Mke wangu ananilazimisha nimuombe msamaha mbele ya Kanisa

Wakuu nawasalimu,

Niko katika hali hii kwa sasa.

Ni kweli nilimkosea mke wangu. Nilifanya dhambi kama binadamu wengine wafanyavyo dhambi. Nimejutia kosa langu na nikaamua kumuomba msamaha mke wangu ili maisha yaendelee.

Jambo la kushangaza ni kuwa mke wangu huyu wa ujanani amekataa kunisamehe. ametoa mashariti kadhaa ili niweze kupata msamaha wake. Mashariti hayo ni haya.

1. Jumapili hii twende kanisani nikaombe msamaha mbele ya kanisa.

2. Turekodi mkanda wa video ili hata watu wengine ambao hawatakuwepo kanisani waweze kuona tukio hilo hapo badae.

3. Amesema pia nikiwa namuomba msahama mbele ya kanisa nimuite mama na wala siyo mke huku nikiwa nimepiga magoti.

Wakuu, nimefikiri sana swala hili. Nia hasa ya mke wangu ni nini. Hivi ndivyo msamaha unavyoobwa?

Nimejiuliza tena kwani atapungukiwa nini kama atanisamehe tukiwa wawili tu bila kamera?

Nilichopanga ni hiki , nataka kugoma kufanya kitendo hiki. Ninagoma kwa sababu nataka kulinda utu wangu. Kufanya dhambi au kumkosea mke wangu hakuondoi utu wangu hata kidogo.

Siko tayari kuuza utu wangu kwa gharama ya kulinda ndoa. Utu huwekwa na Mungu ndani ya mtu. Kuuza utu wako kwa mtu ni kumfanya mtu huyo kuchukua nafasi ya Mungu katika maisha yako. Siko tayari.

Msamaha una misingi yake. Moja ya misingi hiyo ni kulindiana heshima.Msahama ni upendo .Upendo haudhalilishi wengine.

Kama ndoa ni ndoano , basi ndoano hii haitaninasa.
Muombe Mungu msamaha lakini nawewe usizikumbuke tena dhambi zako ''if you ask God to forgive your sins God forgives for all, but also do not remember your sins any more
 
Ungetaja hiyo dhambi ingekuwa vyema kujua tunashauri vipi. Inawezekana dhambi uliotenda hamna namna lazimi youtube ihusike ili usirudie tena

Duh, huyo mkeo mbabe sana. Kwa hiyo yeye hana dhambi?
 
. Jumapili hii twende kanisani nikaombe msamaha mbele ya kanisa.

2. Turekodi mkanda wa video ili hata watu wengine ambao hawatakuwepo kanisani waweze kuona tukio hilo hapo badae.

3. Amesema pia nikiwa namuomba msahama mbele ya kanisa nimuite mama na wala siyo mke huku nikiwa nimepiga magoti
Kwa masharti haya mimi nakushauri umuombe aende kwao kwanza kwa maana ya kwamba ujiandae
kumtafuta mtu wa kurekodi video siku ya msamaha. Ukifanikiwa kukamilisha utampigia simu mkutane kanisani
siku ya tukio. Akikubali kuondoka we nyamaza utaona sms za kukuomba wewe msamaha zinatiririka.
 
Huu ndo ubaya wa kuoa mwanamke mwenye akili!!we fought for the same hole!!
 
Mimi nisingemuomba msamaha hata kidogo,huyo ashakupanda kichwani.
 
Wakuu nawasalimu,

Niko katika hali hii kwa sasa.

Ni kweli nilimkosea mke wangu. Nilifanya dhambi kama binadamu wengine wafanyavyo dhambi. Nimejutia kosa langu na nikaamua kumuomba msamaha mke wangu ili maisha yaendelee.

Jambo la kushangaza ni kuwa mke wangu huyu wa ujanani amekataa kunisamehe. ametoa mashariti kadhaa ili niweze kupata msamaha wake. Mashariti hayo ni haya.

1. Jumapili hii twende kanisani nikaombe msamaha mbele ya kanisa.

2. Turekodi mkanda wa video ili hata watu wengine ambao hawatakuwepo kanisani waweze kuona tukio hilo hapo badae.

3. Amesema pia nikiwa namuomba msahama mbele ya kanisa nimuite mama na wala siyo mke huku nikiwa nimepiga magoti.

Wakuu, nimefikiri sana swala hili. Nia hasa ya mke wangu ni nini. Hivi ndivyo msamaha unavyoobwa?

Nimejiuliza tena kwani atapungukiwa nini kama atanisamehe tukiwa wawili tu bila kamera?

Nilichopanga ni hiki , nataka kugoma kufanya kitendo hiki. Ninagoma kwa sababu nataka kulinda utu wangu. Kufanya dhambi au kumkosea mke wangu hakuondoi utu wangu hata kidogo.

Siko tayari kuuza utu wangu kwa gharama ya kulinda ndoa. Utu huwekwa na Mungu ndani ya mtu. Kuuza utu wako kwa mtu ni kumfanya mtu huyo kuchukua nafasi ya Mungu katika maisha yako. Siko tayari.

Msamaha una misingi yake. Moja ya misingi hiyo ni kulindiana heshima.Msahama ni upendo .Upendo haudhalilishi wengine.

Kama ndoa ni ndoano , basi ndoano hii haitaninasa.

Huwezi kumwamnbia mkeo MSHAMBA halafu ukategemea msamaha kirahisi hivyo. Hili ndo tatizo la kuoa wanawake wenye akili finyu, visasi na kukurupuka. Nimejaribu kusoma katikati ya mistari yako Mkuu
 
hahaha mpaka hapa hakuna mke wala kanisa....hizi ni codes.....kuhusu msamaha wa juzi...
 
Majibu unayo alafu bado unasema upo njia panda !!!

Kaka zetu mnatufundisha nini yani uende kanisani ukaombe msamaha huyo mwanamke anatoa wapi jeuri na kibri cha kukupa condition hizo..

Amekuzidi umri japo unasema wa ujanani
Amekuzidi kipato japo unasema wa ujanani
Amekuzidi nini haswa ??
Je wewe ni mlemavu mke wako anakuhudumia ??
Una matatizo ya kiafya ??

Umuite mama yeye ndio alikunyonyesha ??mke wako ni mkristo mwambie biblia gani inasema tuwaite wake zetu Mama..
Wakuu nawasalimu,

Niko katika hali hii kwa sasa.

Ni kweli nilimkosea mke wangu. Nilifanya dhambi kama binadamu wengine wafanyavyo dhambi. Nimejutia kosa langu na nikaamua kumuomba msamaha mke wangu ili maisha yaendelee.

Jambo la kushangaza ni kuwa mke wangu huyu wa ujanani amekataa kunisamehe. ametoa mashariti kadhaa ili niweze kupata msamaha wake. Mashariti hayo ni haya.

1. Jumapili hii twende kanisani nikaombe msamaha mbele ya kanisa.

2. Turekodi mkanda wa video ili hata watu wengine ambao hawatakuwepo kanisani waweze kuona tukio hilo hapo badae.

3. Amesema pia nikiwa namuomba msahama mbele ya kanisa nimuite mama na wala siyo mke huku nikiwa nimepiga magoti.

Wakuu, nimefikiri sana swala hili. Nia hasa ya mke wangu ni nini. Hivi ndivyo msamaha unavyoobwa?

Nimejiuliza tena kwani atapungukiwa nini kama atanisamehe tukiwa wawili tu bila kamera?

Nilichopanga ni hiki , nataka kugoma kufanya kitendo hiki. Ninagoma kwa sababu nataka kulinda utu wangu. Kufanya dhambi au kumkosea mke wangu hakuondoi utu wangu hata kidogo.

Siko tayari kuuza utu wangu kwa gharama ya kulinda ndoa. Utu huwekwa na Mungu ndani ya mtu. Kuuza utu wako kwa mtu ni kumfanya mtu huyo kuchukua nafasi ya Mungu katika maisha yako. Siko tayari.

Msamaha una misingi yake. Moja ya misingi hiyo ni kulindiana heshima.Msahama ni upendo .Upendo haudhalilishi wengine.

Kama ndoa ni ndoano , basi ndoano hii haitaninasa.
Hapo cha kufanya ni kutofanya kama anavyotaka pia hayo masharti inaonyesha kakuchoka kuishi na wewe kwenye ndoa kwa maana nyingine naona dhamira yake nikuachana na wewe INDIRECTLY akijua hayo masharti hutayatekereza ili apate sababu.
 
Duh hata kama kuchepuka ndio akapige magoti mbele kabisa kanisani!?? Mke ana masharti magumu mno aisee! !
Aende tu akaombe kwani wakati anafanya hayo yote hakujua kama anamke? Mke ashikirie hapo hapo goti madhabahuni [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
kama unajitaji huo msamaha fuata tu masharti lazima kuna sababu mpaka akakwambia uende kanisani , yumkini ulitenda kosa hilo mkiwa kanisani au katika mazingira ya kanisani hivyo anataka na yeye ajisafishe,kubali yaishe urejeshe amani uokoe ndoa huko nje kuna mbwa mwitu wakali utakuja mkumbuka mke wa ujana wako na itakuwa too late.
Mwambie , ataenda zoa huko atamkumbuka kweli mke wa ujana wake
 
Ni kosa gani hilo ulilomkosea mpaka uombe kwa kanisa? Nenda kwa mchungaji ukaongee huko [emoji23][emoji23][emoji23] yawezekana ndiyo kawaida yako sasa kaamua kukupa mtihani huo, ukiona mke anakupa shughuli nzito kama hiyo basi kqkuchoka kwa tabia zako.
 
Du hii hatari. Ninachokiona hapo upendo wa mwanamke kwa mwanume umeisha kabisa mtu unayempenda huwezi kumdhalilisha kiasi hicho. Lakini pia haya ni maelezo ya upande mmoja inakuwa ni vigumu kufanya judgement bila kupata taarifa za upande wa pili. Kama ni mwanamke wa kawaida mwenye hekima zake ukiacha wanawake wasiojitambua, swali la msingi kwanini mpaka mefikia hatua hiyo?
Angesema na kosa hapo tungetoa hukumu isiyo pendelea lakini hajasema kosa! Na huenda ni kawaida yake ndiyo maana imefikia hapo sizani kama mke ni kichaa mpaka atoe msamaha wadizaini hiyo, pole yake
 
Ishini na wake zenu kwa akili, mabaharia mnafeli wapi?
 
Back
Top Bottom