Kupanic kwako kumekukosesha ukweli wote. Mtu ametuma meseji, unamuuliza wewe nani; anakujibu mimi fulani. Hivi kweli kama ni watu ambao wanawasiliana kila siku, ungemuuliza yeye ni nani si lazima angeshtuka? Hadi anamuomba picha, Ina maana hana picha zake, right? What if baada ya zile chats za wasap ndiyo akaamua kumpigia mkeo?
Shida ni kwamba ulikurupuka; ungetulia nina uhakika ungepata majibu sahihi. Bila shaka ni ex wake, lakini alikuwa ex wa muda gani? What if walishaachana kitambo huko na mwanaume ndiyo amenza kumtafuta sasa hivi?
Usifuatishe mkumbo wa wanaume wa JF; humu wao wanawake hawawasumbuagi, wanafukuza tu. Usijefanya maamuzi kwa hasira na ukawa umemuonea huyo mzazi mwenzako mtarajiwa na mtoto wenu; baadaye ukaja kujuta. Punguza hasira, utapata wakati mzuri wa kudigest hili. So far sijaona ushahidi wowote kuwa mkeo amechepuka na huyo mwanaume akiwa kwenye mahusiano na wewe.