Ni kituko kwa kweli pale gazeti la serikali linapogeuka kuwa gazeti la udaku, tena udaku wa upande mmoja usiouliza na upande wa pili. Hivi ni lini hawa watawala wetu watajua kwamba wanatufanyia madhila makubwa pale wanapotumia madaraka yao kwa binafsi yao na si kwa umma??? Mimi nadhani imetosha sasa, tumeshadhalilishwa sana tumeonewa sana tuamke tuwaulize lini wanafikiri watakoma??? Bahati nzuri uchaguzi ndio huu na ndio nafasi yetu ya kuwaadabisha.
Hapa nina hoja moja ya msingi:
Kwa mtazamo wangu ni kwamba kwa watanzania wenye uelewa wa wastani na wa juu kuchagua chama mbadala wa CCM si tatizo, tatizo lipo kwa watanzania wanyonge wenye uelewa mdogo ambao wengi wao wapo vijijini na hawana access ya vitu kama internet ndio kikwamo cha mafanikio yetu. Mi nadhani tuunganishe nguvu zetu sote tuwafikie hao watu ili iwe rahisi kufanya mabadiliko ya kweli. Kwa mtu kama mimi sikuhitaji mama Josephine aje hapa JF akanushe au akubali lolote kuhusu shutuma za mume wake kwenye habarileo. Kwa mwanaume makini na mkamilifu hawezi kutoa shutma za namna ile. Ok tuseme sawa mama Josephine kamsaliti kaenda kwa Dr Slaa, sasa magazetini kuna nini??? Ni kweli kwamba mama Josephine ndo mkosaji namna hiyo?? Watu wakifahamu kwamba kakimbiwa na mkewe ndio iwe nini sasa??? Kwa kweli ukijiuliza haya utaona kuna nguvu zipo nyuma yake zimemtuma aseme haya. Lakini hilo pia si shida, shida ni pale gazeti letu (habarileo) linapotumika kufikisha ujumbe wa kifisadi. Hii inchi imeoza na soon watawala wetu watalibaini hilo baada ya kupopolewa mawe na wananchi wenye hasira.
Mama Josephine, sisi wengine tumekuelewa hata kabla hujasema, ila kuna haja ya kuwaeleza wale ambao hata ukisema wapo ambao hawataelewa. Kutafutwe namna waelezwe na wao waelewe. Wala hakuna haja ya kuja JF na suala hilo ni dhahiri kwamba ni njama. Waelezwe wananchi na ikibidi tutumie magazeti na mikutano ya hadhara kuwaelewesha wananchi.