Ninachosikitika Mimi ni Castro kumsaliti na kushirikiana na CIA kumuua che Guevara
Sio kweli mkuu, che alioachia nyazfa zake cuba alienda congo ila baada ya kujaribu alishindwa na kuzidiwa na kukimbilia embassy of Tanzania ndipo fidel alipomwandikia barua kuwa aachane na hizo mambo arudi cuba ila alikataa kurudi hadi pale ambapo atafanikiwa kufanya mapinduzi nchi ingine
Che ndipo akaenda Bolivia na kukutana na kiongozi wa Bolivia communist party wakaongea kuhusu revolution ila jamaa akamwambia kuwa wanaweza kuungana ila kwa sharti moja, kuwa jamaa asiwe kiongozi wa hayo mapinduzi ispokuwa chama ndio kiongoze ila che akagoma, ye alikuwa anataka awe kiongozi
Baada ya jamaa kukataa che akawa na kundi dogo sana la wanajeshi ambao walikuwa 25 tu na hawana silaha za kutosha wala madawa na chakula, ila mwaka 67 akakutana na mdada mwana harakati kutoka france ndio akawasaidia nguo, chakula, madawa ila bado alikosa watu wengi wa kumuunga mkono ila ye akawa analazimisha tu
Kabla hawajaingia msituni kwenye mission walikuwa karibu na nyumba ya mfugaji mmoja ndio akawa anawapa misaada midogo midogo kama chakula na maji na makazi sasa walipoanza safari ya matumaini yule mkulima akawachoma, akaenda kutoa taarifa police na kuwaelekeza walipo, na hapo tukumbuke kuwa CIA walikuwa teyari wapo Bolivia hivo baada ya kupata hizo habari wakafanya ambush na kushambulia kikundi cha che na kuuwawa wengi wao na kubaki wachache
Baada ya kuona hivo che aliamua kutoa vijana wawili waende kutafuta namna ya kuwasiliana na fidel ili awape msaada ila wakati wako njiani wakatekwa, na msitu nzima umezungukwa, hivo fidel hakupata huo ujumbe na huku che amekaa anasubil msaada wa ndugu yake fidel
Kumake story short che alikamatwa akiwa na msaidizi wake na kufungiwa kwenye shule ya primary huku wanajeshi wakisubili order kutoka Washington DC, walilala hadi kesho yake ambapo order ilitoka che auwawe, kiongozi wa kikundi alimfata che na kuongea nae kuwa ameambiwa amuue ila ye akasema hawezi kumuua kwa mkono wake maana anajua che ni nani na asingependa mumtoa roho mwana mapinduzi
CIA alitoka nje na kuweka pozi kisha akapigwa picha na che then akamrudisha ndani nakumwambia commander I'm sorry i tried my best kuhakikisha unakuwa hai ila imeshindikana, che akasema usijali tekeleza majukumu yako, je una ujumbe wowote kwa ndugu na jamaa che akasema mwambie mke wangu aolewe na mtu mwingine na awe na furaha "kumbuka mama yake alifariki che akiwa msituni Bolivia"
ila CIA Rodriguez hakuweza kumuua basi alitoka nje kutafuta volunteers wa kumuua che, ndipo akajitokeza askari mario torano na kupewa maelekezo wapi ampige risasi na wapi asimpige, dogo akaingia class na kumuwasha shaba che huku akiwa kauma kiganja chake ili asilie kwa sauti, ndipo akala risasi 9
Na kabla hajala shaba che alisema "shoot coward you only gonna kill a man but you can't kill my ideas"
ila hapo habari zilikuwa zimeenea kuwa che aliuwawa msituni kwenye mapambano ila haikuwa kweli, ndipo fidel alipopata taarifa za che kufariki ila hakuamini kuwa che anaweza kuuwawa vyepesi namna hiyo ndipo walipokata viganja vya mikono ya che na kutumwa Cuba ndio fidel kuamini na kuutangazia uma kuwa che amefariki
Mwisho, che alikuwa haamini Dini ila alisaliwa na padre wa roman kwakuwa tu wengi walikuwa wanampenda che na kuamini kuwa jamaa hakuwa terrorist