Robert Heriel Mtibeli
Platinum Member
- Mar 24, 2018
- 40,153
- 93,069
MKE WANGU AMENINYANG'ANYA SIMU AMESEMA ATANIRUDISHIA MPAKA UCHAGUZI UPITE. HATAKI YANIKUTE!
Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli.
1. Kiukweli nimetukanwa na wadau sana. Wanasema mke wangu ameniweka kiganjani. Amenikalia na sifurukuti.
2. TaikonMaster unawezaje kunyang'anywa simu na mwanamke?
3. Aaah! Kiukweli niligombana naye lakini ikafikia hatua akaivunja siku ya kwanza. Tukagombana sana. Nikakaa muda natumia kiswaswadu. Wengine wakaona nipo kimya. Members baadhi wa JF wakasema labda nimetekwa, wengine wakasema sijui kutumia VPN. Basi kila mtu na hisia, maoni, mtazamo na uelewa wake.
4. Baadaye nikanunua simu nyingine ya bei nafuu kabisa. Mke wangu akaniambia nisipost mambo ya siasa mwezi mzima mpaka uchaguzi upite. Nikamwambia kwa nini?
5. Akaniambia akiwa anamnukuu Kikwete " Sio kama sisikii yanayosemwa, sio kama sioni" kumbe anaona na kusikia taarifa za watu wanaotekwa na wengine kukutwa wameuawa.
6. Nikamwambia lakini mimi sipo Radical. Akasema hata kama. Basi nikakubaliana naye sitapost chochote kuhusu siasa.
7. Baadaye kidogo kama siku kadhaa kupita nika-post unajua sisi waandishi na wapenda haki tunakuwa na kitu kule upareni kinaitwa kidughusha, tunakereketwa, tunawashwa, kunakuwa na msukumo wa ndani unatulazimisha kuandika hasa tukiona mambo hayaendi sawa.
8. Akaingia kwenye akaunti yangu akafuta. Ni kweli mimi na mke wangu kila mtu ana uwezo wa kuingia kwenye akaunti ya mwenzake. Akiamua kupost akiamua kufuta anafuta.
9. Oooh! Robert so kumbe tukimfuata mkeo unajua na husemi, unatuchora! Hapana siwachori. Au kumbe hakuna siri tukikutumia ujumbe maalum. Siri ukitaka ni kunipigia simu. Lakini meseji kwa kweli hakuna siri.
10. Ndio maana umekaliwa... Mjinga wewe. Sawa! Mtazamo wako ni sahihi kabisa kwa watu wa aina yako lakini haiongozi mfumo wote wa Jua.
11. Kwa nini umefuta ile post? Nikamuuliza. Oooh! Tulikubaliana hutopost kuhusu siasa. Nikamwambia hatukukubaliana ila wewe ndio uliniambia. Akajibu ndio nilikuambia ukakubali.
12. Wakaitwa wazazi, na wazee, nikanyang'anywa simu. Nimeambiwa namnyanyasa mke wangu. Kwa nini simsikillizi kwenye jambo nyeti kama hilo.
13. Madai ya mke wangu, wazazi, wakwe na wazee ni kuwa ninahatarisha usalama wa familia kwa kuingia kwenye anga la washenzi. Unaambiwa huko siasani kuna watu washenzi wasiojali wala wasioogola. Wasiosita kuua na kufanyia unyambisi.
Ndivyo nilivyoambiwa.
14. Nikaambiwa, tazama wewe bado ni kijana mdogo, una malengo mengi, mtazame mkeo alivyo mzuri na mbichi. Hapo nikakatazama ka mke kangu. Jamani! Ni kazuri sana. Nikaambiwa unataka ukaache kajane kaanze kuhangaika.
Nikawaambia kwani wajane wote waliachwa kwa waume zao kuongelea siasa?
15. Nikanyamazishwa! Muda huo ikatolewa simu nyingine ndogo. Nikaambiwa utatumia hiyo.
16. Akaendelea yule mzee wa Ukoo.
Unamwona Mke wa Mdude na watoto wake? Unawajua wazazi wake? Unamuona mzazi wa Polepole jinsi anavyoteseka.
Nikawaambia nawaona!
17. Hatutaki tuteseke kama wao. Acha hayo mambo Robert.
18. Lakini mimi ni mtibeli. Nikajibu
19. Mtibeli ya nyokwe! Sisi ndio tulikuzaa. Na huyo mke tulikukabidhi sio umuache mjane au Yatima kwa upuuzi wako.
20. Kutetea Haki za watu ni upuuzi? Wazee nini hiki?
21. Wakafungua post yangu moja niliyoandika miaka kadhaa iliyopita. Inakichwa kisemacho Kamwe usitetee Maskini na wapumbavu.
Unaikumbuka? Wakaniuliza.
22. Lakini
23. Hakuna cha lakini. Hutotumia simu janja mpaka November 5 ndio tutakupa simu yako.
24. Pia tutahakikisha tunakuwekea mtu wa kukusaidia ili uzoee hali ya kutokuwa na simu janja. Ili usipate Arosto.
25. Mke wangu akaingilia kati. Yaani nashukuruni Wazee wangu kwa kunisaidia.
26. Fikiria sasa hivi angekuwa ameshatekwa huko mimi nahangaika hapa pekeangu
27. Nikawauliza kwa hiyo nyie mnafurahia kuona watu wengine wanatekwa na kuuawa?
28. Wakajibu wakasema tungekuwa tunafurahia tusingekuzuia na kukunyang'anya hii simu ili nawewe utekwe na kuuawa.
29. Wameniambia tarehe 27 nitakuwa na safari kuelekea Gaborone, Botswana. Nafikiri Lengo lao nisishiriki maandamano.
Wanajua ati mimi nitashiriki maandamano. 😂
30. Ndugu wa mitandaoni hali kwa upande wangu iko hivyo.
31. Licha ya kuwaambia mimi kupost napost kwa lengo jema kabisa na lengo la uzalendo wa kitaifa.
31. Professa aliyenifundisha fasihi kutoka pale udsm akaniambia ninachoandika na kumaanisha ni jambo moja. Alafu msomaji anachosoma na kutafsiri ni jambo jingine. Akaniambia alinifundisha maana kutoka kwa msomaji haiwezi lingana kati ya msomaji mmoja na mwingine.
32. Nikamwambia nakumbuka ulinifundisha hivyo. Basi sikiliza wazee wako kwanza. Kifungo cha mwezi mmoja kwani shi.ngapi?
Alaaah! Dadeki! Nimesahau leo ni sabato. Ndugu zangu. Hii simu nimeiazima huku kanisan kwa muumini ili niingie mtandaoni humu niwape kinachoendelea.
Haleluya! Sabato njema!
Taikonmaster
Kwa sasa Dar es salaam