Mke wa Nyalandu asema mumewe hakutaka kutoroka nchini

Mke wa Nyalandu asema mumewe hakutaka kutoroka nchini

Vipi Mbowe anaenda ubalozi gani ? Au na yeye ataibukia Kenya, mna drama kama ma slay queen vile 😂...
Mkianzisha CDM reality TV show mtapata pesa nzuri zaidi hata ya ruzuku, maana mpo vizuri kwenye maigizo.
Ukikua utaelewa kwa sasa najua unategemea K ya dada yako kuishi na kuchat hapa JF!
 
Mkuu wa Wilaya ya Longido, Frank Mwaisumbe amesema, Lazaro Nyalandu amezuiwa Namanga kwasababu hakuwa na nyaraka muhimu na atafikishwa Mahakamani endapo atashindwa kuwasilisha nyaraka hizo.

Mke wa Lazaro Nyalandu, Faraja Kotta Nyalandu amesema wao wanaishi Arusha na mumewe hahitaji nyaraka ili kufanya shughuli zake akiwa upande wa Tanzania na wala hakuwa na mpango wa kuvuka mpaka wa nchi.

Pia amesema tukio hilo halikutokea Novemba 9, kama ilivyoripotiwa bali lilitokea Novemba 6.

Lazaro Nyalandu alikuwa Mgombea Ubunge wa Jimbo la Singida Kaskazini kupitia CHADEMA. Iliripotiwa kuwa anashikiliwa na Maafisa Uhamiaji wa Tanzania kwa tuhuma za kutaka kuondoka nchini bila nyaraka muhimu.

Mke Wa nyalandu kaongea ukweli Nyalandu ni Jirani yangu anaishi Arusha alihamiaga kitambo sana kwa hiyo kwenda kwake namanga ni kama kaenda Dukani kununua maziwa ya mtindi tu
 
Kwa sisi tulioanza kufuatilia tawala za kiimla toka zama za akina Amin, Mobutu, Bokassa, Doe nk tunaelewa namna hawa madikteta wanavyo-operate.

Kwanza sifa kuu ya dikteta yeyote ni kuwa muoga kiasi cha kuamini watu wachache sana au kutoamini yeyote kabisa.

Hii hulka huwafanya wawaue wapinzani wao au kuwapa hofu ili wakimbilie uhamishoni. Yeyote yule mwenye kuwafuatilia hawa watawala wa kiimla watakubaliana na mimi.
 
Kwani Lissu akijifungia ubalozini Tz inaathirika vipi, acha akae humo ndani hadi January akitoka train za SGR zitakuwa zimefika 😂.
Au Lissu akikaa ndani ubalozini ndio fanatics wake watagoma, hizi strategy na mipango ya Twitter na JF ni ya kitoto na kipuuzi, hata hao mabalozi watakuwa wanamdharau Lissu saivi.
Kunywa maji upumzike kidogo, alafu ukirudi ujenge hoja na si mipasho
 
Tunasubiria episode ya nne ya bwana mashavu Boniface Jacob, sijui yeye atatokea border gani na igizo jipya la Chadema 😂
Hivi wewe masikini unafurahia mateso ya wengine unapata faraja sio..wenzako wanachota matrilioni wewe unasugua gaga bwa bwa
 
Yaani haya majamaa ndizi haswaa, Zitto anasema eti wapiganaji wanagawanyika makundi mawili moja litakuwa nje kama wakimbizi na lingine litapigana humuhumu ndani. Jamaa viazi sana wanajaribu kuiga wale diaspora waliosaidi kuleta mapinduzi kwenye nchi za kiarabu ambazo hadi leo hata hao waliosaidia kupindua hawathubutu kuingia nchi hizo. Kwa tanzania watasubiri sana, nchi hii si ya kulinganisha na nchi za kiarabu na kiafrika magharibi,hii ni Tanzania ya nyerere. Halafu kikundi chenyewe kimejaa ma form four failure, msomi ni zitto pekee ambaye naye ni vuguvugu hajitokezi waziwazi anajaribu kupima kina cha maji.
Hao jamaa ma pimbi sana, yani wanafanya hesabu za kitoto kabisa
 
Tunasubiria episode ya nne ya bwana mashavu Boniface Jacob, sijui yeye atatokea border gani na igizo jipya la Chadema 😂
Wewe ni mpumbavu,.kwa hiyo watu wasisafiri nje ya nchi kwa kuwa Magufuli yeye hawezi kusafiri?
 
Wewe ni mpumbavu,.kwa hiyo watu wasisafiri nje ya nchi kwa kuwa Magufuli yeye hawezi kusafiri?
Poaaa, Mbowe anasafiri lini 😂
Tunajua kuna episodes inafuata ya Mbowe na mashavu Boniface, hizi ni reality show kabisa, CDM mtafute copyright BASATA.
 
Serikali inatakiwa ijiongeze haiwezekani kwenda mikono nyuma kila wakati. Hawa mabeberu wametuletea mgombea wao kwenye uchaguzi. Maana ni mjinga tu na asiye na akili wala hekima atakayesema Lissu alikuwa mgombea wa cdm na alikuwa anawakilisha baadhi ya Watanzania. Ni ujinga kufikiria hivyo.

Lissu alikuwa mgombea wa mabeberu aliyeletwa kushiriki uchaguzi wa Tanzania ili awakilishe maslahi ya mabeberu ukiwemo ushoga.

Sasa Tanzania kuwa nchi huru maana yake nini? Kama tunaweza kuletewa mgombea katika uchaguzi wetu na mabeberu. Uchaguzi umeisha bado chokochoko zao haziishi. Hivi Tanzania inaweza ikampeleka mzungu au rai wa nchi za kibeberu awe mgombea katika chaguzi zao kwa ajili ya maslahi ya Tanzania.

Wakati umefika balozi wa ujerumani au aitwe atoe maelezo na kama hayatajiridhisha afukuzwe. JK Nyerere alifanya hivyo na JPM hatakuwa wa kwanza. Hivi nani asiyejua Wajeremani na Wazungu wana maslahi Tanzania? Kwa nini maslahi hayo yasitumiwe kuwafanya hawa wawe na adabu.

Utaratibu huu wa sasa wa kuenda kihewala Bwana mkubwa kila wakati hautatusaidia lolote ila utatuumiza kidogo kidogo mwisho wa siku tutashindwa maana unafiki haujawahi kulipa hata siku moja.

Radio yao ya DW imekua propoganda machinery dhidi ya serikali. Balozi naye kaingia mstari wa mbele sasa kusaidia uhuni wa Lissu na genge lake halafu anaangaliwa tu, haiwezekani.

Lazima lifanyike jambo. Amsterdam ana tentales zake sasa hadi nchi ya jirani ya Kenya bado tunaangalia tu. Ukisikia maneno ya mwanasheria wa Lema utaona bila ubishi ni spika tu ya Robertison. Hao NTv ya Kenya ni dhahiri wanalipwa kutuhujumu kwa propoganda zao. Halafu wanamtumia Bwege tunaangalia tu. Sasa kama Taifa tunatakiwa tushughulikie hivi viashiria vidogovidogo mapema bila kukawia.
Maelezo yote haya unajisumbua tu. Hakuna mtu ndani ya serikali hii anayeweza kumfukuza balozi wa Ujerumani ama Marekani ama wa nchi yoyote ya Ulaya.

Nasema hakuna usione wamekaa kimya ukadhani ni wajinga.
 
Sijui nani msema kweli hapo au Nani muongo..nilichopenda tu vile mke alivyosimama kutetea Mume.
 
arv ZIKO DUNIA NZIMA ISSUE NI PESA TU , WALA USIJIDANGANYE KWAMBA ULAYA NA MAREKANI NDIYO WAFADHIRI PEKEE.CHINA YUPO NA URUSI
Huyo China anayewekewa vikwazo kila siku na Marekani ndo awe mtetezi wa mwafrika?

China hana muda na mambo ya siasa yeye kikubwa ni kukopesha nchi za kiafrika kwa riba isiyolipika ili avune mavuno manono lakini sahau suala la kukusaidia.
 
Mkuu wa Wilaya ya Longido, Frank Mwaisumbe amesema, Lazaro Nyalandu amezuiwa Namanga kwasababu hakuwa na nyaraka muhimu na atafikishwa Mahakamani endapo atashindwa kuwasilisha nyaraka hizo.

Mke wa Lazaro Nyalandu, Faraja Kotta Nyalandu amesema wao wanaishi Arusha na mumewe hahitaji nyaraka ili kufanya shughuli zake akiwa upande wa Tanzania na wala hakuwa na mpango wa kuvuka mpaka wa nchi.

Pia amesema tukio hilo halikutokea Novemba 9, kama ilivyoripotiwa bali lilitokea Novemba 6.

Lazaro Nyalandu alikuwa Mgombea Ubunge wa Jimbo la Singida Kaskazini kupitia CHADEMA. Iliripotiwa kuwa anashikiliwa na Maafisa Uhamiaji wa Tanzania kwa tuhuma za kutaka kuondoka nchini bila nyaraka muhimu.

She is very right.
Waliomshikilia wanaweza kushinda kesi mahakama kirahisi tu.

Haya mambo ndiyo yanaichafua nchi.
 
Hawa akina Lema na Lissu pamoja na ndugu zao chini ya kapeti hawitakii mema Tanzania,wanacho kifanya ni kuichafua taswira ya nchi yetu mbele ya Jumuia ya kimataifa ili kuvutia vikwazo vya kimataifa.

Wananchi tumeamua kupitia sanduku la kura hawawezi hata wakiungana matusi kututukana
 
Poaaa, Mbowe anasafiri lini 😂
Tunajua kuna episodes inafuata ya Mbowe na mashavu Boniface, hizi ni reality show kabisa, CDM mtafute copyright BASATA.
Sasa kama ni maigizo Why dikteta Mla nyama za watu anahangaika? Nyama za akina Alphonce Mawazo, Akwilina, Azory Gwanda, Ben Saanane, maelfu ya Wananchi wasio na hatia wa Pemba na Kibiti zilizojaa kwenye mafriji nyumbani kwake hazijamtosha tu kwenye tumbo lake?
 
Yaani haya majamaa ndizi haswaa, Zitto anasema eti wapiganaji wanagawanyika makundi mawili moja litakuwa nje kama wakimbizi na lingine litapigana humuhumu ndani. Jamaa viazi sana wanajaribu kuiga wale diaspora waliosaidi kuleta mapinduzi kwenye nchi za kiarabu ambazo hadi leo hata hao waliosaidia kupindua hawathubutu kuingia nchi hizo. Kwa tanzania watasubiri sana, nchi hii si ya kulinganisha na nchi za kiarabu na kiafrika magharibi,hii ni Tanzania ya nyerere. Halafu kikundi chenyewe kimejaa ma form four failure, msomi ni zitto pekee ambaye naye ni vuguvugu hajitokezi waziwazi anajaribu kupima kina cha maji.
Unazungumzia Tanzania ya Nyerere?

Huyo Nyerere aliyeponea chupu chupu mara kadhaa kupinduliwa hadi akaamua kung'oka kuhofia kuondoka kwa aibu.

Kama Nyerere alikoswakoswa kupinduliwa tena nchi ikiwa gizani na wasomi kiduchu vipi sasahivi wasomi kibao na watu wengi wenye uelewa wasiotaka kuwasujudia watawala ishindikane kufanya jambo lao.

Ni suala la muda tu watawala wengi wa kiafrika hawakuamini kilichowapata baada ya kudhani jeshi na vyombo vingine vitakuwa vitiifu milele.

Jeshi likiona wananchi wamechafukwa roho huwa linaungana nao kumuondoa aliyekuwa anatoa amri.

Kibri sio jambo lakujivunia hata kidogo.
 
Mkuu wa Wilaya ya Longido, Frank Mwaisumbe amesema, Lazaro Nyalandu amezuiwa Namanga kwasababu hakuwa na nyaraka muhimu na atafikishwa Mahakamani endapo atashindwa kuwasilisha nyaraka hizo.

Mke wa Lazaro Nyalandu, Faraja Kotta Nyalandu amesema wao wanaishi Arusha na mumewe hahitaji nyaraka ili kufanya shughuli zake akiwa upande wa Tanzania na wala hakuwa na mpango wa kuvuka mpaka wa nchi.

Pia amesema tukio hilo halikutokea Novemba 9, kama ilivyoripotiwa bali lilitokea Novemba 6.

Lazaro Nyalandu alikuwa Mgombea Ubunge wa Jimbo la Singida Kaskazini kupitia CHADEMA. Iliripotiwa kuwa anashikiliwa na Maafisa Uhamiaji wa Tanzania kwa tuhuma za kutaka kuondoka nchini bila nyaraka muhimu.

Mbinu chafu za CCM
 
Back
Top Bottom