Tears of the Sun
Member
- Jun 2, 2022
- 96
- 294
Tatizo kubwa lilianza pale nilipogundua anachepuka na ex wake. Baada ya kuligundua hilo sikutaka kuchukua hatua za shari sana papo kwa papo, bali nilichukua hatua ambazo mpaka leo anashindwa kuelewa afanyeje, sasa imefikia hatua muda wote ni analia tu, saikolojia hayupo sawa na kama anataka kuchanganyikiwa hivi.
Baada ya kugundua kwamba anachepuka nilichukua maamuzi yafuatayo
1. Siku hiyo hiyo niliyogundua sikutaka kumuuliza kama ni kweli au siyo kweli kwa sababu nilishajihakikishia kwa asilimia 100.
2. Sikula Chakula chake, nilifika naingia jikoni na kuandaa Chakula mwenyewe (hii imeendelea hadi leo)
3. Najitahidi sana niwahi kurudi nyumbani tofauti na siku za nyuma.
4. Tukilala kitandani mimi nageukia mzungu wa nne.
5. Tangia siku hiyo sijawahi kumuomba unyumba(japo anaweka mazingira ya jambo hili kila siku)
6. Akiniuliza namjibu kidogo halafu naendelea na utaratibu wangu.
7. Kila kitu najifanyia hadi nguo chafu zote za kwangu nakusanya na kufua mwenyewe nikipata nafasi(Ninapokuta amezifua narudia kufua)
8. Simtukani wala kumuongelesha vibaya bali nafanya mambo yangu ndani ya nyumba kivyangu.
9. Baada ya kuona hivyo, akasema anataka akaonane na Mama yake(ilikuwa Ijumaa usiku, nikampatia nauli muda huo huo na kumwambia asubuhi na mapema aende, ghafla akasema ameahirisha hadi sasa yupo)
10. Nimeacha kuchangia naye kitu chochote ndani ya nyumba isipokuwa sehemu ya kulala tu(kitandani na penyewe mzungu wa nne au nalala sebuleni wakati mwingine).
Sasa leo ni siku ya 6 tangia nimeanza kuishi hivyo na mke, mke wangu amenyongonyea ghafla, amekonda, amekuwa mtu wa mawazo na wasiwasi muda wote.
Katika kipindi hiki chote alijua sababu ya mimi kuishi hivyo ni yeye kuchepuka, hii ni baada ya jana jioni kuniita Chumbani na kusema anajutia sana kufanya vile na hatarudia, jambo baya zaidi akasema ameshafikiria mara mbili kunywa Sumu, anaona hana thamani tena kwangu, Dah [emoji24][emoji24] nilimwonea huruma sana na nikaamua kumsamehe tuendelee na maisha lakini naona hali haijabadilika kwake yaani ni mtu wa mawazo na wasiwasi muda wote, kiufupi anapitia wakati mgumu sana.
Wito kwa wanaume na wanawake hasa wanaoishi pamoja kama mke na mume kwa namna yoyote ile, kupigana siyo adhabu tosha ya kusuruhisha migogoro, mimi huyu mwanamke nimempa adhabu hiyo lakini naona imemnyoosha kweli kweli japo naona kabisa imemuharibu kisaikolojia kabisa.