Mke wangu amenibadilikia, anataka talaka (ushauri)....... (Na ushauri wa mdau)

Mke wangu amenibadilikia, anataka talaka (ushauri)....... (Na ushauri wa mdau)

matuya06

New Member
Joined
Aug 12, 2026
Posts
1
Reaction score
2
Habari hii nimeitoa fb, huyu jamaa anatafuta ushauri, ila ushauri wa "Simon" kama utakavyo usoma hapo chini, haukuwa wa KISTAARABU kwa uelewa wangu na kwa utu wangu mimi!

Hebu na wewe naomba soma hiyo stori umshauri mhusika na bila kumsahau na "Simon" pia ashauriwe.



Niwe muwazi tu mimi nateseka sana, mke wangu amenibadilikia kitu ambacho sikuwahi kufikiria kabisa kwenye maisha yangu.

Mimi na mke wangu tuko kwenye ndoa huu ni mwaka wa Saba, na tulikuwa hatuna changamoto yoyote, tuna Watoto wawili

Mwaka juzi aliniambia amechoka Kushinda nyumbani hivyo anataka kufanya Biashara, nikamuuliza unataka kufanya biashara Gani? Akaniambia yeye hana wazo lolote la Biashara ila akaniambia nifungue Biashara yoyote nimfundishe namna ya kuifanya, nikasema sawa.

Kwa vile nilikuwa na wazo la kumiliki duka la spea za Pikipiki ikabidi nifungue, tukawa tuna Shinda nae pale Dukani, na kweli ni Biashara ambayo ilifanikiwa ndani ya muda mfupi sana, nilikaa hapo Dukani mwaka mzima nikaacha Biashara zangu zingine Kwa sababu zenyewe zilikuwa Zina jiendesha tayari.

Sasa mwaka Jana akaja kuniambia eti ameona atafute kazi yake mwenyewe ambayo hainihusu, nikamuuliza kazi gani? Akaniambia rafiki yake kamtafutia kazi ya Ukonda Wa basi za kwenda Mikoani, alivyo nijibu hivyo nilijua anatania, ila kuanzia hapo akawa haendi Dukani tena.

Siku Moja niko kazini jioni akanipigia simu anaenda kuanza kazi, na siku hiyo nilivyo rudi nyumbani sikumkuta ndo akawa amesafiri.

Huo mgogoro uliendelea mpaka mwezi wa 4 mwaka huu huku Mimi sitaki afanye kazi hiyo, lakini aliendelea kushikilia msimamo wake na mwisho akaamua kuondoka kwangu akaenda kupanga, akaniachia watoto wote.

Sasa nimeambiwa anafuatilia talaka Ili tugawane Mali, juzi Kuna mwanasheria wake alifika nyumbani kwangu na wamesha nipigia simu mara tatu ila sitaki kuwapa ushirikiano.

Najiuliza kosa langu nini? Mke wangu nilinunua gari Kwa ajili yake Mimi nikawa natembelea Pikipiki, mke wangu alitaka nifanye nini nionekane mwanaume kwake? Mbona alikuwa anavaa na nilimpa uhuru wa pesa?

Najua ataona hii post ila nimwambie tu kinacho niumiza siyo hizi Mali na Wala siyo uzuri wake bali ni hawa watoto, na nikuambie tu Kila ninapo watazama hawa watoto najikuta natamani kufanya maamuzi magumu, sikuwahi kufikiria kuwa na watoto ambao mama Yao yuko mbali, nateseka sana ninapo waona watoto wana lelewa na dada wa kazi nakosa amani nikiwa sipo, natamani mama angekuwa hai.
 
Mwambie aoe huyo house girl alee watoto maisha yaendelee. Huyo ameshakuwa chakula Cha madereva na mawakala hivyo hawezi kusikia Tena chochote utakachosema. Na nyuma yake Kuna washauri wengi sana. Funga ukurasa achana nae. Suala la malipo hakuna kugawana we sema ni sehemu ya kulea watoto. Achana na stress hizo we kuka maisha
 
Mwambie aoe huyo house girl alee watoto maisha yaendelee. Huyo ameshakuwa chakula Cha madereva na mawakala hivyo hawezi kusikia Tena chochote utakachosema. Na nyuma yake Kuna washauri wengi sana. Funga ukurasa achana nae. Suala la malipo hakuna kugawana we sema ni sehemu ya kulea watoto. Achana na stress hizo we kuka maisha
Nadhani ushauri huu aupigie mstari na auzingatie.

Ndoa ni mkataba wa hiari ambao hakuna sheria inaulazimisha kuendelea.

Haya mambo ya kusema "watoto' ni kisingizio tu ili kuficha udhaifu wake wa kumpenda mwanamke huyo kupindukia na akikaa peke yake 'off line', huyo mwanaume lazima huwa analia sana.

Kwani mwanamke huyo angelikufa asingelea watoto wake?

Na ni mwanasheria gani huyo anayefuatilia ndoa za watu badala ya kupokea samansi ya wito wa mahakamani, ambayo nayo itakuwa imekiuka procedure za mwenendo wa mashauri ya talaka?

Kuna utapeli mkubwa umepenyezwa kwenye ndoa hiyo kwa kupitia mwanamke.
 
siku zote mwanamke wako akianza kureta dharau na yeye mwenyewe kutaka muachane huyo muache na uheshimu maamuzi yake lasivo litakukuta jambo baya
 
Back
Top Bottom