Na wahanga wakuu wa hizi micro credit ni kina mama.Hao OYA ni hatari balaa, kuna sehemu walikuwepo wametega IST moja nasikia watu wanasema anadakwa mtu sasa hivi...mara Mama mmoja akiwa na mwenzake kaambiwa "haya leo tunaondoka na wewe ingia kwenye gari, wewe kila siku unatupiga chenga chenga tu na kuambiwa umehama unapokaa, ingia kwenye gari" jamaa wanaongea kwa sauti hadi watu kujaa, yule mama nilimhurumia asee.
Hali inatisha wakuu
Kuna namna inapaswa kufanywa kuwanusuru kina mama na kadhia hii.
Harakati za kina mama kupitia hii mikopo zimeleta majanga mengi sana kwenye familia