Mke wa Dk. Slaa awa kivutio mkutanoni

 


Gaga una mashida makubwa sana mkuu .Kwa mfano kama Slaa mke wake angelikuwa Muislam na yeye Mkristo na wameamua kuishi kwa imani zao zilivyo na bado Slaa akawa mchungaji mkristo ana hubiri Ukristo ungalisemaje ?

Swala lao la msingi ni ndoa ambayo ina kanuni moja kwamba Slaa ni dume na Mume wake na yule ni Mke now imani zao katika vyama is not an issue to me .Leo Rose Slaa anatoboa juu ya wizi wa CCM huko waliko na ndani ya CCM the same thing being done by Slaa , nina amini kwamba wangalikuwa wote CCM nia ile ile njema ya kuwatetea Watanzania wa Jimbo lao na kata yao na Watanzania wote kupitia Bunge ingalifanyika .
 
Kweli halifichiki pembe la ng'ombe.... Mrs Slaa ni msanii wa nguvu sawa na mumewe .....
 
Kiongozi shurti awe kioo. Kama Dr anasimama jukwaani kutuhimiza kuwaunga mkono kwa kuwa CCM inaendeleza uoza huku akishindwa kumshawishi mkewe binafsi naona kama kuna tatizo. Call it democracy or anything !

Kuna tatizo kwa base ipi hiyo, maana sio kisheria sasa on what base?
 
Mkuu FMES,
Tatizo lililopo ni la kisiasa kwani mke wake anakuwa sehemu ya mafisadi walewale kulingana na kaulimbiu ya chama.
 
Tatizo lililopo ni la kisiasa kwani mke wake anakuwa sehemu ya mafisadi walewale kulingana na kaulimbiu ya chama.

Mkuu Gee,

Ni kwamba sio wanachama wote wa CCM ni mafisadi, na sio kwamba viongozi wote wa CCM ni mafisadi kuna baadhi ya viongozi na wanachama wa CCM ambao ni mafisadi. Kauli mbiu ya chama chochote cha siasa Tanzania, sio lazima iwe ni ukweli wa siasa wa taifa, ni kauli mbiu tu ya kile chama cha siasa,

kama kuna tatizo lingine la DR. Slaa na mkewe, lisemwe tu tujue lakini hatuwezi kujificha nyuma ya a couple kua na itikadi tofauti kama kigezo cha uaminifu wao kwa vyama vyao vya siasa na taifa, au kwa sisi wananchi, that is asking for too much kutoka kwa wananchi kama sio viongozi.
 

Wananchi itabidi wapigwe msasa kuhusu Partisan na Bi Partisanships...
 
Mushi,
Hilo zoezi la kutupiga msasa kwa Bongo linaweza kuwa gumu kuliko unavyofikiri.
 

Mkuu FEMS,
Sidhani siasa kuifanya iwe ajira ni jambo baya au ni kwa vile mtu hana ajira nyingine. La hasha, ni uamuzi tu anapoona kuwa siasa ni ajira bora zaidi kuliko nyingine. Pengine ni kwa kupenda kuihudumia jamii au ni kwa maslahi binafsi. Lakini kilicho wazi hapa ni kuwa wote, Dr. & Mrs. Slaa wameamua kuacha mengine yote, including utumishi kanisani, na kuifanya siasa iwe ndio ajira yao kuu.


Chama ni ideology, kwa hiyo kabla ya Dr. Slaa kunyimwa nafasi CCM, ina maana alikuwa hakubaliani na siasa za CHADEMA. Kwa hiyo kwa yeye kujiunga CHADEMA ni reaction ya yaliyomkuta CCM na sio kuwa alishabihiana na agenda za Chadema. Alifanya jambo zuri kwani alielewa walichotaka wananchi, lakini haukuwa uamuzi wa kiitikadi.


Kwenye migogoro ndani ya vyama itategemea uko upande gani. Kama yupo katika upande wa kuiminya demokrasia, kama walivyofanya walipomsimamisha marehemu Wangwe uongozi, basi kuna haki ya kuwajibishwa na wanachama na wapigakura wake.
 

Mkuu FMES,
Kwanza naomba tuondoe mawazo ya kuwa, mwanasiasa anapodadisiwa ni sawa na kum-abuse. Ni muhimu tukadadisi yote yaliyopo machoni petu ili watakapofanya maamuzi tuwe tunaelewa ni hisia zipi zilizowapeleka kwenye hayo waliyoamua. Dr.Slaa sidhani kama alikuja humu mtandaoni kuhubiri tu na sisi tuwe wasikilizaji. Tupo wengi wenye mawazo tofauti naye ambao tungependa ayasikie hata kama yatakuwa yanamhusu yeye binafsi. Naomba tuachane na mawazo kuwa kwa vile yupo humu, basi awe immune from critisism.

Ni vizuri tunapompa zana za kufanyia kazi yake bungeni, majukwaani n.k., lakini pia tumuweke kiti moto kwa yale yanayomhusu. He is still a political figure just like JK, Lowassa, Mtikila etc. Hatuhitaji atujibu tunapotohoa background yake na ya spouse wake, lakini tusiache kufanya hivyo katika jitihada zetu za kumuelewe vema, kwa vile tu ni mwenzetu humu JF.
 
Kithuku,

..kweli kabisa, Dr.Slaa ni msanii.

..hebu fikiria alivyokuwa akimuandama Sumaye kwa "kashfa" ya kukodisha shamba la eka 7 kibaigwa, wakati Mkapa na Yona wamejinyakulia kiwira.

..katika listi ya mafisadi hajamtaja mu-Iraqw mwenzake Dr.Idiris Rashidi[former governor wa BOT].

..upotevu wa fedha BOT ulianza wakati Dr.Rashidi akisimamia fungu la fedha za misaada toka Japan. kamati ya Bunge iliyoongozwa na Edward Ayila ilipendekeza Dr.Rashidi achukuliwe hatua kali.
 


POINT of Wondering


Juzi ZITO kule tarime aliwataka wana taarime wasichague chama cha mafisadi CCM.
 
 


Kwanini umtake Kuhani awe mwandishi? Yeye kuonyesha mfano ndiyo itasaidia vipi, mbona mifano ya kuigwa ipo mingi sana. Halafu vacuum ya critics itajazwa na nani? Unaweza ku-criticize kauli zake ukitaka; that way we will benefit.



"Mimi siipendi kabisa Chadema na kwenye eneo langu la udiwani nahakikisha wafuasi wa CCM hawarubuniwi kuhama. Lakini nipo pamoja na Dk. Slaa katika suala zima analofanya la kufichua mafisadi," alisema Kamili.


Pengine kuna kitu huyu mama alitaka kutuambia. Hata mimi amenichanganya.



.
 
Nafurahi sana mada kama hii inapotokea JF kwa kuwa inatuwezesha wengi wetu wenye uchungu wa kweli kweli kuwagundua wanafiki kwenye hii vita ya mustakabhali wa taifa. Unaposukumwa na wito wa kuitendea mema nchi yako, bila shaka swala la chama linatakiwa lichukue nafasi ya pili. Mbunge ni mwakilishi na mteteaji wa wote bila kujali itikadi na kama hili lingezingatiwa, Tanzania tungekuwa tunapaa haswa.

Mtu akihamasika na akashawishika kuwa ana nia, sababu na nguvu za kuweza kushiriki kikamilifu katika harakati za kuleta mabadiliko kwenye mfumo wa uendeshaji wa nchi, anajiunga katika siasa. Hivi sasa sheria zetu tuliojiwekea wenyewe ni kuwa ili ugombee nafasi yoyote ya kisiasa lazima utokane na chama cha siasa. Sasa kama chama chako kimekunyima hii fursa kuna mawili - ujiunge na chama kingine ufanikishe malengo yako ama ubwage manyanga kama wengi wanavyofanya na ubaki tu mpiga debe.

Kwenye nchi zingine ungeweza kugombea kama mtu huru asiyefungamana na chama chochote na ukiwa na ushawishi wa kutosha utapeta tu. Tatizo la Tz ni kuwa mara nyingi hatuangalii uwezo wa mtu bali tunajali anatoka chama kipi na matokeo yake hatupati viongozi bora bali bora viongozi. What a shame !! Tunashindwa kuelewa kuwa hakuna chama chochote cha siasa kisichoitakia Tanzania mema kwenye malengo yake. Chama chenye viongozi wabovu huishia kutetea ufisadi kwa kuwa kinategemea ufisadi kubaki madarakani.

Adui mkubwa wa giza ni mwanga na kwa kuwa maovu mengi yanatendeka gizani, watu kama Mh. Dr. Slaa wanakuwa mwiba kwa ufisadi kwa sababu wanaleta mwanga. Kama matendo kama ya Dr. na Mama Slaa ni usanii sidhani kama huo mwanga ungemulika lakini tulio na macho tunauona ati. Si ajabu watakuwapo kundini wasiouona na hapa ndipo kuna usanii wa kweli kweli ama wamevaa vitambaa vyeusi usoni?
 

Utafanya kosa la karne kujaribu kumwamini MWASIASA anapoibua UOVU wa mwanasiasa mwenzake.

Pila utafanya kosa la karne kujaribu kuamini ama kumtafsri mtu kutokana na maandikp yake badala ya matendo.

Mimi ningekuomba unieleze ILANI ya hao wapiganaji iliyowaingiza 2005 bungeni ni mangapi wameyatekeleza waliyo waahadi wananchi ktk majimbo yao?
 
Sadakta muungwana.Hapa si suala la usani hapa ni fedha za wananchi zinatumikaje.Kama ni usanii basi usanii wa Dr Slaa na Mkwe ni mzuri .
 
Kakweli nimeshindwa kuona point ya msingi ya kumshambulia DR. slaa kwa sababu yeye na mkewe wana itikadi za siasa zinazotofautiana, naomba kunawa mikono hapa maana sioni elimu hapa zaidi tu ya ku-showoff.

Dr. Slaa naomba tu uelewe kuwa kuwa kuna tunaothamini uongozi wako shupavu usio yumba na wenye faida kubwa kwa taifa letu, hasa sisi wanyonge wa Tanzania, na Mungu akupe nguvu na maisha marefu zaidi uendelee hivyo hivyo bila kuyumba.

Ahsante Wakuu.
 

Sio kweli, wapo wanasiasa ambao ni committed kama Dr. Slaa, Hon. Zitto na the likes pia wapo wanasiasa ambao ni wasanii, wanajulikana hakuna haja ya kuwataja. Msanii anajulikana kwa maneno na matendo.

Mungu ibariki Tanzania
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…