Mke wa Waziri Mkuu wa zamani wa Ukraine adaiwa kujaribu kutorosha mamilioni ya dola

Mke wa Waziri Mkuu wa zamani wa Ukraine adaiwa kujaribu kutorosha mamilioni ya dola

brazaj

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2016
Posts
31,698
Reaction score
41,733
Ama kweli ni kipi kilicho bora kuliko pesa? Wengine wakisema pesa ni sabuni ya roho.

Hizi si ndiyo chimbuko la tozo? Ndiyo chimbuko la kung'angania madaraka? Chimbuko la wizi wa kura? Chimbuko la kukataa katiba mpya?

Hawa ni wa Ukraine mbona hata kwetu ni hivi hivi?

IMG_20220320_232046_864.jpg


Hapa mke wa mbunge mmoja wa zamani wa huko amevuka na kitita cha zaidi ya $28m cash.

Kwa kazi zipi wapendwa wanaweza kujikusanyia ukwasi kama huu yumkini wawapo madarakani?



Uzoefu umeonyesha neno uzalendo ni mahsusi kabisa kuhalalisha wizi wao. Hamna lolote.

Yumkini ndiyo sababu kiapo ni kutokutoa siri unazoweza kutokea kuzijua uwapo huko.

Kulikoni siri wakati nchi wenyewe ni sisi?

Si huko au huku, wote ni baba mmoja mama mmoja.

Mijizi mitupu!
 
Unapitishaje mzigo Kama huo kizembe hivyo..?
Hajua Kama sikuhizi kuna fedha mtandao! Ila dah! Waliomkamata nao wanamoyo na shida nilizonazo hizi nisile miburungutu minono hivyo..😀
 
Mke wa waziri mkuu wa zamani kichwa cha habari alafu habari mke wa zamani wa waziri mkuu kipi ni sahihi tuelewe

Kwani wewe umeandika je mkuu?

Au ungependa marekebisho sasa?
 
Pamoja na kwenda kuedit ili uje kusema hujakosea still bado haileti maana
Jifunze kukubali makosa

Kwamba? Kimeumana eeh?

Heading siwezi kuedit. Wewe umeboronga hata kabla ya kuedit, umekuja kunirukia miye?

Jikite kwenye mada mjomba.

Au nyie ndiyo ile mijizi yetu kwamba siri sirini huku mnakwiba?
 
Mkuu zidi kushangaa. Mke wa Ngeleja alitaka kupitisha mabilion kwenye mabegi JkNIA kupeleka Nairobi TISS wakamzuia kwa kuwa mume wake alikuwa waziri wa nishati na madini wakamshauri azipitishe Namanga

Wewe unadhani kama baada ya kufa Magufuli upekuzi ungefanywa nyumbani kwake Chatto na D'Salaam unafikiri wangekuta magunia mangapi ya $$$$$$$$$$DOLLAR? Hizo alizokamatwa nazo huyo mama wa UKRAINE zingekuwa chamtoto!! Huko Msoga pengine hivyo hivyo kuna masefu yamezikwa kwenye mazizi ya ng'ombe ; ndio maana hairuhusiwi kupiga picha kijijini kwa Mjomba!!! Wanasiasa wanajitajirisha kwa wizi!
 
Back
Top Bottom