Mke wangu ananilazimisha nimuombe msamaha mbele ya Kanisa

Mke wangu ananilazimisha nimuombe msamaha mbele ya Kanisa

Hivi kwanini wanandoa hamtuleteagi inspirational stories manake kila story tunayoisoma hapa JF, sie wengine tunabaki kujisemea "...kumbe sijakosea kujiepusha na hiki kikombe!"

Na wewe mleta mada umezidi! Unaoaje malaika wakati unajua kabisa wewe ni binadamu wa kawaida?! Ningekuwa mimi huyo, ningemwambia sawa mke wangu!!!

Potelea mbali hata kama kanisa haliruhusu talaka, ningeandika tu!

Nikifika church, muda wa tukio naitoa bahasha yangu yenye talaka ndani nampa Baba Paroko na kumuomba ausome kwanza "waraka wangu wa ushauri kwa Waumini wengine".
 
Umeshamuomba msamaha Kama anataka kukusamehe atafanya hivyo. Huko anakotaka kukupeleka ni kukudhalilisha na itapelekea mambo mengi sana ikiwa ni pamoja na wewe kuathirika kisaikolojia na kudharaulika.
Yaani umkosee yeye halafu msamaha ukaombe kwenye umati wa watu!!? Sioni kama ina maana yoyote

Simama kiume bro
 
Ungekuwa ni ndoa ya kiislam hapo hapo unamwambia siwezi kuita mama .ninakuandikia talaka uende .
 
kwa sisi mabaharia tunakataa kata kata kufanya huu upuzi..
muulize kwani yeye jahawahi kukukosea?
 
Anaweza akawa anatoka na muinjilist huyo chunguza
 
Naskia ucchungu wanaume tunazidi kupungua...

Mke wako amepata wapi ujasiri wa kukwambia upuuzi huo aiseee !!!

Hata Mungu hapendi ujinga kama huo kasema tuungame dhambi zetu kimya kimya sio kudhalilishana😁😁😁..

Au ndugu yetu umekwama jogoo hapandi mtungi

Pole baharia, umekwama matopeni😂
 
Kwahiyo ni haki yako kumkosea mke wako siyo??
Kuomba msamaha mkeo ni kuanzisha kesi isiyokwisha maisha yenu yote. Maana hilo kosa litakumbushiwa kila wakati. Walio kwenye ndoa wananielewa
 
Kuomba msamaha mkeo ni kuanzisha kesi isiyokwisha maisha yenu yote. Maana hilo kosa litakumbushiwa kila wakati. Walio kwenye ndoa wananielewa
Kwahiyo usipoomba msamaha ndiyo kosa halikumbushiwi??
 
Wakuu nawasalimu,

Niko katika hali hii kwa sasa.

Ni kweli nilimkosea mke wangu. Nilifanya dhambi kama binadamu wengine wafanyavyo dhambi. Nimejutia kosa langu na nikaamua kumuomba msamaha mke wangu ili maisha yaendelee.

Jambo la kushangaza ni kuwa mke wangu huyu wa ujanani amekataa kunisamehe. ametoa mashariti kadhaa ili niweze kupata msamaha wake. Mashariti hayo ni haya.

1. Jumapili hii twende kanisani nikaombe msamaha mbele ya kanisa.

2. Turekodi mkanda wa video ili hata watu wengine ambao hawatakuwepo kanisani waweze kuona tukio hilo hapo badae.

3. Amesema pia nikiwa namuomba msahama mbele ya kanisa nimuite mama na wala siyo mke huku nikiwa nimepiga magoti.

Wakuu, nimefikiri sana swala hili. Nia hasa ya mke wangu ni nini. Hivi ndivyo msamaha unavyoobwa?

Nimejiuliza tena kwani atapungukiwa nini kama atanisamehe tukiwa wawili tu bila kamera?

Nilichopanga ni hiki , nataka kugoma kufanya kitendo hiki. Ninagoma kwa sababu nataka kulinda utu wangu. Kufanya dhambi au kumkosea mke wangu hakuondoi utu wangu hata kidogo.

Siko tayari kuuza utu wangu kwa gharama ya kulinda ndoa. Utu huwekwa na Mungu ndani ya mtu. Kuuza utu wako kwa mtu ni kumfanya mtu huyo kuchukua nafasi ya Mungu katika maisha yako. Siko tayari.

Msamaha una misingi yake. Moja ya misingi hiyo ni kulindiana heshima.Msahama ni upendo .Upendo haudhalilishi wengine.

Kama ndoa ni ndoano , basi ndoano hii haitaninasa.
Kosa ulilofanya ni kukiri kosa ulilofanya na kuomba msamaha.
Usije ukakiri kosa kwa mwanamke hata Kama kakufumania live kataa katakata na geuza kosa yeye ndio awe mkosaji na msamaha akuombe yeye
 
businessman-apologizing-businesswomanboyfriend-trying-to-convince-girlfriend-man-asking-for-forgivenessgreen-screen_vxcuerq0l__F0000.png
 
Kwa masharti hayo uenda huyo mke wako ndiye aliyekusababisha ukatenda hiyo dhambi japo ujasema ni dhambi gani? Au ulikosea njia ukamu umiza kinyeo chake mama watoto wako maana hayo masharti hayatekelezeki.
 
Wakuu nawasalimu,

Niko katika hali hii kwa sasa.

Ni kweli nilimkosea mke wangu. Nilifanya dhambi kama binadamu wengine wafanyavyo dhambi. Nimejutia kosa langu na nikaamua kumuomba msamaha mke wangu ili maisha yaendelee.

Jambo la kushangaza ni kuwa mke wangu huyu wa ujanani amekataa kunisamehe. ametoa mashariti kadhaa ili niweze kupata msamaha wake. Mashariti hayo ni haya.

1. Jumapili hii twende kanisani nikaombe msamaha mbele ya kanisa.

2. Turekodi mkanda wa video ili hata watu wengine ambao hawatakuwepo kanisani waweze kuona tukio hilo hapo badae.

3. Amesema pia nikiwa namuomba msahama mbele ya kanisa nimuite mama na wala siyo mke huku nikiwa nimepiga magoti.

Wakuu, nimefikiri sana swala hili. Nia hasa ya mke wangu ni nini. Hivi ndivyo msamaha unavyoobwa?

Nimejiuliza tena kwani atapungukiwa nini kama atanisamehe tukiwa wawili tu bila kamera?

Nilichopanga ni hiki , nataka kugoma kufanya kitendo hiki. Ninagoma kwa sababu nataka kulinda utu wangu. Kufanya dhambi au kumkosea mke wangu hakuondoi utu wangu hata kidogo.

Siko tayari kuuza utu wangu kwa gharama ya kulinda ndoa. Utu huwekwa na Mungu ndani ya mtu. Kuuza utu wako kwa mtu ni kumfanya mtu huyo kuchukua nafasi ya Mungu katika maisha yako. Siko tayari.

Msamaha una misingi yake. Moja ya misingi hiyo ni kulindiana heshima.Msahama ni upendo .Upendo haudhalilishi wengine.

Kama ndoa ni ndoano , basi ndoano hii haitaninasa.
Mwambie huyo mkeo akuombe msamaha Kwanza kwa kuthubutu kukupa hayo masharti ya hovyo
 
Back
Top Bottom