Mke wangu ananilazimisha nimuombe msamaha mbele ya Kanisa

Hicho ndicho kizazi cha nyoka tulichonacho karne hii,pole sana baharia shikilia hapo hapo
 
Hivi, unamkoseaje mkeo?
Yaani Ni kosa gani unalifanya linaonesha umemkosea mkeo?
Labda kama umeruka na mama yake mkuu!!
Vinginevyo hakuna kitu naweza fanya mke akanambia nimemkosea!!
 
Hii inafanana na kesi ya wapendanao wawili wanataka kufunga ndoa. Mmoja kamwambia mwenzake wakapime VVU. Kufika kwa Dr. Wanataka wapewe cheti /maandishi kuwa wako salama.
Dr. kawatizama kisha akauliza swali. Mnataka mumpe nani majibu ya vipimo? Waliondoka hata bila ya kusema chochote.

Sasa hii misamaha mingine, kama umeua vile au anakisasi nawe. Ingekuwa umeiba akasema ukarejeshe ulichoiba au mali sawa na ulichoharibu sawa. Lakini kuna kitu anataka usifanikiwe.
 
Mkuu hapo ndio ujue maisha sio lelemama
Wanawake wakishikilia kitu jipange
Pambana
 
Kama ulitenda dhambi ambayo kanisa lilijua kuwa ulitenda hiyo dhambi, basi inabidi ukatubu kanisani. No muhimu kufanya hivyo kwa ajili ya ushuhuda wako mwenyewe na kulinda heshima yako na familia yako.
 
Hhuyo mwanamke anatafuta mapengo kinguvu
 

Au una maanisha kwamba Membe ndiye amegoma kuomba msamaha mbele ya camera na hayupo tayari kuita baba kama alivyofanya Nnape? Haiwezekani mke wako afanye Copy and Paste kama Magogoni, huyo 'mke' atakuwa ni Mkulu (Numero uno) na wewe utakua umesimama badala ya Membe.
 
Ndo tatizo la kusali kwenye vibanda
 
Kwani dhambi yenyewe ilirekodiwa?
 
Mkuu tumekushauri sana. tupe mrejesho sasa
 
Nadhani tukubaliane kwamba sio kila mtu ana-qualify kuingia kwenye ndoa wengine tunapaswa kuwa wapenzi watazamaji tu otherwise mambo ya ajabu sana yatatokea. Now back to the subject, unapoomba msamaha unaomba kwa faida ya nani?? ninachokiona hapa familia yenu itageuka TV show maana nawewe akikukosea utampa masharti magumu km ya kwake. My friend a human being if free by nature, if you want to do it...do it kama hujiskii then don't, we all make mistakes anyways.
 
Nenda nae kanisani,
Muombe msamaha na yote anayotaka uyafanye,
Hii itafanya upime ujinga wa mkeo,ujinga wa viongozi wa kanisa,
Halafu ukisha Fanya anayotaka tangaza hapo hapo kuachana nae mbele ya hao hao anaotaka waone unavyomuomba msamaha
Yaaaani umelenga mlemle unamwacha palepale Na uombe msamaha kwa kuchelewa kufanya hilo
 
Haya ni madhara ya MAKANISA YA HOVYO NA KIHOLELA. Hakuna KIONGOZI wa kanisa mwenye akili zake timamu akaruhusu huu UPUUZI WA MKEO.

Mathayo 6:14-15
[14]Kwa maana mkiwasamehe watu makosa yao, na Baba yenu wa mbinguni atawasamehe ninyi.
[15]Bali msipowasamehe watu makosa yao, wala Baba yenu hatawasamehe ninyi makosa yenu.
 
Kapige magoti wewe hautokuwa wakwanza au wa mwisho.
Ila hakikisha baada ya vitendo hivyo unakuwa zaidi ya Adolf Hitler kwake
 
Bila shaka kabisa hilo kosa ulifanya kanisani na watu walikuona,hivyo nenda kalitubie huko huko sizani kama mke ni kichaa AKWAMBIE ukatubu mbele ya kanisa, kuna mmoja aliitwa mbele ya kanisa akiwa na mchepuko wakati huo huo na mkewe yupo humo humo Ibadani alichokifanya aliondoka hapo mbele ya kanisa na mchepuko wake wewe mtu kama huyu unamsamehe ukiwa wapi? Wewe nenda katubu mbele ya kanisa
 
Hehehe mimi angenambia hivyo angekula talaka within 24hours.
 
Ningemuongezea kerebu tano kwanza sio kwa masharti ya kijinga kama hayo .

Eti nini! [emoji3].....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…