Mke wangu ana uvimbe kwenye ovari (ovarian complex cyst)

Mke wangu ana uvimbe kwenye ovari (ovarian complex cyst)

Mkuu nenda hospitali acha hz mambo za mitishamba,nakwambia hv kwa sababu kuna dada namjua alishauriwa aende kwa ajili ya kuondoa uvimbe akahamia kwenye mitishamba,kurudi hospitali wakamwambia chance ya kumsaidia tena haipo sababu mirija ilishaziba completely-Ni huzuni asikwambie mtu.Ikibd fika kairui tafuta ma super specialist pale
Sawa kiongozi.

Je kwa kanda ya ziwa ni hospitali ipi nzuri?
 
Hospitali nzuri za haya mambo ya uzazi ni Kairuki Hospital, Jitahd sana uende mapema otherwise kadri unavyochelewa ndo tatizo linazid kuwa kubwa na pengine kupelekea kutopata mtoto kabisa.Jitahd uwezavyo ufanye mapema sana
Je lake zone ni wapi wapo vizuri?
 
Wataalam habari za asubuhi?

Naomba msaada wa elimu katika hili.

Baada ya kuishi na mke kwa muda kwa mwaka mmoja na miezi saba bila kupata hata dalili yoyote ya mimba, nikaamua kwenda hospital moja yenye huduma bora na za uhakika ili kupata majibu ya uhakika juu ya tatizo linalosumbua.

Vipimo vyangu vilionesha hakuna shida yoyote, lakini kwa upande wa wife tukaambiwa ana Rt. Ovarian Complex Cyst, Hemorrhagic Cyst (55.4×49.2mm).

Tukaambiwa tiba yake ni oparesheni kubwa kuondoa uvimbe huo. Tulibaha hadi kushindwa kuuliza maswali ya msingi tukaaga kwamba tukajipange kwanza tutarudi kwa operation hiyo.

Hapa nilipo kichwa hakipo sawa kabisa.

Je, operation ya namna hiyo huwa kizazi kinabaki au kinaondoshwa kabisa?

Hata kizazi kikibaki kwa hali hiyo anaweza kupata mimba/kuzaa?

Tatizo hilo haliwezi kujirudia tena?

Side effects za operation ya namna hiyo ni zipi?

Hakuna tiba mbadala?

Naombeni elimu mujarabu.
TIBA IPO Mkuu.PACHA WANGU ALIPONEA HII NA ALIKUWA NA 67.9 mm.
FANYA HIVI CHEMSHA MCHAICHAI NA MAJANI YA MDALASINI KUNYWA KIKOMBE KIMOJA ASUBUHI KABLA HUJALA KITU NA KIKOMBE KIMOJA JIONI SAA 1 KABLA HUJALA MLO WA JIONI TUMIA KWA SIKU 14 KISHA KAPIME ULTRASOUND KATKA HOSPITALI 2 TOFAUTI UJUE MAENDELEO YA HIYO KITU
 
TIBA IPO CHEMSHA MCHAICHAI NA MAJANI YA MDALASINI KUNYWA KIKOMBE KIMOJA ASUBUHI KABLA HUJALA KITU NA KIKOMBE KIMOJA JIONI SAA 1 KABLA HUJALA MLO WA JIONI TUMIA JWA SIKU 14 KISHA KAPIME ULTRASOUND KATKA HOSOITALI 2 TOFAUTI UJUE MAENDELEO YA HIYO KITU


Majani ya mdalasini yanapatikana wapi?

Je magome ya mdalasini hayafai?

Mdalasini unapatikana kwa urahisi kwa njia ya magome au unga wa magome.
 
Kuna Dk mmoja anaitwa Dk Mashavu: ana hospitali yake Mwalusembe (Wilaya ya Mukuranga) na ana'attend' pia hospitali ya Sabrina iko Mbagala karibu na Shule ya Sekondari ya St Anthony (upande wa pili wa barabara), Kings Hospital, Kariakoo, na hospitali nyingine iko Ilala kabla ya Soko la Karume kama unatokea Buguruni (upande wako wa kulia) na baada ya Bungoni - iko chini ya ama Shirika la Dini ya Kiislamu au owner ni Muislamu.

Huyu Dk, kwa maoni yangu, ni mzuri sana kwa upande wa magonjwa ya wanawake na anamsikiliza mgonjwa vizuri sana (hana complications).
Huyu Dr.Mashavu namjua amewahi kumhudumia sister angu.ni kweli ni Dr.Mzuri sana sana
 
Majani ya mdalasini yanapatikana wapi?

Je magome ya mdalasini hayafai?

Mdalasini unapatikana kwa urahisi kwa njia ya magome au unga wa magome.
Mkuu majani ya mdalasini Ni greenish, mchachai kadhalika yanakuwa na ufanisi .Mimi niliyapata kea kuagiza Moshikwa magome mkuu Sina hakika japo nayo hutumika kutibu masundosundo
 
TIBA IPO Mkuu.PACHA WANGU ALIPONEA HII NA ALIKUWA NA 67.9 mm.
FANYA HIVI CHEMSHA MCHAICHAI NA MAJANI YA MDALASINI KUNYWA KIKOMBE KIMOJA ASUBUHI KABLA HUJALA KITU NA KIKOMBE KIMOJA JIONI SAA 1 KABLA HUJALA MLO WA JIONI TUMIA KWA SIKU 14 KISHA KAPIME ULTRASOUND KATKA HOSPITALI 2 TOFAUTI UJUE MAENDELEO YA HIYO KITU
Asante mkuu.

Kwa kanda ya ziwa majani ya mdalasini yanaweza kupatikana?
 
Majani ya mdalasini yanapatikana wapi?

Je magome ya mdalasini hayafai?

Mdalasini unapatikana kwa urahisi kwa njia ya magome au unga wa magome.
Mkuu Ni majani Pacha alipona kwa njia ya kuchemsha mchaichai na majani ya mdalasini na wengi waluokuwa na tatizo hilo wametumia na kuondokana nalo.
ACHA shortcut mkuu
 
Hospitali nzuri za haya mambo ya uzazi ni Kairuki Hospital, Jitahd sana uende mapema otherwise kadri unavyochelewa ndo tatizo linazid kuwa kubwa na pengine kupelekea kutopata mtoto kabisa.Jitahd uwezavyo ufanye mapema sana
Hivi gharama za tiba kama hizi mtu anatakiwa kujipanga kwa pesa kiasi gani hapo kairuki
 
Boss, pole sana, hiyo ishu iliwapata ndugu zangu kadhaa wa karibu sana, kuna mtu alinisaidia ikapona kwao kabisa na leo hii nina wajomba, tiba yake ni ya kienyeji lakini inahusisha dawa za mizizi nitakutumia, kwa miezi kadhaa anakuwa sawa kabisa, nipe namba yako nikupigie nikuelezee. Pole sana, ninajua unachopitia. Msifanye kwanza upasuaji.
Twashukuru sana
 
Natamani kujua ulienda hospitali gani, mimi kama muhanga wa ovarian cyst na nilishafanyiwa operation kwajili ya hizo ilipelelekea nikatolea yai moja likabaki moja, ila kusema ukweli huwa zinarudi hasa hizo ambazo ni complex
 
Kuna dawa za mitishamba zinaondoa vizuri bila upasuaji.

Sema kuipata inahitajika neema ya Mungu!
 
Back
Top Bottom