Mke usimpande kichwa Mumeo

Mke usimpande kichwa Mumeo

Amos David Mathias

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2022
Posts
1,576
Reaction score
3,094
Wanawake wengi wa sasahivi wamekuwa ni pasua kichwa katika familia zao.Wanafanya mambo ambayo yanachochea UGOMVI na chuki Kila mara.

Hawana heshima Kwa Waume zao sababu hawajui thamani ya mume.Hawataki kujitiisha mbele za Waume zao na kuwaheshimu Bali wanataka wawatawale hali ambayo inazua taharuki na tafarani katika ndoa.

Ndiyo maana asilimia 98.9 ya wanawake wanaenda Kwa waganga Ili wawaroge Waume zao Ili wawatawale na kuwapelekesha kama mazezeta. Sijui niseme Wanawake wamesahau majukumu Yao katika ndoa ya kuwa wasaidizi wa mwanaume ikiwemo kufanya kazi ya nyumbani na kuwalea watoto Badala yake wamekimbilia majukumu ya mwanaume ya kutawala na kuiongoza familia.

Nataka niseme tu hakuna mwanamke mwenye uwezo wa kuiongoza familia Kwa ufanisi kama mwanaume.Familia nyingi zinazoongozwa na mke huku mume yupo zimeishia pabaya sababu wameruhusu mpango wa shetani katika familia wa mwanamke kushikilia usukani wa kumtawala mwanaume.

Ifikie hatua wanawake mjitambue mrudi kwenye asili yenu ya kweli ya kuwa wasaidizi wa Waume zenu na sio kutaka kuwa kama wao.Tatizo linaanzia pale mwanamke mjinga anapotaka kujilinganisha na mwanaume na kuacha uanamke wake.

Biblia inakataza Mwanamke kumtawala au kumfundisha mwanaume.Hii ni dhambi na mwanaume anayeruhusu kutawaliwa na mwanamke katika familia naye ashiriki katika hii dhambi pia.

Someni 1 Timotheo 2:12mpaka 13 .

Wanawake watapendeza ikiwa hawatakuwa watu wa kupayuka payuka na kuwapigia makele wanaume wao Bali itakuwa vyema na kupendeza ikiwa watakuwa watulivu na wenye heshima katika ndoa zao.Wawe na busara katika namna ya kuwaendea Waume zao yanapotokea matatizo wasiwapigie makelele Wala kuwapayukia au kuwa uchungu katika mioyo Yao Bali wayatatue wakiwa wapole na wanyenyekevu .
 
Nimeoa ila nakushauri kataa ndoa ni ubatir mtupu na wizi, ni wiki sasa hatuongeleshani, suruhu hadi nimnunulie zawadi,...pole yangu 😥😥😥

usiposikia utajuta
 
Wanawake wengi wa sasahivi wamekuwa ni pasua kichwa katika familia zao.Wanafanya mambo ambayo yanachochea UGOMVI na chuki Kila mara.
Mwamba hao kwa karne hii hawawezi tena kujitambua, wameshakuwa wanaharakati na shetani ndio ameshashika akili zao, nyuchi zao wameshaona ni madini muhimu.

Chakufanya. Mimi nakataa ndoa za garama, weka pisi ndani akizingua tupa leta mwengine. Wapo wengi sana hao.
 
Wanawake wengi wa sasahivi wamekuwa ni pasua kichwa katika familia zao.Wanafanya mambo ambayo yanachochea UGOMVI na chuki Kila mara.
ki katika hii dhambi pia.

Someni 1 Timotheo 2:12mpaka 13 .

Wanawake watapendeza ikiwa hawatakuwa watu wa kupayuka payuka na kuwapigia makele wanaume wao Bali itakuwa vyema na kupendeza ikiwa watakuwa watulivu na wenye heshima katika ndoa zao.Wawe na busara katika namna ya kuwaendea Waume zao yanapotokea matatizo wasiwapigie makelele Wala kuwapayukia au kuwa uchungu katika mioyo Yao Bali wayatatue wakiwa wapole na wanyenyekevu .
Ukweli ni kwamba wanaume ndio tumekua dhaifu ndio maana wanawake wanaonekana hivyo usemavyo. Sio kwamba wanawake hawataki kujitiisha kwa wanaume ila ni kwamba hawajisikii amani kujiachia mbele za wanaume, hasa wanaume dhaifu. Kiasili mwanamke ni mtiifu na anapokutana na mwanaume mtawala hujiachia kwake kwa sababu anajua yupo salama.
.
Wanawake wengi sikuizi wanaenda kwa waganga, au hata kubadilisha makanisa kila siku, kwa manabii ili wapate kujisikia ile hali ya kuwa chini ya kitu kinachompa changamoto. Kuna kitu wanakikosa kwa wanaume wa sasa, ambacho ni uongozi, kiurahisi anaenda kuupata uko japo kwa macho ya kawaida unaweza kuona kwamba wameenda kutafuta limbwata au kuomba kitu.

Mwanamke ambaye anaridhishwa na mwanaume wake kiroho, kiakili na kimwili ni vigumu kumkuta huko na hata akienda ni mara moja moja sana.
Ila tukisema wanawake ndo wachukue hatua na kubadilika, tutakua tunatwanga maji kwenye kinu sababu inajulikana mabadiliko yoyote yanaanza kwa kiongozi na kiongozi ni mwanaume, hivyo ni jukumu letu sisi kama wanaume kuchukua hatua na kuanza mabadiliko, wanawake watafuata tu na wote tutafurahia matokeo.

Mwanamke hataki kuchukua nafasi ya uongozi ya mwanaume ila sababu wanaume tumezubaa basi mwanamke ndio anajilazimisha kuuchukua uongozi ili jamii kiujumla isivurumuke kwa kukosa uongozi.
Vituko vingi wanavyofanya wanawake ni ishara tu kwamba kuna sehemu umelega na tukaze.
.
Cha kufanya sisi kama wanaume tuache kulaumu wanawake, tuanze kuchukua hatua. Tuchukue nafasi yetu ya uongozi. Maswala ya 50 50 kwamba na wenzetu nao inabidi wawe hivi tuyaache, tujiangalie sisi na kujiendeleza zaidi kuwa bora zaidi na kuwa viongozi.
 
Wanawake wengi wa sasahivi wamekuwa ni pasua kichwa katika familia zao.Wanafanya mambo ambayo yanachochea UGOMVI na chuki Kila mara.
Ukiona mwanamke anamdharau mwanaume, mara nyingi sana shida inakua kwa nwanaume. Na kurudisha heshima kwa haraka ni rahisi mnooooo kuliko unavyofikiria.

Wanawake hua wanatest wanaume. Na hata wao hawapangi kuwa wamtest mwanaume, wanajikuta tu wameshamtest mwanaume.

Ukipewa test ya kwanza ukafeli, mwanamke anaanza kukushusha thamani taratibu. Mpaka ikifika mwanamke akakufokea kama mtoto, anakudharau na kukutuma ukapakue mboga jikoni mbele ya wageni, akakuonesha kiburi mbele ya watu, ujue ulipewa test nyingi na ulifeli vya kutosha, anakuona bozo, bwege la mwisho.

Asa ili kukwepa hili la kudharauliwa, kuna mambo ya msingi ya kufanya:
1. Kujua test zao zikoje
2. Kujua kama anakutest ama la
3. Kujua kama anakutest ufanyeje ili ufaulu.
 
Back
Top Bottom