Mke wa mgombea wa CHADEMA Manyoni : Nilimwambia Polisi naomba usimuue mume wangu lakini alimpiga risasi nne

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
1,869
Reaction score
4,877
Wakuu,

Nimekutana na video ya mke wa Mgombea kupitia Chadema wa Kitongoji cha Stand, kata ya Mkwese, Jimbo la Manyoni Mashariki George Juma Mohamed akielezea namna ambavyo polisi walimkamata na kumuua mume wake kwa kumpiga risasi nne.

Mama huyu anasema kuwa aliwaomba polisi wasimuue mumewe lakini polisi walimpiga mume wake risasi nne na hivyo mume wake alifariki dunia

Pia alisema kuwa mwanae aliona jinsi baba yake alivyouwawa kikatili na polisi.

Soma pia: Manyoni: George Juma Mohamed, Mgombea wa CHADEMA auawa kwa kupigwa risasi usiku wa kuamkia tar 27, 11, 2024

=========================================

Naomba niishie hapa. Nisije nikaandika zaidi nikaharibu.

Ila haya mambo yote huwa yana mwisho na mwisho wake huwa sio mzuri

Your browser is not able to display this video.
 
Duh Tanganyika! Ndipo tulipofikia hapa?
 
Wanaua kama Nyani tu.

Kumbe jamaa walishatumwa kabisa atajayezuia wizi wa kura malizane naye.

R.I.P Steven
 
Umechanganya mambo. Huyu ni mke wa yule wa Manyoni George
 
Hakuna mwebye DHAMANA anayejali.

Watanzania wanauawa na polisi bila huruma.

Wananchi tuanze kuchukua hatua kuwazuia polisi wasiue raia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…