Nyanda Banka
JF-Expert Member
- Mar 14, 2023
- 304
- 1,054
Kama mjuavyo sisi wanaume mara nyingi ni kuamka asubuhi na mapema na kuondoka, na kurudi ni usiku, muda ambao Mimi nashinda nyumbani ni Jumamosi na Jumapili.
Usiku wa kuamkia Jana alhamis mtoto wa marehemu dada yangu alianza kulia sana chumbani, akalia sana mpaka ikabidi niamke niende chumbani kwao Ili nione Kuna nini, nilivyo fika nilimkuta kakaa chini huku wenzie wamelala, nikamwuliza Kuna nini? Akanijibu mguu unamuuma sana, ikabidi niuangalie mguu, aisee nilijikuta nalia na Mimi, mguu ulikuwa umevimba sana, nikamwuliza ilikuwaje? Akaniambia mke wangu alimpiga na kipande Cha tofali.
Pale pale nikaenda kumwamusha mke wangu kumwuliza hiki alicho fanya, akawa amekataa na kuanza kumfokea mtoto eti anataka kutugombanisha, Nikasema sawa, ila kwanini mguu unafikia hatua hii ina maana alikuwa hamuoni? Akawa amezidisha hasira eti natafuta sababu kama nime mchoka niseme arudi kwao, nikaona maneno yasiwe mengi ikabidi nimpakie mtoto kwenye gari nikampeleka hospital usiku ule ule, iligundulika kuwa mfupa wa mbele wa mguu uliachia kidogo akafungwa P.O.P.
Nilivyo rudi nyumbani asubuhi Jana hiyo asubuhi ilibidi nishinde nyumbani, ikabidi nifanye upelelezi mana Kuna vitu niliiona haviko sawa, ndo mpangaji wangu mmoja akaniambia kama Kuna sehemu naweza kumpeleka huyu mtoto Bora nimpeleke vinginevyo itatokea hatari kubwa, mtoto anateswa mno na mara nyingi shuleni haendi, na siku alivyo mpiga na tofari alikuwa amemtuma vitafunwa asubuhi akachelewa kurudi, tofari alimpiga mbele ya wapangaji siku tatu nyuma, na siku zote hizo hakwenda shule.
Nawaza mtoto nimpeleke wapi, marehemu dada yangu baada ya kufariki 2022 tuligawana watoto sisi ndugu zake, hili tukio limefanya nimkumbuke marehemu dada yangu aliye fariki Kwa maumivu makubwa ya kansa akiwa mikononi mwangu, nawaza Bora kuachana na mke wangu kuliko kuacha mtoto wa dada ateseke ntakuwa nimemkosea dada.
Mke wangu alimchukua mtoto wa kaka yake anaishi hapa na anaelekea kumaliza form 4 Kwa Gharama zangu, ila mtoto wa upande wangu kashindwa kumlea Kwa miaka miwili tu,hii ni sawa kweli?
Halafu baada ya mtoto kuniambia kuwa yeye ndo alimpiga, muda wote saivi ni kumuangalia Kwa jicho Kali sana na kumwambia eti ametumwa aje kutugombanisha, mtoto wa miaka 8 anawezaje kutugombanisha?
Sikuwahi kumfikiria mke wangu kuwa anaweza fanya hiki alicho fanya kutokana na mambo ninayo wafanyia ndugu zake, na ndiyo maana huyu mtoto nilimleta hapa Kwa kuamini atamsimamia kama mwanae na kama anavyo wasimamia watoto wetu wawili.
Mpaka naogopa kwenda kazini na huyu mtoto kumuacha hapa, nahisi atampiga Yani