Mke wangu ananilazimisha nimuombe msamaha mbele ya Kanisa

Mkeo atakuwa 'ameokoka', anataka wapendwa waone jinsi gani 'mlivyookoka' hadi kanisani wajue ya familia yenu.

Hakika amekupanda kichwani
 
Huyu siyo baharia, baharia kama baharia hakai namna hii
 
Ungemuuliza tu swali dogo.
Je umelikosea kanisa au yeye?
Umewakosea waumini au yeye?
Ulipomkosea mlikuwa kanisani?
Fanya jambo moja la kijasiri, mkubalie nenda kanisani ukifika muda wa kwenda kuomba msamaha pokea maiki na useme maneno haya.
Mimi fulani nipo mbele ya kanisa kuwatangazia wachungaji na waumini wenzangu wote kuwa kuanzia leo tarehe fulani bila kulazimishwa na mtu yoyote, mimi na mke wangu tukiwa na akili timamu tumeamua kuachana rasmi na mke wangu na kila mtu afuate maisha yake. Tumeamua kuachania kanisani kwakuwa ndipo tulipofungishwa ndoa, asanteni.
Baada ya hapo ondoka kbs kanisani nenda home katoe vijinguo vyake muwekee sehemu salama, kama kwao karibu vipeleke home kwao.
Najua pande zote kanisa, wazazi wa pande zote hawatakubali, mkikutanishwa meza ya duara ndio ueleze pande zote haya mkeo anayotaka kama ni sahihi. Baada ya hapo atakujua wewe kirambasi hatokuletea tena mapigo ya kingeda.
 


Tafuta tu hela...ukiwa nazo zaidi yake lazima akusamehe
 
Kama uliweza kuonyesha nia ya kumpenda kwa kufunga ndoa kanisani.. unashindwaje kuonyesha unampenda kwa mara nyingine kwa kuungama kanisani??

Trust is the most scarce commodity nowdays, ukishavunja uaminifu kwa mtu kuupata tena lazima ufanye kazi ya ziada.

Acha ujeuri! wewe ni mkosaji, jishushe na umpe mwenzio sababu ya kukuamini tena.
 
Gud idea ikiwezekana aandae kabisa na watu ambao watakua tayari. Yaani pindi amalizapo tu ku omba msamaha wamkabidhi na begi lake kabisa
Nenda nae kanisani,
Muombe msamaha na yote anayotaka uyafanye,
Hii itafanya upime ujinga wa mkeo,ujinga wa viongozi wa kanisa,
Halafu ukisha Fanya anayotaka tangaza hapo hapo kuachana nae mbele ya hao hao anaotaka waone unavyomuomba msamaha
 
Njoo uwe mke wangu uone moto wangu.

Na umbo lako namba nane hilo. Umbo tamu. Walahi utanilaumi kama ukileta upuuzi
Niwe mke wa pili? Daah eti umbo namba nane[emoji3][emoji3] hujaacha tu matusi
 
Heheheeee....Hivi naanzaje kumwambia mume wangu hayo mambo ya kuniomba msamaha mbele ya kanisa? Khaaa...Nikishamsamehe mie inatosha saaana.
Inawezekana kafanya makosa makubwa sana alafu humu watu wanampa kichwa[emoji3][emoji3][emoji3] inawezekana mtaa mzima unajua uovu wake,, mke lazima ampeleke mbele ya kadamnasi ili apate amani ya moyo na amwamini tena.. mbona siku ya harusi walienda humohumo kanisani.

Kwani kumwomba msamaha umpendaye mbele ya watu kunashida gani? Ninachojua kutakua kuna shida kama maombi hayamaanishwi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…