Mke wa Mtu Sumu: Asiyesikia la Mkuu Huvunjika Guu

Rorscharch

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2013
Posts
878
Reaction score
2,014
Nakumbuka miaka ya 2010 nikiwa nimetoka chuo, bado nanuka optimism ya maisha. Nilikuwa na uhakika kwamba mshahara wangu wa kwanza ungekuwa milioni moja, na mawazo mengine ya mchana kama hayo yalinifanya niamini kuwa maisha yangenyoosha tu. Katika kipindi hicho, nilijijengea utamaduni wa kujichanganya na wazee wa kijiweni pale Kinondoni Studio, jijini Dar es Salaam.

Niliingia kijiweni kama kijana mwenye ndoto kubwa na matumaini tele, lakini nilitoka nikiwa nimebeba hekima ya maisha. Nikajifunza kuwa dunia si lelemama, na kuna mambo ambayo ukiyafanya, basi gharama yake ni kubwa zaidi ya unavyoweza kufikiria.

Miongoni mwa mafunzo makubwa niliyopata ni kwamba wanaume wanapaswa kuheshimiana kwa kutohusiana na wake za watu. Lilikuwa somo lililorudiwa mara kwa mara, na kila niliposikia wazee wakilisema, nilihisi uzito wake. "Kuna mambo ukifanya, utaomba bora ungeuawa, kwani fedheha yake ni mbaya zaidi ya kifo," alisema mzee mmoja pale kijiweni.

Na kama kuna hadithi iliyothibitisha hilo, ni ile aliyotueleza kuhusu kilichomkuta dereva mmoja wa teksi miaka ya 90.

Hadithi yenyewe ilikwenda hivi…

Alionywa, Lakini Akadharau

Katika kijiwe cha teksi maeneo ya Kinondoni, kulikuwa na dereva mmoja aliyepata mteja wa kudumu—mke wa mwanajeshi. Mwanamke huyo alipozoea huduma yake, alihakikisha kwamba haendi na dereva mwingine yeyote. Muda si mrefu, uhusiano wa kibiashara ukageuka kuwa uhusiano wa kimapenzi.

Kwa muda, walifurahia penzi lao la siri. Mwanajeshi, bila kujua, alikuwa akitoa pesa za matumizi na mizunguko, lakini kumbe zilikuwa zinaishia malodge na magesti.

Baadhi ya madereva wenzake kijiweni walimwonya:

"Mkuu, mke wa mwanajeshi si mtu wa kuchezea. Sisi tumekaa hapa muda mrefu, tunajua haya mambo yanavyomalizikaga. Achana naye kabla mambo hayajakuharibia."

Lakini kijana alikuwa na kichwa kigumu. Aliona kama wanamwonea wivu kwa sababu amepata "zali" la mentali lenye malipo mazuri na starehe ya bure.

Hakujua kuwa siku za mwizi ni arobaini.

Njama Zafichuka

Kwa bahati mbaya kwake (na nzuri kwa mjeda), kuna jamaa mtaani aliyegundua kinachoendelea. Jamaa huyo, kwa kutumia mbinu za kipelelezi, alikusanya ushahidi wa kutosha na akaenda kumtonya mume wa mtu.

Mwanajeshi hakupoteza muda. Alianza kupanga mpango wa kulipiza kisasi bila kuonyesha dalili zozote kwa mkewe.

Siku moja, kama kawaida yao, mke wa mtu na mchepuko wake walipanga kukutana gesti. Mwanajeshi, kwa ustadi wa kijeshi, alijifanya ana safari ya ghafla na kumwambia mkewe. Mwanamke, kwa furaha, aliiachia nafasi hiyo bila hofu yoyote, akidhani amepata muda wa kuwa na mpenzi wake wa siri bila mashaka.

Alichosahau ni kwamba mjeda alishatengeneza mtego.

Mtego Wanasa

Wakiwa chumbani, wakiendelea na mambo yao, ghafla mlango ulipigwa teke moja zito!

Wakaingia ndani wanaume wa miraba minne, wakiongozwa na mjeda mwenyewe.

Mke wa mtu alipigwa vibao vya uso kwa nguvu hadi akatema meno mawili. Mjeda kisha akawageukia wenzake na kuwaamuru:

"Mchukueni huyu mwanamke, mkampeleke kwenye gari."

Wanaume wawili wenye miili mikubwa walimbeba na kumtoa nje huku akilia na kuomba msamaha.

Lakini kwa mchepuko wake, mambo hayakuwa mepesi.

Dereva huyo alipigwa kwa nguvu huku akitukanwa na kukemewa kwa ukosefu wa heshima. Alijaribu kuomba msamaha, lakini hakusikilizwa. Hatimaye, alipigwa kwa nguvu kichwani na kuzimia pale pale.

Fedheha Iliyoshinda Kifo

Kilichotokea baada ya hapo hakikujulikana mara moja.

Kwa siku kadhaa, dereva huyo hakufika kijiweni. Wenzake walishangaa kimya chake, lakini hakuna aliyekuwa na ujasiri wa kuuliza.

Siku chache baadaye, alirejea. Alionekana kama mtu aliyepoteza roho yake. Macho yake hayakuwa na uhai ule wa zamani.

Kwa siku mbili tatu, alihisi kuna kitu hakipo sawa. Watu walimkwepa, wengine walimtazama kwa huruma, na wachache walikuwa wakimpa pole bila maelezo.

Hatimaye, rafiki yake wa karibu alimvuta pembeni na kumkabidhi bahasha ndogo.

Dereva alipoifungua, mwili wake ulitetemeka.

Ndani yake kulikuwa na picha kadhaa.

Alipozitazama, miguu yake ilikosa nguvu. Alikaa chini ghafla, huku macho yake yakikodoa kwa mshtuko.

Ilikuwa picha yake akiwa uchi wa mnyama, akiingiliwa kinyume cha maumbile na wanaume wa miraba sita.

"Pole sana ndugu yangu," rafiki yake alisema kwa sauti ya huzuni.
"Hizi picha zilibandikwa kote mtaani. Zimeonekana kwenye mistimu, kwenye kituo cha mabasi pale, na zingine zimeokotwa. Tumefika hapa kijiweni tukakuta zimebandikwa. Ni nyingi sana, tumezibandua tulivyoweza."

Siku hiyo, dereva aliacha gari yake pale kituoni pamoja na funguo zake. Baadaye, bosi wake alipewa funguo hizo.

Hakuna aliyewahi kumuona tena.

Alitoweka na kuacha historia ya fedheha ambayo watu bado wanazungumzia mpaka leo.

Hitimisho

Mke wa mtu ni sumu. Sumu mbaya kuliko hata sumu ya nyoka.
 
Chai 🍵 ili kutisha watu. Akuna! Tutaendelea kuwabokoa na kugawa dozi kwa idadi kama watalavyokuja
 
FB_IMG_1719557793598.jpg
 
Shida ni hao nao wake za watu,kukana hawana mume,ila ukigundua achana nae kabisa,hata kama ni abiria wako,potezea,Ni sumu na ni kifo!
 
Honestly speaking, kwa mwanaume anayetembea na mke wa mtu kwa dunia ya sasa lazima kuwe na kitu hakiko sawa kwenye akili yake. Kuna watoto wengi mnoo leo hii wapo wapo tuuu ya nini ukakitafute kifo kwa lazima?

Labda iwe emergency tu ambayo pia ukimaliza unajutia upumbavu umefanya
 
Back
Top Bottom