Mke wako wako asikuzidi jina, nyumba yako itambulike kwa baba au mzee fulani na sio kwa mama au bibi fulani

Hamna lolote. Awe na jina au niwe na jina, it doesn't matter. What matters ni kutimiza wajibu kama wanandoa na wenye familia. Mimi na mke wangu (kwa kadiri kila mmoja wetu anavyojaliwa) tuna 'common fund' na tunatumia hizi fedha kulingana na mahitaji ya familia na personal upkeep na tulifanya hivi kuepuka mmoja kumwomba fedha mwingine kusema: naomba nauli niende kwetu, naomba elfu...niende saluni, naomba kiasi...ninunulie nguo, etc. Sitaki niombwe fedha na mke wangu au mimi nimwonbe fedha. I feel embarrassed kuomba au kuombwa fedha. Of course, kuna tunayoshauriana kuhusiana na mahitaji ya kila mmoja wetu.
Mimi au mke wangu, mmojawapo anaweza kununua vitu vya kutumia nyumbani au kuwanunulia watoto nguo etc. Sisi tulitaka kila mmoja wetu aishi kwa amani na asijione anashindwa kufanya ABC na we are happy with our system, ambayo watoto wakiona mama ndiye amenunua vitu watasema "asante mama" na wakiona baba ndiye kanunua watasema "asante baba" -but the money comes from the common fund. Mimi sina interest na kuwa na jina. Interest yangu ni kutimiza wajibu wangu kama mzazi mwenza na lugha yetu kwa watoto ni "tumenunua ABC kwa ajili yenu." Mashindano ya kuonyeshana nguvu kuliko mwingine sisi hatuna na mara nyingi tunasema "tunaendesha familia yetu 'kijamaa' (kwa maana ya kushirikiana for the common purpose/wellbeing of the family). Kwa umri nilionao mimi (siyo kijana though) sioni sababu ya kuwa na power struggle katika ndoa/familia yetu - watu waseme whatever they can say, I don't care. What I care about is our wellbeing.
 
Mtoa mada:
1. Wanawake ni waongeaji sana na kiasili kabisa mwanamke ni Extrovert au waweza kumwita Sanguine hivyo ni rahisi wao kuingia kwenye jamaii.

2. Wanaume tunakwepa kujulikana sababu tunakwepa majanga mengi yakiwemo madeni na mimba za michepuko. Hivyo kwako kukijulikana kirahisi inakuwa rahisi kuingia mtegoni.

3. Mmiliki wa jengo ni baba ila mwenye nyumba ni mama. Mwanaume muda wote haupo nyumbani.

4. Namaliza kwa mfano huu: Mfano umefika nyumba kwako mke wako hayupo baada ya muda akarudi ukamuuliza ulikuwa wapi? Akajibu
*NILIKUWA KWA BABA ELIZA
au
*NILIKUWA KWA MAMA ELIZA
Hapo jibu gani linaumiza zaidi?
 
Mnaweza kuzaliwa watoto 10 kwenye familia lakini jina la mtoto mmoja likawa linawatambulisha wazazi wenu.kwa mama fulani au baba fulani.

Alafu wanawake wanamuda mwingi nyumbani.usitegemee mama wa jilani anamtuma mtoto wake kwa mkeo.anapo muagiza lazima amwambie nenda nyumba ya mama fulani.

Uliposema mfano wa uraisi hii inategemea na mfumo.ujerumani wana raisi lakini kuna watu hawajui kuwa nchi ya ujerumani ina raisi,wao wanamjua kansela wa ujerumani.irani nipia ina raisi lakini hawi mashughuli.UK waziri mkuu ndio maalufu kuliko king/queen
 
Inategemea na jamii pia, kuna jamii zingine hata baba ashinde nyumbani mama aende kazini bado kutajulikana kwa mama fulani huwa zinaitwa Matrilineal society hizi upande wa kikeni una nguvu kuliko, otherwise wengine ni limbwata

Pia huchangiwa na nani kiongozi wa maendeleo kwenye familia, unaweza ukawa mtafuta pesa mzuri ila mambo za kimaendeleo anaongoza mkeo mfano biashara na kujenga idea zote zinatoka kwa mke na usimamizi hapa wachaga wanaongoza hasa akipata mme ambae sio mchaga

Mimi napingana na hawa wanaochukilia kigezo cha kushinda nyumbani kuwa ndio kinacholeta umaarufu si kweli, jina huletwa na jinsi ulivyojenga mji wako na unavyousimamia, mji(kaya) ya mtu sio sawa na biashara au umaarufu wa kipaji au cheo
 
Maisha ni vita....inawezekana nyumba yako inatambulika kwa jina la mkeo kwa sababu mkeo "aliaga vyema kwao..."


#NEVER GIVE WISDOM TO UNWORTHY AS IT IS UNJUST TO THE KNOWLEDGEABLE [emoji2956][emoji7]
 
We jamaa kwani we Ni mwizi unayerudi nyumbani usiku usiku tu
 
Kuna lile kabila fulani lina hiyo tabia, unafanywa mpango kiasi baba unafutika katika uso wa dunia ili jina la mama mwenye nyumba liimarike.
 
Mkuu bandiko zako zitaishi na kudumu miaka nenda rudi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…