Equation x
JF-Expert Member
- Sep 3, 2017
- 33,679
- 49,841
Nipo mkoa wa huku kusini kwenye harakati zangu za utafutaji,nikaingia mtaa mmoja wa nyama choma; ile harufu ya nyama ikaufadhaisha mwili wangu, kuangalia mfukoni nina elfu tano tu, na kwenye simu sina salio lingine.
Wazo likanijia nimpigie simu mama k; ile kupokea simu tukaanza kujuliana hali, nikamwambia hapa nilipo nimepita mtaa x nimekutana na harufu ya nyama choma, naomba uniwezeshe salio, langu halisomi.
Akasema subiri, baada ya dakika tatu ikaingia salio la kuniwezesha kula na kunywa, akanipigia na kuniambia, kesho nitakuwa vizuri zaidi nitakutumia fungu kubwa.
Nikaishiwa nguvu, na kuanza kujiuliza kwa nini naangaika na michepuko inayokula hela zangu tu na hainisaidii; kweli mke wangu ametoka kwa bwana.
Michepuko siitaki tena; wkend itabidi nimpeleke mbugani akaangalie wale ndege jamii ya korongo ambao hawaachani mpaka wanapokufa, na akifa mmoja wapo yule aliyebaki anabaki hivyo hivyo mpaka mwisho wake.
Kama mkeo au mpenzi wako wa kike hakutumii hela, huyo hajatoka kwa bwana, bali ametoka kwa shetani.