Mke wangu ananilazimisha nimuombe msamaha mbele ya Kanisa

Wakuu nawasalimu,

Niko katika hali hii kwa sasa.

Ni kweli nilimkosea mke wangu. Nilifanya dhambi kama binadamu wengine wafanyavyo dhambi. Nimejutia kosa langu na nikaamua kumuomba msamaha mke wangu ili maisha yaendelee.

Jambo la kushangaza ni kuwa mke wangu huyu wa ujanani amekataa kunisamehe. ametoa mashariti kadhaa ili niweze kupata msamaha wake. Mashariti hayo ni haya.

1. Jumapili hii twende kanisani nikaombe msamaha mbele ya kanisa.

2. Turekodi mkanda wa video ili hata watu wengine ambao hawatakuwepo kanisani waweze kuona tukio hilo hapo badae.

3. Amesema pia nikiwa namuomba msahama mbele ya kanisa nimuite mama na wala siyo mke huku nikiwa nimepiga magoti.

Wakuu, nimefikiri sana swala hili. Nia hasa ya mke wangu ni nini. Hivi ndivyo msamaha unavyoobwa?

Nimejiuliza tena kwani atapungukiwa nini kama atanisamehe tukiwa wawili tu bila kamera?

Nilichopanga ni hiki , nataka kugoma kufanya kitendo hiki. Ninagoma kwa sababu nataka kulinda utu wangu. Kufanya dhambi au kumkosea mke wangu hakuondoi utu wangu hata kidogo.

Siko tayari kuuza utu wangu kwa gharama ya kulinda ndoa. Utu huwekwa na Mungu ndani ya mtu. Kuuza utu wako kwa mtu ni kumfanya mtu huyo kuchukua nafasi ya Mungu katika maisha yako. Siko tayari.

Msamaha una misingi yake. Moja ya misingi hiyo ni kulindiana heshima.Msahama ni upendo .Upendo haudhalilishi wengine.

Kama ndoa ni ndoano , basi ndoano hii haitaninasa.
kosa lilianzia hapo kuomba msamaha
 
Mwanaume haombi msamaha. Mwanaume akigundua amekosea katika matendo yake utaona tu amejirekebisha
 
Majibu unayo alafu bado unasema upo njia panda !!!

Kaka zetu mnatufundisha nini yani uende kanisani ukaombe msamaha huyo mwanamke anatoa wapi jeuri na kibri cha kukupa condition hizo..

Amekuzidi umri japo unasema wa ujanani
Amekuzidi kipato japo unasema wa ujanani
Amekuzidi nini haswa ??
Je wewe ni mlemavu mke wako anakuhudumia ??
Una matatizo ya kiafya ??

Umuite mama yeye ndio alikunyonyesha ??mke wako ni mkristo mwambie biblia gani inasema tuwaite wake zetu Mama..
Pengine labda anataka kumpiga tukio baya Sana akirudia kosa la dhambi yake ishi kimachale machale na huyu mke wako wewe ndo unamjua mkeo akili zake zipoje all in all kanisani usiende
 
Mkeo
Wakuu nawasalimu,

Niko katika hali hii kwa sasa.

Ni kweli nilimkosea mke wangu. Nilifanya dhambi kama binadamu wengine wafanyavyo dhambi. Nimejutia kosa langu na nikaamua kumuomba msamaha mke wangu ili maisha yaendelee.

Jambo la kushangaza ni kuwa mke wangu huyu wa ujanani amekataa kunisamehe. ametoa mashariti kadhaa ili niweze kupata msamaha wake. Mashariti hayo ni haya.

1. Jumapili hii twende kanisani nikaombe msamaha mbele ya kanisa.

2. Turekodi mkanda wa video ili hata watu wengine ambao hawatakuwepo kanisani waweze kuona tukio hilo hapo badae.

3. Amesema pia nikiwa namuomba msahama mbele ya kanisa nimuite mama na wala siyo mke huku nikiwa nimepiga magoti.

Wakuu, nimefikiri sana swala hili. Nia hasa ya mke wangu ni nini. Hivi ndivyo msamaha unavyoobwa?

Nimejiuliza tena kwani atapungukiwa nini kama atanisamehe tukiwa wawili tu bila kamera?

Nilichopanga ni hiki , nataka kugoma kufanya kitendo hiki. Ninagoma kwa sababu nataka kulinda utu wangu. Kufanya dhambi au kumkosea mke wangu hakuondoi utu wangu hata kidogo.

Siko tayari kuuza utu wangu kwa gharama ya kulinda ndoa. Utu huwekwa na Mungu ndani ya mtu. Kuuza utu wako kwa mtu ni kumfanya mtu huyo kuchukua nafasi ya Mungu katika maisha yako. Siko tayari.

Msamaha una misingi yake. Moja ya misingi hiyo ni kulindiana heshima.Msahama ni upendo .Upendo haudhalilishi wengine.

Kama ndoa ni ndoano , basi ndoano hii haitaninasa.
anatakiwa akuombe msamaha hapo kanisani kwa kukuambia huu ujinga,na arekodiwe kwa kumbukumbu ya baadae
 
Anaamini kwa kufanya hivyo ndio hutarudia kuchepuka tena ? 😆😆😆

Halafu itakuwa ni ndoa changa ukute kama sijakosea.

Be a man bana!

Mpaka hapo ameonesha amekutawala. Kubadili asili ya kanuni mtapata tabu sana.
Mwanaume ukipoteza nafasi na sauti yako kwenye ndoa baaasi !
 
Kwan umelikosea kanisa, mwambie atulie km hataki kukusamehe.
 
Back
Top Bottom