Mke wa ndoa anaposema maneno haya anamanisha nini ?

Mke wa ndoa anaposema maneno haya anamanisha nini ?

utakuwa ni mmoja wa marafiki zake mke wa OP wanaompa kichwa na kumpoteza wakati ndoa zao zimewashinda ama hawajaolewa kabisa, kama wewe tu.
Hahahahaha kutokuolewa haimaanishi hujui sheria za ndoa ....vitabu vipo maandiko ya kiroho yapo na yanasomeka vizuri na kueleweka
 
Iko hivi mwaka 2008 tulibahatika kupata mtoto bila ndoa 2014 tukapata mwingine bila ndoa ila mwaka 2016 tukabariki ndoa na sasa tunaishi kwenye ndoa ya watoto watatu sasa hivi huyu mke amekuwa na maneno makali ya kuchoma moyo na mwili
mfano

1.nilimwambia jana mbona nguo chafu na hapo jikoni hapako vizuri na nasema hivyo coz kulikuwa ma wageni watakuja kututembelea akaniambia mwanaume wewe una gubu

2.ananiambia nimemweka kifungoni nimemfanya mjinga sana kwa mda mrefu ila sasa ninajitambua
ananiambia hivyo baada ya kumwambia tuweke mahesabu sawa kati ya fedha take na yangu kwa ajili ya maandalizi ya watoto shule january alikuwa mkali kama pilipili na hajawahi kuniambia maneno aliyoniambia
mfano;

Miaka yote pesa yangu sina uhuru nayo nimesomeshwa na wazazi wangu kwa ajili ya faida yao na siyo kwako na matoto yako kwa ujue utawapeleka vipi matoto yako shule pesa yangu achana nayo kabisa kama unataka uje uniombe
hapa nikamjibu haitatokea kumwomba kama amechoka watoto anipe wanangu

3.Ongeza hawezi mapenzi ya kubembelezana bembelezana sijui nikupetipeti sijui nikulambe wapi ukiyataka hayo katafute wenye nayo kwangu hutoyapata na ukitaka kaoe kabisa ila ujue watoto wao na akaongeza siogopi kuachwa hata kidogo na ungejua kilichopo moyoni mwangu(kwake mke) ungenyamaza tu

Huwa nina kawaida ya kumsaidia kazi za ndani kama kuchota maji,kufua,kupika, sasa jana kaniambia wala sitaki unisaidie vikazi unavyonisaidia.

then wenzangu mlioko kwa ndoa na mna watoto siyo chini ya watatu nguo zenu zinanyooshwa na wake zenu au nyie wenyewe,viatu au makobazi yanafuta na kupakwa ranging na mke au nyie wenyewe.
je maji ya kuoga mnapeleka wenyewe au mnapelekewa mimi nafanya vyote hivyo mwenyewe .

Anasema hayo yote then asubuhi analia tu na kusema yaishe nashindwa hata kuelewa anataka nini anafikiri nini na matarajio yake nini
Jiandae kisaikolojia Kwa tukio la ajabu kufanyiwa. Amekwambia ungejua kilichopo moyoni mwangu ungenyamaza. Kuwa makini anaweza kukuua mda wowote ule
 
Ndio ilivyo
Hela ya mwanamke siyo ya kutegemea, we somesha watoto wako kutimiza wajibu na wakikua usitegemee msaada kutoka kwao watamjali zaidi mama yao
Na maisha yalivyo tight kama hela ya mwanamke siyo ya kumtegemea ni Bora kama ni mtumishi aache kazi .ili awe mwanamke halisi
 
Huu ujinga wa kusema pesa ya mwanamke ni yake na ya mwanaume ni ya familia ni mojawapo ya factor inayochangia umasikini kwenye familia nyingi za kiafrica.
Sijui nisemaje lakini kukunyima mshahara wake ni haki yake ....pesa za mwanamke ni za kwake yeye mwenyew ..kama ataamua kukusaidia majukumu sawa vinginevyo hutakiwi kuzipangia matumizi zile ni zake....kakwambia kweli kasomeshwa na wazazi wake ili awafae baadae hakusomeshwa sababu nyingine ....kingineee kupeleka maji bafuni sio kazi yake labda aamue kukupelekea kwa mapenzi yake tu .....kufua pia labda aamue kukufulia kwa mapenzi tu vinginevyo tafuta dobi ...samahani kama utakwazika lakini habari ndiyo hiyo

Somesha wanao usimtegemee yeye wewe ndie kichwa na kiongozi wa familia
 
Ulikosea sana ulipoanza kumfulia nguo za ndani...

Huna chako hapo mpaka sasa, mke wako anakazwa na mwanamme mwingine ndio maana amekuwa na kiburi..

Cha kufanya fanya kama unasafiri ili kumwekea mtego na hakika utajua ni mwanamme yupi anaempa kiburi na ukifumania hiyo ndio tiketi ya kumwacha...

Mambo ya kubembelezana nishasahau wanawake wenyewe wengi, tena wazuri hivi...

Anyway pole sana mkuu...
 
Sijui nisemaje lakini kukunyima mshahara wake ni haki yake ....pesa za mwanamke ni za kwake yeye mwenyew ..kama ataamua kukusaidia majukumu sawa vinginevyo hutakiwi kuzipangia matumizi zile ni zake....kakwambia kweli kasomeshwa na wazazi wake ili awafae baadae hakusomeshwa sababu nyingine ....kingineee kupeleka maji bafuni sio kazi yake labda aamue kukupelekea kwa mapenzi yake tu .....kufua pia labda aamue kukufulia kwa mapenzi tu vinginevyo tafuta dobi ...samahani kama utakwazika lakini habari ndiyo hiyo

Somesha wanao usimtegemee yeye wewe ndie kichwa na kiongozi wa familia
Naendelea kupata sababu za kuwachukia wanawake wasomi
 
Huu ujinga wa kusema pesa ya mwanamke ni yake na ya mwanaume ni ya familia ni mojawapo ya factor inayochangia umasikini kwenye familia nyingi za kiafrica.
Pesa ya mwanamke ni ya kwake hilo kataa au ukubali ila ukweli ndo huo ukitaka kupindisha we pindisha tu........kama mnadhani madai ya mtoa mada yapo sahihi mwambieni aende mahakamani akamshitaki mkewe halafu alete mrejesho hapa
 
KAA NAE CHINI MUULIZE MASWALI YAFUATAYO:-

1. MWAMBIE AWE HURU TU...AKWAMBIE UKWELI ULIPO MOYONI MWAKE(hata kama kusema kwa mdomo hawezi, mwambie aandike)...NI NINI HASA ANATAKA KWA SASA..?

2. YEYE KWA UPANDE WAKE ANAICHUKULIAJE NDOA..?

3. NA KAMA KUMUACHA...JE YUPO TAYARI UMUACHE...? NA KAMA ANAVYOSEMA NA ASIKUSUMBUE KUHUSU WATOTO NA HATA UKIOA MKE MWINGINE...?

4. KAMA MAPENZI YAMEPUNGUA JE ANGEPENDA MAPENZI YAKE YAFUFUKE...KAMA KUNA UWEZEKANO MTOKE MAHALI MKARENEW MAPENZI YENU...?

NOTE:
MPE UHURU WA KUJIELEZA NA UHAKIKA WA KUELEZA HISIA ZAKE...NA UMHAKIKISHIE KUWA HUTOONGEZA MASWALI MENGINE YA KUMKERA...UNAWEZA DHANIA ANA MTU MWINGINE NJE...LAKINI HAPANA KUNA KITU TU KIPO NDANI YAKE KINAMSUKUMA OVYO...SO HESHIMU MAWAZO YAKE...NA KAMA KUNA MAHALI PA KUMSAIDIA MSAIDIE KUTATUA TATIZO LAKE...

AU

HUENDA HUKO MAKAZINI MIONGONI MWA SHOSTI ZAKE KAZINI AU ANAPOENDA KUPIGA STORY NI MA'SINGLE MOTHER NA NDIO WANAOMPA KIBURI...

JINGINE..

OMBI LANGU KWAKO...ENDAPO MKAFANIKIWA KUPATA SULUHU NZURI...MWAMBIE KWA FAIDA YA MAPENZI NA NDOA YENU...MWAMBIE AACHE KAZI YOYOTE ILE ANAYOIFANYA..ATULIE KWANZA NYUMBANI AJITAFUTIE...HATAKI MWAMBIE CHAGUA...KAZI AU NDOA YAKO...!

HIYO NI KWA FAIDA YA NDOA YAKO...NA UTAGUNDUA MENGI TU(yale aliyosema ungejua yaliyopo moyoni mwangu)...
Big up saana Mkuu
 
Iko hivi mwaka 2008 tulibahatika kupata mtoto bila ndoa 2014 tukapata mwingine bila ndoa ila mwaka 2016 tukabariki ndoa na sasa tunaishi kwenye ndoa ya watoto watatu sasa hivi huyu mke amekuwa na maneno makali ya kuchoma moyo na mwili
mfano

1.nilimwambia jana mbona nguo chafu na hapo jikoni hapako vizuri na nasema hivyo coz kulikuwa ma wageni watakuja kututembelea akaniambia mwanaume wewe una gubu

2.ananiambia nimemweka kifungoni nimemfanya mjinga sana kwa mda mrefu ila sasa ninajitambua
ananiambia hivyo baada ya kumwambia tuweke mahesabu sawa kati ya fedha take na yangu kwa ajili ya maandalizi ya watoto shule january alikuwa mkali kama pilipili na hajawahi kuniambia maneno aliyoniambia
mfano;

Miaka yote pesa yangu sina uhuru nayo nimesomeshwa na wazazi wangu kwa ajili ya faida yao na siyo kwako na matoto yako kwa ujue utawapeleka vipi matoto yako shule pesa yangu achana nayo kabisa kama unataka uje uniombe
hapa nikamjibu haitatokea kumwomba kama amechoka watoto anipe wanangu

3.Ongeza hawezi mapenzi ya kubembelezana bembelezana sijui nikupetipeti sijui nikulambe wapi ukiyataka hayo katafute wenye nayo kwangu hutoyapata na ukitaka kaoe kabisa ila ujue watoto wao na akaongeza siogopi kuachwa hata kidogo na ungejua kilichopo moyoni mwangu(kwake mke) ungenyamaza tu

Huwa nina kawaida ya kumsaidia kazi za ndani kama kuchota maji,kufua,kupika, sasa jana kaniambia wala sitaki unisaidie vikazi unavyonisaidia.

then wenzangu mlioko kwa ndoa na mna watoto siyo chini ya watatu nguo zenu zinanyooshwa na wake zenu au nyie wenyewe,viatu au makobazi yanafuta na kupakwa ranging na mke au nyie wenyewe.
je maji ya kuoga mnapeleka wenyewe au mnapelekewa mimi nafanya vyote hivyo mwenyewe .

Anasema hayo yote then asubuhi analia tu na kusema yaishe nashindwa hata kuelewa anataka nini anafikiri nini na matarajio yake nini

niko kwenye ndoa lakini nimesisimka hayo maneno. kwanza mimi ni muumini wa mfumo dume huwa sisaidii kazi yeyote nyumbani. kazi yangu moja tuu kuhudumia familia
 
Pole sana kaka..haya mambo kwenye ndoa yapogo sana tu..
Mosi mkeo humridhishi kwakila.kitu.unamchukulia poa poa tu😏
Pili amepata wa kumshika sikio
Tatu..ameanza kuchepuka (huu ni ukweli zaidi) na huyo sio mzoefu wa kuchepuka ndo kaanza..mwqnamke mzoefu kuchepuka anazidishaga mapenzi ndani...aso mzoefu huwa bi bora liende...ss km ww ni kidume kweli jitahd kumrudisha kwenye mstari kabla haijawa worse zaidi😊😊...akizoea kuchepuka imetoka hyo..
Jingine... punguza gubu una vitu vingine bas mwambie ht dada wa kazi...inaezekana uliongea kwa nguv had wagen wkqsikia...nan anapenda kuumbuliwa hvyo...

La mwisho aisee hongera..unamsaidia mkeo kazi??jaman jaman jaman...sie wengi ht handkerchief hawafui😏😏..ww acha kumsaidia kaz as amesema mwenyew...!
la mwisho usitegemee hela ya mkeo..ila ina bahati.sana...wengine hapa tumegawana majukumu pasu kwa pasu...
UMENIVURUGA😣😣
 
Unataka tuwe honest, Amepata jamaa anamzuzua, ndio maana sometimes anakuona takataka sometimes anajutia majibu yake kwako hiyo ni kwaajili ya watoto tu, sio wewe.
asante sana mkuu, umemwambie ukweli, ukisikia mke wako anakwambia hata kuachika ako tayari, jua huyu mke tayari ako na jamaa, na huyu mume pls ajaribu kutafuta njia ya kuishi bile huyu mke, hii ni balaa
 
Yawezekana ana mimba changa. Hawa jamaa wakiwa na mimba changa hawatabiriki ni kama kuku wa kisasa. unapita zako kwenda kuokota mayai yeye analala chini kuwa weye kakuona jogoo anataka umpande.
Mpe muda mkuu, tena ni mkeo mpendwa wako. Huna mwingine hivyo mbembeleze tu hata kuzama chumvini ili umridhishe
 
Kuna njemba linamtia kiburi ndiyo sababu anaweza kukujibu majibu yenye najisi.
 
Back
Top Bottom