Mke wa Nyalandu asema mumewe hakutaka kutoroka nchini

Kastukiwa huyo, wanaacha nyaraka halali ili wakaombe hifadhi ya ukimbizi. Serikali ya Tanzania inashindwa kumtimua balozi wa Ujeremani akawa kielelezo cha msimamo wetu kama Taifa. Kwa nini hawa wanaachwa watuchezee hivi?

Wewe ni mshamba! Hifadhi huwa rahisi zaidi unapokuwa na nyaraka. Usilete mambo ya kuhadithiwa hapa. Unaweza kuwa hujui hili. Kile kiwanja ambapo ubalozi wa Ujerumani (na wowote ule wa nchi nyingine) sio sehemu ya himaya ya Tanzania - kwa mujibu wa mkataba wa Geneva. Kutimua balozi hawewezi, labda watimue hawa wengine waafrika. Hawaachwi watuchezee - hatuna haki wala uhalali wa kuwafanyia unayotaka! Na usiombe wakalipiza!!!
 
Hivi najiuliza kuna tishio gani mpaka waliokuwa wabunge wa upinzani wanataka kukimbia nchi kwa na Kwa kosa lipi au kwa kuwa tu mpinzani au kuna madudu ya maisha yao ya uongozi wanaogopa mkono wa sheria ?

Na kama ni hilo la kwanza yaani tumefikaje hapa kama nchi kuona watu ambao tunatofautina kwa mawazo tu wawe ni maadui hivyo au tukubali kwamba mtu mweusi namna yake ya kufikiria ina upogo/ kasoro

Maana kama wana makosa yaliyo dhahiri je si ni vyombo vyetu vya dola vinapaswa kuonyesha na kupeleka / kuwapeleka mbele ya sheria ili haki ipatikane lkn kama shida ni kuwa mpinzani tu but we have long way to go
 
Maelezo yote haya unajisumbua tu. Hakuna mtu ndani ya serikali hii anayeweza kumfukuza balozi wa Ujerumani ama Marekani ama wa nchi yoyote ya Ulaya.

Nasema hakuna usione wamekaa kimya ukadhani ni wajinga.

Balozi wa USA ahangaikie hali yake na TRUMP.
 

Mlikuwa na maneno haya haya kuhusu Corona. Awamu ya JPM haina akili za kulamba makalio ya wazungu. Nambo haya tumeyasahau miaka 5 iliyopita Tanzania.
 
Hili swala sioni mantiki wa ccm wanaoamin tumeshinda kwa halali kulipigia kelele, bali tufurahini sababu wanaotukwamisha bila sababu wameamua kuondoka, haina haja kuwaongelea ni kuwapa kiki.
 
Tatizo la Watanzania wengi malezi yetu yametuathiri sana... Tunajipima kwa matokeo na hatujifunzi wa kujipima kutoka katika mapitio.

Ni wagumu kukubali kushindwa na kujipanga, na tunapenda sana mafanikio ya muda mrefu na kuambiwa maneno mazuri.

Hatupendi ukweli na tunadhani kuhusianishwa na anguko ni vibaya sana..hali inayopelekea kutufanya tupende kutafuta sababu za kuhalalisha anguko letu na kulijengea mazingira ya kuonekana kuwa achievements.

Mungu Atusaidie.

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Safi Faraja, too much spinning na pengine kumpotosha mkuu wa kaya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…