio aliye kuleta ktk hii dunia, na ndio ukawa nae yy ,, awe mstahamilivu ,mushirikiane,, ihope utanielewa kidogo
 
unajua bro what goes around what comes around,,, utakapo kuja kumtendea mzazi wako sio haki ,bealive me,, one kizaz chako kitakuja kukutendea,, kuna watu wanapo kua na familia zao au pale wanapo jiona wako already mature basi wanawaona wazaz wao saa zote wana makosa howcome una msema mama yako kama anataka kukuachanisha na mumeo au mkeo ,, unagundua kua mzazi wako kama fanya makosa tumia njia ya hekma ya kumuelewesha mzazi wako ,, yule sio kusema ovyo ,mzaz anatoa radhi ,, n mke hatoi radhi ,, kusema la haki hakuna mkamilifu, kila mtu ana udhaifu ,but use common sense kumuelewesha wife na ikiwa mama na yy utamuona kfanya wrong pia,but kaa na mama yako,, hakuna mama wawili only one,, naandika sana bcz mm mwanamke but napenda haki,, nishaona hayo mambo,
 
Huo ni mtihani mkuu! Kuna mambo yamejificha hapa. Pengine mke wako ni roho mbaya, pengine mama ni roho mbaya, pengine mke na mama hawapatani, paka na moshi... Lakini mwisho wa yote, mama ni mama. Kama haiwezekani kusuluhisha tafaouti baina ya mama na mke, na kama hakuna budi kabisa, mpe mapumziko ya muda mke aende akapumzike nyumbani. Badae tafuta "dada wa kazi za nyumbani" umwajiri kukusaidia kuuguza mama yako, akishakupona...arejee alikotoka! Pengine huu ni uamuzi wa "kimsimamo mkali", lakini ukifanya hivyo utajua kile kinachojificha ndani ya nafsi ya kila mmoja. Mke atakubali kuondoka ili uuguze mama yako? Mama atakubali kukaa nyumbani na dada wa kazi?
Ni mawazo tu, nilichotaka kusema hasa, POLE SANA MKUU.
 
NAWASHUKURU SANA WADAU WOTE KWA USHAURI MLIONIPA.LAKINI NISEME TUU NIMEFURAHISHWA NA JINSI MNAVYOTOFAUTIANA KWENYE USHAURI WENGINE MMESEMA NITUMIE NGUVU KUHAKIKISHA MAMA ANATIBIWA NA KUKAA KWANGU WENGINE MMESEMA MKE YUKO SAWA NA WENGINE MMESEMA NI MIMI KUONYESHA MSIMAMO,HAYO YOTE NDIO YALLIYO KICHWANI KWANGU.


kwa ujumla nawashukuru sana

MAMA TAYARI YUPO KWANGU NA MATIBABU YANAENDELEA JAPO HAMNA RESPONCE NZURI KWA WIFE
 

Good,....muuguze mama_achana na response ya mkeo kwa sasa,....mama akipona ndio heri yako mkuu......
Well done
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…