Mke wangu ana ujauzito wa mwezi mmoja tuu lakini nanyooka

Mke wangu ana ujauzito wa mwezi mmoja tuu lakini nanyooka

Tuko pamoja mkuu mimi wangu ina miezi kama 2 lakini nanyooshwa balaaa yani ye mda wote anadai anajiskia vibaya ... ila kuhusu gemu kuna mda anataka mwenyewe nimnyandue kuhusu gemu wangu hana tabu ..
 
Hivi wadau ni sawa kwa mwanamke mwenye mimba ya mwezi mmoja kuanza uvivu na kuumwa umwa!!

Naona mwanamke wangu ananiletea vipengele sana yaani tangu tujue ana mimba basi kazi zote za ndani ndio hawezi tena….hapiki hafui hadeki…vitu vyote hivyo nafanya mimi. Mara ajitapishe mara aseme anasikia kizunguzungu mara agome kula.

Yaani ni kama wiki mbili sasa lakini nimeshanyooka. Game nanyimwa kwa kisingizio kuwa anajisikia vibaya

Ni kweli inakuwa ivi sometimes au ndio nanyooshwa!!?
Ulifanya tendo pasipo ndomu? Aaaah!
 
Yes avumilie mkuu mimi , pasaka nilifukuzwa ndani , nlichukua vitu vyangu nkasepa .. two days later napigiwa simu Rudi nyumbani ukwapi ... Nimefanya shughuli nyingi Sana mwanzoni niliona kero ila nashukuru Nilikuwa karibu sana na mama yangu kupitia simu kanitia moyo Sana .. na miezi tisa ikatimia.

Na Ili uone umuhimu wa kitu lazima ukipambanie ...

Naongea Sana ila nini ... Hakuna wa kuniambia chochote KWA mwanangu [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] nampenda

[emoji1787]
 
Mara nipikie wali ... Umeanza kuiva hiyo harufu siitaki...

Oga basi siogi .. KWA wiki mara moja au inakata kabisa...

Hiyo perfume siitaki ...

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Hapo kwenye kuoga huwa inakuwaje mkuu kama ushawahi kukukuta ya design hiyo

[emoji1787]
 
Siku kataka chips yai nikaleta akadai zinanukia vibaya hataki anataka tu viazi kwaiyo nikalete viazi vya kukaanga na miguu ya kuku full pilipili alafu chips zenge ndio nile mwenyewe yeye hawezi kupika usiku [emoji17][emoji17][emoji17]

Nikasema zege mm nikila sitosshiba nikachukua unga nikabandika ugali akadai mboga nitapata wapi apo nimeshafura asira nikamwambia ntajua mwenyewe pa kupata nikasoga ugali umeiva nimenuna akanionea uruma akanipa buku 2 nikanunue paja la kuku nije kurumangia ugali akasisitiza paja la kuku sio kitu kingine mana ni kama nitakuwa nimechokoza ugomvi hataki harufu nyingine.

Nimeenda chukua paja saa tano iyo sasa nakula ananiangalia nimekula nimemaliza nikasema sasa niende kunawa nije kutoa vyombo ile narudi namkuta anakula mifupa niloiacha kaimix na pilipili [emoji16][emoji16] ase nilichoka.

[emoji1787][emoji1787][emoji1787]kudadadek
 
Sababu kubwa ni mabadiliko ya hormones na ugeni wa kuwa mjamzito...

Hata hivyo usimuendekeze sana inabidi ajitahidi kufanya shughuli za hapa na pale la sivyo mimba inaweza ikamsumbua...
 
Hivi wadau ni sawa kwa mwanamke mwenye mimba ya mwezi mmoja kuanza uvivu na kuumwa umwa!!

Naona mwanamke wangu ananiletea vipengele sana yaani tangu tujue ana mimba basi kazi zote za ndani ndio hawezi tena….hapiki hafui hadeki…vitu vyote hivyo nafanya mimi. Mara ajitapishe mara aseme anasikia kizunguzungu mara agome kula.

Yaani ni kama wiki mbili sasa lakini nimeshanyooka. Game nanyimwa kwa kisingizio kuwa anajisikia vibaya

Ni kweli inakuwa ivi sometimes au ndio nanyooshwa!!?
Ndio madhara ya mimba ya mara ya kwanza.
Kuna siku usiku wa manane saa nane hivi atakuambia anataka mirinda nyeusi au zabibu zilizoganda
 
Back
Top Bottom