Mke wangu anamtesa sana mtoto wa marehemu dada yangu

Mtoto wa miaka minane hafai kukaa boarding.

Amandla...
 
Roho mbaya haiwezi badirika kwa kukaa kuiongelea hapo atakuwa aamempatia nafasi ya kubadiri mbinu za kumtesa huyo mtoto. Dawa hapo ni kumtengenisha huyo mtoto na mke wake kwa kumfukuza mke wake au kumtaftia makazi mapya mtoto
 
Je, Una uhakika kwamba hiki ulichoandika hapa kina ukweli au ni hadithi ya kutunga ili kufurahisha genge??
Kwamba unataka kusema visa kama hivi havitokei kwenye jamii yetu au?

Kama una bisha niambie uko wapi nikuonesha mwanamke aliyempiga na flypan mtoto wa dada wa mume wake mpaka sikio likakatika.
 
Nilitegemea hadi muda huu huyo mke wako angekuwa na kesi mahakamani.

Mliwezaje kupata matibabu bila PF3 au na wewe ulidanganya hospital?

Mchukulie hatua za kisheria huyo ni mhalifu. Ungekuwa wewe umefanya hivyo asingekuacha uraiani.
 
Tatizo nyie bluepilled men huwa mnaamini eti wake zenu huwa wanawapenda sana ndugu zenu kama vile ambavyo wewe unawapenda na kuwajali sana.ndugu zake.

Msichokijua ni kwamba hakuna binadamu ambao mwanamke huwa anawachukia kama ndugu wa mume wake na tena muda mwingi anakuwaga hana hata sababu ya msingi za kuwachukia ila kutokana na zile negative stori anazoskia kutoka kwa mashoga zake kuhusu mawifi na wakwe kwa ujumla ndio kunamtengenezea strong aggression dhidi ya ndugu wa mume na hivyo upelekea yeye kuishi kwa kujihami na kuwachukia ndugu wote wa mume mpaka watoto wadogo.

Kwa kesi yako wewe mleta mada kwa hapo ulipofikia sululisho pekee ni kuachana kabisa na huyo mke wako, maana mpaka hapo tayari ameshatengeneza uadui na ukoo wako kwa kumtesa huyo mtoto mdogo..... sasa unaendeleaje kuishi na mwanamke ambaye hata yeye mwenyewe anajua kwamba ni adui wa ukoo wako?
 
upuuzi huu, kuna nati haziko sawa
 
Nilitegemea hadi muda huu huyo mke wako angekuwa na kesi mahakamani.

Mliwezaje kupata matibabu bila PF3 au na wewe ulidanganya hospital?

Mchukulie hatua za kisheria huyo ni mhalifu. Ungekuwa wewe umefanya hivyo asingekuacha uraiani.
Kabisa huyo ni anastahili kufunguliwa kesi kama child abuser

Tena hii itakuwa ndio njia rahisi ya kuachana nae, maana huyo mwanamke akitoka hapa atakuwa na hasira sana na yeye kitu kitakachopelekea kutoendelea na hiyo ndoa.
 
Ushauri mzuri sana
 
wewe ni msukuma na mkeo mweupe?
acha kua mjinga. hakuna mke hapo unakaa na lijambazi. na lijambazi sharti kuliua.
Kwanini kila jambo la kipuuzi lazima mlihusishe na msukuma?

Kwani hao wanaume kutoka jamii zingine hawawezi kuwa wajinga na dhaifu kwa wanawake hivi?

Na una uhakika ni wanaume wa kisukuma pekee tu ndio wanawapenda hao wanawake weupe??
 
Huyo mke wako ndio kiongozi wa familia? Mpaka Sasa hujachukua hatua unamwogopa? Kama huwezi kumsimamia huyo mtoto, nani atafanya? Angewnda kwako tu, huyo ni kiuaji. Hilo tofali subiri la kwako na wewe ukichokwa utandikwe tofali ukalale mbele
 
hilo limwanamke ningeligonga si mchezo kama nkusepa lisepe baadhi ya wanawake wana roho mbaya mno..

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…