Mke wangu anamtesa sana mtoto wa marehemu dada yangu


Huwa sina muda wa kubembeleza upuuzi km ulivyosema hapo juu.
ARUDI KWAO KWA MUDA
 
Ita ndugu upande wa mwanamke, wambie ukweli wa tukio, wape msimamo wako na mpe mke msimamo wako mbele Yako, then mpe muda, akiendelea achana naye haraka uwezavyo , huyo ni shetani , na unawezaje kuishi na mama wa nyumbani haleti pesa eti majukumu kupika chai, na kuosha uchi wake , so
 


"Baadhi ya wanawake wanaroho mbayaa sana hapa kitaa hapa kuna jamaaa aliachana na mkewe akachukua single maza moja hivi mshikaji nae ana mtoto mmoja na huyu mtoto ndo mama yake na huyu mwamba walipambana wakajenga mji.Single maza kaja na mwanae lakini cha ajabu alikua anamtesa mtoto wa mwanaume ile mbaya ila mwanae anaishi nae poa tu."👆👆
Umeenda madarasa haya haya ya Tanzania au ni nje ya nchi?
 
Sheria ya ndoa iweke muda wa matazamio, hiki kiumbe ni hatari sana
Haina haja ya kusubiri Sheria na tamaduni za kizungu ziendeshe maisha Yako,mke mmoja sijui ndoa za kanisani huo ni utamaduni wa wazumgu,wewe fukuza ukiona mambo hayaendi sawa na leta chombo mpya uendelea kuupa amani moyo wako
 
Hkas
Halafu tukisema wanawake ni waovu kuliko shetani tukaonekana wanyanyasaji, sasa piga makofi huyo mwanamke au mpeleke polisi akafungwe, hatutaki upumbavu hapa.
 
Tulio lelewa na mama wa kambo tuna experience ya hvyo vitimbi.....

Hakuna rangi tuliacha kuona ila mwisho wa siku.....Mungu huwa upande wetu,huyo mama atajuta dogo akiwa mkubwa
 
Pole sana. Huyo mkeo ana upungufu wa akili. Na sababu ya kusema kama humtaki anajua mtagawana mali. Na ukikaa vibaya atakuua. Na atakuwa na wanaume wengine wanaompa kiburi. Weka vizuri mali zako then piga chini uachane naye. Huyo hakufai. Tafuta mke mwingine.
 
pole sana mimi ushauri wangu naomba huyo mtoto mpeleke boarding school maana hapo nyumbani huyo mke wako anamnyanyasa sana yaani mpaka nimelia 😭😭😭😭😭
 
Kama mwanamke hawezi kukaa na ndugu zako kwa Amani Huyo sio mke ullingia Choo cha kike, Mimi mwaka flan nilimfanyia mdogo wangu sherehe aliingia kumi Bora kitaifa kidato cha sita.

Mchumba wangu akanijia juu natumia hela vibaya , kwa kosa hilo nilimfuta kabisa na kuahirisha mipango yote. Kwangu Mimi Bora kosa lolote ila sio kushindwa kujali ndugu zangu
 
Mkuu samahani naomba unijibu kitu, mkeo kwao ni masikini au hali duni fulani hivi sio?
 
Umeoa mtu mkatili sana mpeleke mtoto boarding tu
 
Yeye mtoto wake wa kumzaa angeweza kumpiga tofari mbele za watu kisa kachelewesha kitafunwa halafu amuache na maumivu ndani ya siku tatu.

Mkuu nimeona wanawake wengi tu wana roho mbaya sana kwa damu zisizo zao au hawana undugu nazo. Ila huyo mwanamke ni shetani
 
Hatari sana kisaikolojia kwa mtoto, solution ya haraka mhamishe hapo to boarding school au trusted relatives, usilazimishe akae hapo kama mkeo hataki maana ni kwake pia
 
Huna mke hapo unajambazi mana huyo anaroho ya kishetani..kama anaweza kumpiga mtoto tofali wewe atakuchoma kisu au kukufanyia unyana wowote.hapo unaishi na jambazi sugu
 
Pole sana kwa hayo lakini rafiki nikueleze ukweli kuwa unayo roho nzuri na hakika nawiwa kusema Mungu akubariki kwa hiko unachofanya Ila bila kukuficha ni kuwa hayupo na akiwepo ni wachache wenye uwezo wa kuishi na ndugu baki au mtoto wa ndugu akamtreat vizuri hivyo nasisitiza huku nalia ya kuwa pambana mpaka umpe bright future huyo mtoto kwa gharama yoyote ,sikushauri umfukuze mkeo maana hata kwa kufanya hivyo Kuna mgogoro wa nafsi utawatengenezea wanao wa kuzaa .

Angalia kila unaloweza huyo mtoto wako ubaki naye hata kwa gharama zozote .

Pole sana ,imeniuma japo imebidi nichangie tu kwakuwa mke wangu Nyamwi255 Yuko hapa na amechangia mchango positive na Mimi nimejua Yuko vizuri kwa kulea
 
Kama sio story ya kutunga,basi mimi ningekuwa niko singo tangu mpangaji alivyonisimulia. Maana mwanamke wa hivyo anaasili ya roho mbaya hawezi kukuacha salama hata wewe mwenyewe hata kama ni baada ya miaka 24 ya ndoa ,subiri tukio lingine la kukata na shoka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…