Mwanangu rapcha umeimba hili goma leo ndo nimejua kuwa wanawake ni watu wa ajabu mno can you imagine leo ni siku ya 11 wife ananinyima tendo la ndoa bila sababu ya msingi.
Sasa leo nimeamua kuchachamaa bado wife amekaza. Daaah, kiukweli roho imeniuma sana let me summarize:
Mimi: Mama, naomba haki yangu basi
Wife: Kwanza tengua kauli yako ya juzi uliyosema
Mimi: Kimya kinanitawala mawazo yanachukua nafasi kichwani mwangu palepale hisia za mahaba zinanitoka na kuona sasa huyu mwanamke kuna kitu kinamtia kiburi kwa hasira naamua kuropoka oya mama mtu mimi naona nikamwambie babaako hili unalonifanyia tuone mzee wako atachukua uamuzi gani
Wife: Anacheka kwa dharau halafu kanasema “wewe mara ya mwisho si ulisema utatoka nje ya ndoa? Sasa babaangu ukamwambie wa nini?”
Mimi: Hasira zinanijaa namwambia oya mimi nimekuchoka mwanangu, kama vipi tuachane tu kwasababu haiwezekani nakuomba haki yangu halafu wewe unachukulia poa tu
Wife: Ananiangalia usoni kama sekunde 30 halafu anasema bila ya maandishi toa karatasi (talaka) niende nayo nyumbani (tena kwa kujiamani kabisa)
Mimi: Moyoni gadhabu Inanijia kitanda chote cha moto naamua Bora nishuke nikalale kwenye kochi maana kuendelea kulala naye kitanda kimoja naona itakuwa ni hatari kwa afya yake maana naweza nikampa kipondo heavy alafu kesho anipe shida kwenye matibabu
Waungwana mpaka hapo nyie mnaonaje huyu shemeji yenu, kuna usalama kwenye hii ndoa yenye mwaka mmoja na miezi 10??