Mke wangu ana kadi mbili za kliniki, moja jina langu, lingine la bwana mwingine!

Mke wangu ana kadi mbili za kliniki, moja jina langu, lingine la bwana mwingine!

Tembelea vituo vya afya ukachunguze afya yako hasa uzazi pengine mkeo alipona mnakaa ndani ya ndoa pasipo mafanikio ya ujauzito akauza mechi sasa yupo njia panda ajui mimba yako au ya jamaa maana wote mlikuwa mnamtumia

yes umesema vyema WANAMTUMIA - coz tumehalalisha mwanamke ni kimachine sio....weledi katika hili muhimu,,, jamaa keshazama,,,,,anaomba msaada...
 
Habari wanajamvi,

Nimeamini usemi usemao usione watu wanaangua vicheko barabarani na wakati mwingine hadi machozi yanawamwagika kutokana na sababu mbalimbali, Ni kweli kwamba yapo machozi ya furaha lakini pia machozi mengine ni uchungu unaoonekana kama aina fulani ya furaha.

Mtu anaweza kucheka lakini siyo kweli anacheka kutoka moyoni bali anajaribu kuficha yanayomkera lakini katika kujipa moyo anashiriki kicheko pale anapozungumza na jamaa au rafiki yake.Huo ni ukweli.

Ushiriki huu wa kicheko, hakika humpunguzia mawazo fulani kwani vile nijuavyo mimi kicheko ni afya. Hufanya hata makunyanzi kwenye uso kupotea kwa muda.

Lakini pia kipo kicheko cha ukweli kinachotokana na jambo fulani la kufurahisha alilokujulisha mwenzako na katika kuonyesha wingi wa furaha, chozi nalo hujikuta likimwagika. Je, imewahi kukutokea hivyo? Mimi Yes!mara nyingi tu.

Naam, nimeanza hivyo ili kukuweka sawa kwa kile tutakachojadili hapa chini kwamba usione watu wanapita barabarani, wako maofisini wakichapa kazi ukadhani wana furaha tele moyoni.

Pale kazini wanajitahidi au niseme wanajitutumua tu kutimiza wajibu lakini baadhi wanapofikiria kule majumbani wanakotoka, mapigo ya moyo huenda mbio na afadhali kama angeambiwa apige mbio lakini yanamdunda wakati katulia tuli. Kisa amekumbuka vitimbi vya nyumbani kwake.

Mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 28, nimejaliwa kufunga ndoa na mke wangu miaka 4 iliyopita, ingawa tumechelewa kupata mtoto lakini ndoa yetu ina upendo na amani ninaishi Dar.

Mwezi wa Machi mwaka huu, mke wangu alifanikiwa kupata ujauzito kitu ambacho kimeongeza upendo ndani ya nyumba yetu na mimi najitahidi kadri ya uwezo wangu kuhakikisha mke wangu anapata mahitaji yake yote muhimu kiasi kwamba hakuna kitu anachokikosa.

Hata hivyo, kilichonifanya niombe ushauri kutoka kwenu wana JF kwa ujumla, ni kwamba hivi karibuni nimemfuma mke wangu kwenye kabati lake la nguo nimekuta ana kadi mbili za kliniki, moja ina jina langu na ya pili ina jina la bwana mwingine hizo kadi zote kaziandikisha vituo tofauti vya Afya (Majina ya yule bwana mwingine ninayo).

Angalia Mungu alivyo mwema, amenielekeza hadi nikaziona kadi zile kunidhihirishia kuwa mke wangu siyo mwaminifu na lipo au yapo mambo mengi labda bado ananificha.

Kwa kweli baada ya kuzifuma kadi hizo nilichokifanya nilizirudisha nilipozikuta na mpaka hivi sasa mke wangu hajui chochote kinachoendelea.

Ndugu wanajamvi Madam B, Watu8, @KakaKiiza, KakaJambzi, FROWIN, Tutor, ASHUA, na wengineo, mwenzenu yamenikuta nimebaki njia panda kiasi kwamba nashindwa la kufanya. Naombeni ushauri wenu kabla sijachukua uamuzi wowote.

Wasalaam.

Wewe Ni Muongo!

mkuu pole sana,,, kwanza hujachelewa kama ambavyo wengi ya wachangiaji wasemavyo.....ila kikubwa kapime uwezo wa manii zako,,,, sehemu 3 tofauti....ujiridhishe,,, copy ya hizo kadi ni muhimu sana fanyia kazi haraka,,, hili silipendi ila nakushauri fanya, fuatilia nyendo zake kwa makini,,, u might hire a spy kimya kimya... ni gharama but unatafuta ukweli.....kulea mimba ya mtu mwingine inauma nyie....duh...najua unaumia sana @ this time coz hujui nini kinaendelea, la msingi na kwa usalama wako,,,kuna HIV....utajishauri mwenyewe....

Hawa viumbe hawa.......they make us crazyyyy... pole mkuu na jiandae kuseparate...
 
Ndugu mwanajamvi pole sana na maswahibu yote yaliyokukuta. Kwanza nikupongeze kwa hatua stahiki uliyoichukua. Umetumia busara ya hali ya juu. Ni kweli kuwa matatizo kaumbiwa mwanadamu. Mimi binafsi ninao mtazamo mdogo unaoweza kurejesha heshima ya ndoa na faragha yako. Naomba ukipenda na kuweza ufanye yafuatayo:

1. Hakikisha unatoa soft copies za hizo kadi na uzitunze kama backups in case lolote litatokea.

2. Baada ya hapo fanya utaratibu wa kupima DNA ili kujiridhisha kuwa huyo mtoto mwenye jina lako ni wako au la! Maana inawezekana naye pia akawa ni changa la jicho.

3. Ukifanikiwa hilo pasina mkeo kugundua chochote, fanya mpango wa kutafuta software inayoweza kufanya hacking ya mawasiliano yake yote, iwapo anatumia smart phone, ili uweze kujiridhisha kuwa si mwaminifu.

4. Kama utapata ushahidi wa mawasiliano yake yote yasiyo rasmi na yenye utata, tunza kumbukumbu zote kama ushahidi, kisha mtafute mshenga/mpambe/kiongozi wa dini au Mzee yeyote unayemuheshimu akupe muongozo zaidi.

5. Itakuwa busara zaidi, kama mambo hayatakufurahisha, ufanye mpango wa kuwaambia wazazi/walezi wako (kwa ushahidi wote) kabla ya kuyafikisha katika familia/ukoo wake.

6. Mwisho kabisa hakikisha yamefika kwao na vikao shirikishi vifanyike kutafuta suluhu ambayo haitaathiri ndoa yako. Msamaha ama kinyume chake itakuwa ni maamuzi yako binafsi, kwa msukumo wa nafsi yako, yatakayotokana na uzito wa jambo husika.

Nitashukuru kama nimesaidia kitu.
 
Nadhani umepewa ushauri mzuri saana, However, kuwa makini saaaana coz inawezekana kweli mzee unatatizo la uzazi na wife akaaamua kutoa kiaina ili upate mtoto bila wewe kuhisi kama una tatizo la kuzalisha mtoto...

Nimekuelewa pia Mkuu, tuko pamoja ila nahisi wife kuna labda mtu anampanganya ili achepuke.
 
Wataalamu wa mambo ya DNA wanasema ukichukua watoto 50 ukawapima DNA asilimia 40 ya watoto baba zao watakuwa siyo wale tunaowajua. Ndiyo kusema hata sisi wengine ambao kwa bahati nzuri tu hatujagundua kilichoko nyuma ya pazia wengi wa watoto tena tunaowapenda pengine siyo wetu, hiyo ni siri ya akina mama. Siku Mungu akija kuamua kuwaumbua watu wengi tutakuwa kwenye mfadhaiko mkubwa. Hilo ni tatizo nyeti, kama hadi sasa hujachukua hatua yeyote ya hovyo, kuwa mvumilivu, kuwa mpole ukipenda pepeleza la hupendi kupeleleza acha mambo yaende yalivyo ili mradi kuna kitu umegundua hadi hapo Mwenyezi Mungu atakapokuonesha vinginevyo. Unaweza ukapaniki kumbe mambo hayako kama unavyofikiria.
 
Attachments

  • 1435696754285.jpg
    1435696754285.jpg
    33 KB · Views: 143
Kama unatatizo la uzazi wewe mezea kitanda hakizai haramu=nimilija atinangunda =kibarua hana shamba ,wewe poa usiwe mkali
 
Habari wanajamvi,

Nimeamini usemi usemao usione watu wanaangua vicheko barabarani na wakati mwingine hadi machozi yanawamwagika kutokana na sababu mbalimbali, Ni kweli kwamba yapo machozi ya furaha lakini pia machozi mengine ni uchungu unaoonekana kama aina fulani ya furaha.

Mtu anaweza kucheka lakini siyo kweli anacheka kutoka moyoni bali anajaribu kuficha yanayomkera lakini katika kujipa moyo anashiriki kicheko pale anapozungumza na jamaa au rafiki yake.Huo ni ukweli.

Ushiriki huu wa kicheko, hakika humpunguzia mawazo fulani kwani vile nijuavyo mimi kicheko ni afya. Hufanya hata makunyanzi kwenye uso kupotea kwa muda.

Lakini pia kipo kicheko cha ukweli kinachotokana na jambo fulani la kufurahisha alilokujulisha mwenzako na katika kuonyesha wingi wa furaha, chozi nalo hujikuta likimwagika. Je, imewahi kukutokea hivyo? Mimi Yes!mara nyingi tu.

Naam, nimeanza hivyo ili kukuweka sawa kwa kile tutakachojadili hapa chini kwamba usione watu wanapita barabarani, wako maofisini wakichapa kazi ukadhani wana furaha tele moyoni.

Pale kazini wanajitahidi au niseme wanajitutumua tu kutimiza wajibu lakini baadhi wanapofikiria kule majumbani wanakotoka, mapigo ya moyo huenda mbio na afadhali kama angeambiwa apige mbio lakini yanamdunda wakati katulia tuli. Kisa amekumbuka vitimbi vya nyumbani kwake.

Mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 28, nimejaliwa kufunga ndoa na mke wangu miaka 4 iliyopita, ingawa tumechelewa kupata mtoto lakini ndoa yetu ina upendo na amani ninaishi Dar.

Mwezi wa Machi mwaka huu, mke wangu alifanikiwa kupata ujauzito kitu ambacho kimeongeza upendo ndani ya nyumba yetu na mimi najitahidi kadri ya uwezo wangu kuhakikisha mke wangu anapata mahitaji yake yote muhimu kiasi kwamba hakuna kitu anachokikosa.

Hata hivyo, kilichonifanya niombe ushauri kutoka kwenu wana JF kwa ujumla, ni kwamba hivi karibuni nimemfuma mke wangu kwenye kabati lake la nguo nimekuta ana kadi mbili za kliniki, moja ina jina langu na ya pili ina jina la bwana mwingine hizo kadi zote kaziandikisha vituo tofauti vya Afya (Majina ya yule bwana mwingine ninayo).

Angalia Mungu alivyo mwema, amenielekeza hadi nikaziona kadi zile kunidhihirishia kuwa mke wangu siyo mwaminifu na lipo au yapo mambo mengi labda bado ananificha.

Kwa kweli baada ya kuzifuma kadi hizo nilichokifanya nilizirudisha nilipozikuta na mpaka hivi sasa mke wangu hajui chochote kinachoendelea.

Ndugu wanajamvi Madam B, Watu8, @KakaKiiza, KakaJambzi, FROWIN, Tutor, ASHUA, na wengineo, mwenzenu yamenikuta nimebaki njia panda kiasi kwamba nashindwa la kufanya. Naombeni ushauri wenu kabla sijachukua uamuzi wowote.

Wasalaam.
Rip mkuu
 
Back
Top Bottom