Yaani iko hivi
Ukiwa na mke wako mkiwa wawili hacheki kabisa yaani full kununiana full ukauzu
Ila sasa wakiwepo washkaji na marafiki zako wa wa kazini au hata mtaani unakuta tabasamu halikauki usoni mwake
Yaani ni kucheka mwanzo mwisho
Bashasha za hapa na pale hatari yaani hadi unaona aahh
Sasa wakuu hiki ni nini????
Imekaaje hii
Jibu hili ambalo lipo kwa mtindo wa swali ni zuri.Sa unataka anune mbele za wageni jameni???
Huwajui wana-wakeFuraha ipi sasa wakati kila kitu anatimiziwa kwenye ndoa
Ndoa ni ngumu jamani. Acheni tu!Kihekima siri za ndoa hazipaswi kutolewa nje/kujulikana ovyo ovyo bila sababu maalumu.
Kila mwana ndoa anapaswa kuficha siri za ndoa yake.
Hiki kitendo cha kununiana mkiwa pekee yenu halafu mnachangamkiana mkiwa public ni mojawapo ya mbinu ya kutunza siri za ndoa.
Kila jambo ni gumu ukiwa huna ujuzi nalo, halafu kila jambo lina umuhimu wake.Ndoa ni ngumu jamani. Acheni tu!