Mke wangu alirudi kwa ex wake siku ya ndoa yangu

Mke wangu alirudi kwa ex wake siku ya ndoa yangu

nimekutana na mtoto mkali.
Katika kumchallenge nikaona kidogo IQ yake na yangu zinaendana Basi nikafanya kila kitu hatimaye nikatoa mahari na kupanga siku ya harusi.
Labda kama sikuielewa hii line umesema kitu kama IQ zenu zinaendana?,na ni baada ya kum-challenge....right???

Nilitaka nikulaumu kwa nini bado upo nae but niliporudi juu kuupitia tena huu mstari nikajua kumbe wote mlikutana pipa na mfuniko coz kama uliweza kumuona ni smart lakini bado akaweza kukuacha hotel tena siku ya pili ya ndoa akaenda kuuchezea na wewe hadi muda huu hujui ufanyeje kweli mpo timamu ninyi?
 
Yaan humu jf kama umeoa na unamoyo mwepesi unaweza kujikuta siku unarud home unamuacha mkeo na kumfukuza aende kwao maana kilasiku nyuzi za kugongewa wake zinaongezeka mbaka sielewi kila nikiingia jf lazima kwanza nikutane na nyuzi mtu kagongewa mkewake [emoji848]
Kweli kabisa,
Inasababisha vijana wetu wanakata tamaa ya kuoa kabisa, ndo zimekua magereza Sasa.
 
Mkuu umefunga ndoa tarehe 29 june,ila bado unatafakari hatua za kuchukua hadi Leo! Au ulimaanisha tarehe 29 December labda...BTW inawezekana hukumkaza vizuri (ungekaza vizuri asingekuwa na nguvu ya kwenda kwa jamaa siku iliyofata)
Mwanamke mchepukaji hata akazwaje hiyo ni kama tabia tu, hawezi acha.
 
usitoe mahali wala kuwai ndoa mpaka utakapo lizika .ni wengi wanajikuta wakijilaumu
 
Dah pole sana Mkuu. Natarajia kuoa mwezi w 3. Hii itakuwa ni ndoa ya 3. Sugu kazini..lakini.........ok pole! Ukifikia muafaka kuhusu adhabu anayostahili G usisite kutustua. Ipo Package ajili ya watu kama hao. Kuhusu Mkeo utajua mwenyewe cha kuamua.
 
Pole sana,huyo ni ex mmoja,uliyemjua.Pole sana,mi ninachokushauri,muache ili akaolewe na George,ninavyojua George nae atamkataa ila atataka awage anamla,hivyo atakua msimbe,atakua anaokoa WADAU wakitingwa.
 
pole sana mdogo wangu ulioa mke wa mtu,Mungu akutie nguvu.
Mshukuru Mungu umejua mapema kwa hiyo usikurupuke kufanya maamuzi kwa kuwa hukuoa bikra basi lolote laweza kutokea
Ushauri wangu,muite mueleze kuwa unajua kila kitu kuhusu yeye na George kwa hiyo aamue kama anaitaka ndoa ama anamtaka G,hapa najua atajiliza na kusema anahitaji ndoa usiwe na shida mpe misimamo yako kama ifuatavyo
1.Siku nitakayogundua unawasiliana na G,au kufanya mazungumzo yoyote hata kama ni barabarani au umewasiliana ndugu yake basi ndo utakuwa mwisho wa ndoa yetu.
2.hata ikitokea msiba wa George ukaenda msibani na nikajua basi ndoa inaishia hapo.
Mambo ya kuzingatia,jitahidi sana kutompa ujauzito mpaka umejihakikishia kwamba yuko tayari kukaa kwenye ndoa.
Jitahidi kila mara kurekodi mazungumzo yenu mnapokuwa mnakubaliana jambo(weka ushaidi wa kutosha ili ukitaka kuchukua uamuzi basi uwe na sababu)
kaa chonjo ukijua lolote laweza kutokea yaani unaweza kuacha ama kuachwa
 
Nmesoma yote,

1.mkeo kaolewa kwasababu zingine, hajakupenda kwa dhati

2.Mapenz yake kwa huyo George
Ndo maana Yuko radhi kurisk kutoroka na kusingizia ajali ili akamkate jamaa Nyege.

3.Uyo George anakudharau sn,
Katumia mgongo wa honeymoon kukuonesha nguvu aliyonayo kwa mkeo.

4. .....
yaani hii imekuwa too much,George ana dharau sana na mke wake hana akili
 
kaka jina la George ni hatari alishawahi nigongea dada zanGu wote watano yule jamaa roho yake ni mbaya sana[emoji24][emoji24][emoji24]
[emoji1][emoji1][emoji1][emoji1][emoji1][emoji1][emoji1] George mtu mbadi
 
Dalili zote zimeonekana hupendwi,,,ni vile tu kajishkiza kwako ili katika wanawake walio katika ndoa na yeye awemo,,onyesha masculinity wako,,,fanya maamuzi...siyo kuendelea kufikiria hatua za kuchukua.
 
Yaan humu jf kama umeoa na unamoyo mwepesi unaweza kujikuta siku unarud home unamuacha mkeo na kumfukuza aende kwao maana kilasiku nyuzi za kugongewa wake zinaongezeka mbaka sielewi kila nikiingia jf lazima kwanza nikutane na nyuzi mtu kagongewa mkewake [emoji848]
Kugongewa ni balaa zito, wivu tunao lakin ukimchunguza sana mkeo hamuwez maliza salama
 
Nimekwambia hapa hatoki mtu na kama utaniacha basi hutokuja kuoa mwanamke mwingine,Hayo ni maneno ya mke wangu.

Ilikuwa ijumaa tulivuu tukiwa hotel ya Sea cliff baada ya kutoka kwenye sherehe iliyo fanyika hapo hapo hotelin.

Imekuwa ni kawaida ya watu wenye kipato cha kati wakati wa harusi kutafuta sehemu ambayo watasuza mioyo yao baada ya kupitia msoto wa huko uswahilini kwa miaka. Hutumia siku ya ndoa yao kuondoa hizo nuksi kwa kutafuta sehem nzuri yakupumzika baada ya ndoa.

Sherehe ilikuwa baabu kubwa zawadi zilikuwa nyingi majirani na rafiki zangu walinisapoti sana kufanikisha harusi hii tulipata pongezi nyingi.

Hii ilitokana na msimamo wangu niliokuwa nimeuweka kuwa stokuja kuoa mpaka nifikishe miaka (30)lakn haikufika hata (29) nilikuwa tayari nimekutana na mtoto mkali. Katika kumchallenge nikaona kidogo IQ yake na yangu zinaendana Basi nikafanya kila kitu hatimaye nikatoa mahari na kupanga siku ya harusi.

29 June nikiwa nimetulia kwenye suiti nilishona kwa Sheria NGOWI huyu huyu anayekula deal za Jezi za Yanga. Suti imenikaa imetulia kama mnavyojua sherehe zetu huwa zinapangwa kwa mda lakin kufuata huo mda ni changamoto.

Wakwe wamepangiwa kuingia ukumbini saa 1 usiku lakin mpaka saa 1 hiyo inafika hakuna mtu na ni wakwe hawaguswi wanaingia saa 1:45usiku mda umeenda.

Nimepoa kwenye Gari V8 ya mwaka 2018 na wife amatulia upande wa pili tunaongeaa mambo yako safi kabisa.
Shetani alianza kuingilia harusi yangu baada ya DJ kupiga nyimbo ya King Crazy GK ntakufaje ambapo kila mtu alishangaa.

Dj akaomba msamaha mambo yakaendeleea katikati ya harusi akaja jamaa akaning'oneza kwamba Private room kuna mtu anakusubiri nikashangaa harusi inaendelea tena kuna mtu ananisubiri nikazuga baada ya mda nikamtarifu msimamizi wangu nikaenda naye.

Kufika private room maana haikuwa mbali nikamwambia msimamizi naomba mcheki wife ikinyanyuka niambie.Kuingia private namkuta SUZAN huyu ni EX wangu tumeaachana kama 1yrs imepita nikamliza kulikoni.

Akaniambia mbona hupokei simu nikajibu ntapokea vipi wakati unaona shughuli inaendelea ni hicho ndio umeniitia si unajua shughuli ni yangu sitakiwi kuwa mbali.Basi alilalamika nikaona malalamiko yake hayana msingi nikaondoka zangu kurudi ukumbini lakini akaniambia Honeymoon ikiisha atanipigia kuna jambo anieleze.

Sherehe iliendelee wa kunywa walikunywa.Mambo yalikuwa bambam kama unavyojua sherehe hukusanya kila kitu na ambao ulipita nao wanakukata jicho lakin sasa ndio tayari unaaga ukapera unaenda kuuliza ukichelewa ulikuwa wapi.

Kunawengine wanakukumbatia matani ya hapa na pale kama pale FRED alivyonitania kuwa wewe si ulikuwa mke wa J basi mzee baba jiandae kuliwa tena wako waiti Dah mapigo ya moyo yakaenda kasi jumlisha na wivu .Akaja mwingine ni mshikaji oya Adam wamekaa kule nyuma lakini BIA zinaishia hapa katikati fanya mambo si unajua wamejitoa sana.

Mama ambaye ni jirani huyu aliniacha hoi aliniambia wao na kikundi chao gari yao imepata break down kama nina sh.30k niwakopeshe baada ya harusi atarudisha lakin pia alisisitiza hata kama sina basi nimwambie msaidizi wangu ampe zile walizo tunza watu dah.

Harusi ilijaa mambo mengi yani hawa wadau wakilewa ni taabu kila mtu anakuja na lake lakini yote heri mambo yalienda kama tulivyo panga.

Tarehe 31 june niko bafuni wife anapokea simu nikajua mambo ya kawaida ni pongezi lakin baada ya sekunde nikasikia anapiga ukunga. Nikauliza nini tena kuna msiba? hapana GEORGE kapata ajali alikuwa amepakizwa kwenye bodaboda na ndio maana jana hakutokea.

Nikauliza G ni nani ni mtoto wa Ba mdogo na huyu ndio nilisoma naye na kuna wakati alinisaidia sana Zimbabwe tulipo kuwa tunarudi DSM aliniletea stry ambayo hata kama ni wewe ungemwambia basi twende tukamwangalie yupo Hosptal gani?

akanijibu yupo Muhimbili MOI nikasema poa pale nina jamàa Dr. Faraji chapu tuu tukifika atatusaidia kwa haraka. Akasema jana tu harusi leo unahangaika na masimu wewe baki ngoja mimi niende kwa vile gari iko tinted basi hakuna kitakacho haribika basi kama tulivyo shauriwa kule kanisani kwamba mwenzio akiwa anahitaji kufanya jambo fulani mwache atimize maana mzozo huanzia hapo.

Baada kama ya lisaa hivi nikapiga simu ya WIFE ikawa haipatikani nikapiga simu ya wakwe nikawaelezea wakasema mbona sisi hatuna tarifa Duh mapiga ya moyo yakaenda kasi ikafika wakati nikajituliza labda chaji.

Lakini nikikaa naona kama kunajambo halipo sawa why wazazi waseme hawana tarifa hii imekaaje nikajituliza.

Nikarudi kwa wazee kuuliza kuwa kuna tarifa zozote au niende kituo cha police wakasema ni mapemaa mno maana now ni masaa 3 yamepita tusubiri kidogo.

Nimetulia napokea simu nauliza nani SUZAN nikamuliza kulikon si ulisema utanipigia baada ya honeymoon akasema ameshindwa kuvumilia nikamwambia funguka. Taxi pls naomba kama stoeleweka liache kama lilivyo nikamliza mbona unajikanyaga nenda kwenye point akaniambia mkeo anatoka na GEORGE akakata simu.

Nilifikiria na ukitazama SUZAN ni EX wangu maneno yake sikuyatiria maanani maana nilijua nachezewa mchezo basi baada ya kama masaa 5 wife akarudi.

Jambo la kwanza mbona hupokei simu kulikoni akasema chaja si unajua jana tulikuwa busy hatukuchaji ok mgonjwa anaendeleaje Hajambo wamemfunga P.O.P ok naweza mpa pole akasema wazazi wake ndio wana simu zake.

Baada ya kumaliza honeymoon tukarudi home kama mwezi hivi Simu yake ikawa ina shake AIRPLANE NA DISTURB zikawa zinajibonyeza kwa wakati mmoja ikawa hapatikani niliporudi nyumbani nikamliza ndio kaniambia simu ina shida Basi nikamwambia K/koo nina jamaa pale NIZO MATELEPHONE Hizo ndio kazi zake ntamwachia ntapitia baadaye.

Nilipo rudi jamaa akaniambia tatizo ame badilisha kioo na touch inasumbua nikamwambia gharama 50k hii kishikaji nikarudi home lakin kabla sijafika simu inaita G (kifua bega) nikasema hii sipokei atapokea mwenyewe lakin nikajiambia huyu si mke wangu nimetoa mahari why sina uhalali wa kupokea simu zake (kibabe) nikaweka sikioni.

Hello baby mbona hupatikan toka jana kulikoni vipi unaendeleaje je umemaliza kuchinja (period) Dah nikakaa chini maana nilikuwa karibu na home duka la Mangi.

Mangi kuniona akacheka sana akasema yani Yanga bwana mkifungwa tu Ruvu shooting mnakaa chini hivyo je ikiwa SIMBA. Taxi Si utavua nguo wewe.

Nikamwambia Mangi bora tungefungwa nikamliza Mangi mbona nyumban kwangu sipaoni Aisee bwashee unajua umri unaenda huo unatakiwa ukatayarishe mashamba unakaribia kustafuu.Nikaendelee kupekuwa simu nilichokikuta nikajilaum why nilienda kuitengeneza KWELI MKE WANGU ANATEMBEA NA GEORGE NA SIKU MOJA BAADA YA HARUSI WALIKUTANA MOUNT LODGE.

Hii ilinikata kiasi kwamba nipo tuu wiki nipo tu ninachokifanya sikielewi naangalia HATUA ZA KUCHUKUA.
YAANI SIKUMALIZIA IIKABIDI NIFWD HII STORY KWA PAGE YA DK MWAMPOSA ATAJUA SABABU KAMILI HOPE UMEME WAKO UKO SAWA ....KAMA.UMEZIDI NJOOO KAWE KWA MKATA UMEME..HATA KAMA HAUPO KABSA NJOO TANGANYIKA.PKS WATU WANAPONA...
NDOA NDOAN
 
Back
Top Bottom