Mke Wa Dr. Salaa Josephine Alonga Na JF

Status
Not open for further replies.
Toka lini kuwa na Kimada au kupora mke wa mtu kwa viongozi wa afrika uikawa issue,acheni hizo mbona hata huku CCM wapo kibao,jaribuni kwenda pale dodoma wakati wa mikutano mikuu ya CCM ndipo utakojua kuwa hakuna mwadilifu

Wale wale wanachukua uchafu wa watu wengine kujustify uchafu wa mtu mwingine. Yaani ni sawa kwa rais mtarajiwa kupora wake za watu? Sijui Watanzania tutajifunza lini.
 
=======

Watu wengine bwana! Mlinzi wa Zuma kazaa na mke rais Zuma haikuwa nongwa.
Mwinyi alikuwa na watatu mpaka wakati wa safari inabidi tumwulize nani yuko zamu, haikuwa nongwa.
Mama Maria alikaa Nyegina (Tarime) miaka 5, haikuwa nongwa
Mama Graca aliacha kaburi la mmewe Maputo kaenda J'burg kuwa FL haikuwa nongwa

The fact kwamba hii inafanywa kuwa issue, kuna mawili:
-CCM wanaona taa nyekundu wakati kwa Dr. Slaa kuna kijani
-CCM wameishiwa ya kusema, na sasa wanatumia meno katika mchezo wa ngumi.

Wameshauriwa vibaya maana hii wangeisubirisha angalau wiki 2 kabla ya uchaguzi. Itawageuka.
 

Hata mimi nimekuwa nikijiuliza mbona hawakumhoji Dr Slaa na "mke wake" kabla ya kupublish hiyo habari? Bila hata kujadili kama habari yenyewe ni ya kweli au uongo, kwa uandishi bora wa habari hawa watu ingebidi nao wahojiwe na mwandishi aliyeandika hizo habari.
 

Ndoa yake haikusababisha matatizo ya watanzania lakini inaweza ikasababisha matitizo zaidi kama akiwa rais. Ndio maana tunaka kusikia ukweli wa ndoa yake. Ndoa yake ilistop kuwa ya binafsi pale alipotangaza kuwa mgombea wa rais. Nikiwa kama mpiga kura lazima nipate ukweli toka kwake kama kweli yeye ni mwizi wa wake za watu nor not and why. Tunataka watu waende ikulu with clean hands. Ni ngumu but we have to acknowledge and start practicing this.
 
Wanaume wengine kwa kujidhalilisha bana, wewe Mwanamke Hakutaki na amesema Jukwaani kwamba Hakutaki sasa ya nini Kilia lia Jamani? Tena Kwenye Vyombo vya Habari Mwanamme Mzima unaenda Kulia kwamba Jamaa kaninyang'anya Mke ili iweje sasa, wewe unafikiri Serikali inaweza kumuamuru Akurudie, Ebo

Huyu Mwanaume Hovyoooo Kabisa ni Heri Hata akakaa Kimya kwa Sababu hata Hatujui Sababu ya Kuachwa inawezekena Mzee Hapigi Mashine sasa unatakana nini?
 

Mkuu tuhuma za kuiba mke wa mtu sio cheap politics. Ni suala nyeti na wapiga kuwa wana haki ya kujua what is going on. On one hand tuliambiwa huyu ni mchumba wake. Sasa tunaambiwa ni mume wake. Ina maana waliona lini? Lazima tujue our first lady atakuwa mchumba au mke wa rais. Inawezakana hii ikawa cheap politics kwako, lakini wewe sio mpiga kura pekee. Pia usisahau sio wapiga kura wote wanaoisoma Jamii forums.
 
Kwanza karibu mchunguliaji inakuwaje toka mwaka jana uwe na post moja tu, itabidi niongee na Invisible mtu asipo post kiwango fulani cha posts anapoteza umember wa JF mnajaza saver ya JF bure.

Pili ulianza lini kufuatilia ndoa za watu mbali na ndoa ya Josephine, au unazijua mila na desturi za makabila yote au ukiwa mkristo huruhusiwi kuoa kimila. Kwa taarifa yako kuna makabila ukishatoa kishika uchumba tu tayari huyo ni mke wako na una halali ya kuishi naye.

Mwisho acha kuchungulia na wewe uwe unachangia hata mara moja kwa mwezi.

asam.thegunner
Join Date Wed Oct 2009
Posts 1
Thanks : 0
Thanked 0 Times in 0 Posts
Rep Power
 

Unajua Sheria za Ndoa zinasemaje? Mbona Mkapa aliishi na Mke wa Mtu Ikulu kwa Miaka Kumi?
 
Ndugu wana JF, huyu sio Josephine. Aliyeandika hii habari si ajabu ni Makamba au pandikizi la Makamba. Muandishi anayejiita Josephine amequote mstari wa bibilia kutoka kitabu cha Efeso kimakosa kabisa. Efeso 4:13 inasema hivi "Hata na sisi sote tutakapoufikia umoja wa imani na kumfahamu sana Mwana wa Mungu,hata kuwa mtu mkamilifu, hata katika kwenye cheo cha kimo cha uaminifu wa Kristo"

Maneno ya "Nayaweza yote katika yeye anitiaye Nguvu" yanapatikana kutoka Barua ya Mtume Paulo kwa Wafilipi 4:13


Ni watu kama Makamba ambao wanajifanya kuijua Bible ambao wanaweza kufanya kosa liliofanywa kwenye makala hiyo inayodaiwa kuandikwa na Josephine. Kwa mkristo mlutheri kama Josephine ambaye amesoma bible wakati wa kipaimara, hawezi kutenda kosa kama hilo. Huo mstari ni maaruf, tunauimba wakati wote -- wafilipi 4.13,, ninayaweza mambo yote........ Wale ambao ni walutheri hapa mtakubaliana na mimi.

JF we got to be serious now, kila kinachopostiwa hapa tunaanza kukijadili bila hata ya kujiuliza kweli kina merits za kujadiliwa. I do not trust hii post, inabidi Josephine aka Makamba atafuet mbinue nyingine. Media sasa hivi imevamiwa, so we have to be careful guys!!!

Hii habari imepandikizwa-- Sorry siwezi kuichangia!!!
 
============

Kama ubaya unachaguliwa, heri kumchagua anayeiba wake za watu kuliko anayeiba mali za watanzania wote.
Anayesababisha hata hizo zisiwe na maana kwa sababu ya umaskini uliokithiri mpaka kwenye bedroom za watu. Siku hizi wanaume wanatukanwa na wake "mme gani wewe hata pedi huninunulii".
 

Wale wale. Kwa vile mlinzi wa Zuma, Mwinyi, nk walifanya uchafu fulani basi ruksa kwa Dr Slaa nae kufanya. Simply hakuna jipya hapo. Ndio maana upinzani hautachukua nchi. We need to be different. Issue sio kwa vile fulani alifanya basi sisi tunaweza kufanya.
 
kama unaweza kuiba mke wa mtu vipi ushindwe mali ya umma?
 
Mkuu nimekugonga thanks
 

Mkuu huwezi kujua yaliyomfanya aende kwenye vyombo vya habari. Inawezekana alilazimishwa kwa sababu fulani fulani. Au labda alijiendea mwenyewe. Uchungu wa ndoa?
 
Kwa hiyo wewe umeona matatizo ya watanzania yatatatuliwa na wewe kuwa na FURUSHI la information za Slaa guys tukue kiakili basi tuache ushabiki.

Nani aliyekwambia kuwa mtu mwenye matatizo kama Slaa anaweza tatua ya wenzake?! Lazima nyumba yako iwe safi kabla hujanyooshea kidole za wenzako.
 
Mkuu huwezi kujua yaliyomfanya aende kwenye vyombo vya habari. Inawezekana alilazimishwa kwa sababu fulani fulani. Au labda alijiendea mwenyewe. Uchungu wa ndoa?

Ha ha ha Kujidhalilisha huko Mkuu, ni Mambo ya Aibu tu Mtu kama hakutaki huwezi Lazimisha bana Ebo
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…