Mke Ukiachika, Ukapata Bwana Mpya, Ni Sawa Kumzungumzia Bwana wa Zamani Kila Uchao? Wanasiasa Hamahama, Wanachofanya ni Sawa Kuponda Tuu Walipotoka?

Kila mwanachama wa Chama cha siasa ana kazi ya kufanya kwa mujibu wa katiba ya Chama hicho.

Utekelezaji wa majukumu ya Chama Hata kama umehamia hivi punde yapo palepale kwa mwanachama. Sasa kwa utaratibu w Chama katika kutekeleza majukumu, mwanachama unaweza kupewa wajibu wa aina yoyote!! Na kama ni mtiifu wa Chama utayatekeleza mara moja wajibu huo.

Kwa msingi huu, sikubaliani na katazo lako mleta mada dhidi ya wale wanaohama vyama kutokutekeleza wajibu wao katika vyama vyao vipya. Badala yake jicho lielekezwe kule ambapo wanachama hawa wamehama Kuna Changamoto gani kiasi cha kupoteza wanachama.

Nakaribisha ukosoaji wa hoja yangu.
 
Mchungaji Msigwa amekosa Uenyekiti wa Kanda ya Nyasa Ndio kaenda CCM kutafuta Vyeo

Ni Mtu mjinga tu asiyeona hili
 
Hao ndo Wanasiasa Malaya (harlots) ambao Mzee Nyerere alisha wasema muda mrefu sana.pia hiyo ni ishara ya kuishiwa hoja na kufilisika kisiasa.Bure kabisa
 
Tangu lini Mbowe amekuwa kiongozi wa taifa? Kama wanachama wa chama chake bado wanamkubali basi sisi wengine hata tuseme nini ataendelea kuwa Mwenyekiti wao. Njia pekee ni nyie ambao mumemchoka ni kujiunga na chama chake na kuwashawishi wanachama wenzenu wamkatae.

Humu ndani watu kibao wanasema wameichoka CCM lakini inaendelea kudunda tu. Njia pekee waliyokuwa nayo ni kukiondoa madarakani. Wakikitoa madarakani ndio itakuwa mwisho wake tofauti na vile vyama ambavyo havijawahi kushika dola.

Amandla...
 
naunga mkono hoja, watu hawa tuliwashauri humu
p
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…