Mke wangu anapitia wakati mgumu sana hadi nimemuonea huruma

Mke wangu anapitia wakati mgumu sana hadi nimemuonea huruma

Kununa hajujawahi kua suluhisho la kudumu kwenye migogoro Kama hiyo.

Ulichokifanya Ni kana kwamba uyo mwanamke ni unaiba tu (Mchepuko au hawala yako).
Hujaonesha Yale makucha na mAmlaka ya kiume kuonesha umekasirishwa na alichokifanya.
Unaweza ukaona ni rahisi, lakini hii adhabu ni kali sana, pengine kuliko hata hizi ulizozipendekeza hapa
 
Katika kipindi hiki chote alijua sababu ya mimi kuishi hivyo ni yeye kuchepuka, hii ni baada ya jana jioni kuniita Chumbani na kusema anajutia sana kufanya vile na hatarudia, jambo baya zaidi akasema ameshafikiria mara mbili kunywa Sumu, anaona hana thamani tena kwangu, Dah
emoji24.png
emoji24.png
nilimwonea huruma sana na nikahamua kumsamehe tuendelee na maisha lakini naona hali haijabadilika kwake yaani ni mtu wa mawazo na wasiwasi muda wote,
This is One Very Big Mistake....,,, Ulitumia Hisia badala ya Akili......Yaani ulishindwa kutimiza lile agizo la biblia la kuishi nao kwa Akili.......

Lingine pia Umetoa Msamaha kizembe sana,,,,huyo Muhuni hajajifunza lolote....KUACHA mwanamke inahitaji kuwa MWANAUME kweli..,,,na kama huna uwezo wa kuacha basi hata ungeonyesha kuacha huenda ingebadilisha lolote....

Be a Man, Stay Taliban...

ROBERT HERIEL aliwahi kusema Usimuonee huruma Mwanamke
 
Tatizo kubwa lilianza pale nilipogundua anachepuka na ex wake. Baada ya kuligundua hilo sikutaka kuchukua hatua za shari sana papo kwa papo, bali nilichukua hatua ambazo mpaka leo anashindwa kuelewa afanyeje, sasa imefikia hatua muda wote ni analia tu, saiklojia hayupo sawa na kama anataka kuchanganyikiwa hivi.

Baada ya kugundua kwamba anachepuka nilichukua maamuzi yafuatayo

1. Siku hiyo hiyo niliyogundua sikutaka kumuuliza kama ni kweli au siyo kweli kwa sababu nilishajihakikishia kwa asilimia 100.

2. Sikula Chakula chake, nilifika naingia jikoni na kuandaa Chakula mwenyewe (hii imeendelea hadi leo)

3. Najitahidi sana niwahi kurudi nyumbani tofauti na siku za nyuma.

4. Tukilala kitandani mimi nageukia mzungu wa nne.

5. Tangia siku hiyo sijawahi kumuomba unyumba(japo anaweka mazingira ya jambo hili kila siku)

6. Akiniuliza namjibu kidogo alafu naendelea na utaratibu wangu.

7. Kila kitu najifanyia hadi nguo chafu zote za kwangu nakusanya na kufua mwenyewe nikapata nafasi(Ninapokuta amezifua narudia kufua)

8. Simtukani wala kumuongelesha vibaya bali nafanya mambo yangu ndani ya nyumba kivyangu.

9. Baada ya kuona hivyo, akasema anataka akaonane na Mama yake(ilikuwa Ijuma usiku, nikampatia nauli muda huo huo na kumwambia asubuhi na mapema aende, ghafla akasema ameahirisha hadi sasa yupo)

10. Nimeacha kuchangia naye kitu chochote ndani ya nyumba isipokuwa sehemu ya kulala tu(kitandani na penyewe mzungu wa nne au nalala sebleni wakati mwingine).

Sasa leo ni siku ya 6 tangia nimeanza kuishi hivyo na mke, mke wangu amenyongonyea ghafla, amekonda, amekuwa mtu wa mawazo na wasiwasi muda wote.

Katika kipindi hiki chote alijua sababu ya mimi kuishi hivyo ni yeye kuchepuka, hii ni baada ya jana jioni kuniita Chumbani na kusema anajutia sana kufanya vile na hatarudia, jambo baya zaidi akasema ameshafikiria mara mbili kunywa Sumu, anaona hana thamani tena kwangu, Dah [emoji24][emoji24] nilimwonea huruma sana na nikahamua kumsamehe tuendelee na maisha lakini naona hali haijabadilika kwake yaani ni mtu wa mawazo na wasiwasi muda wote, kiufupi anapitia wakati mgumu sana.

Wito kwa wanaume na wanawake hasa wanaoishi pamoja kama mke na mume kwa namna yeyote ile, kupigana siyo adhabu tosha ya kusuruhisha migogoro, mimi huyu mwanamke nimempa adhabu hiyo lakini naona imemnyosha kweli kweli japo naona kabisa imemuharibu kisaikolojia kabisa.
Kuna mama mmoja amekuja dukani kwangu leo akanunua nyundo kubwa nilipomuuliza ya nini akanielezea stori kama hii na akasema leo usiku ni bora afanye maamuzi magumu ili yeye na mumewe ''waondoke wakafanye kesi mbele ya Mungu'' kwani hata huyu mume wake alishawahi kuchepuka!
 
Kama Ni mtu anaye jielewa.. hivyo ulivyo msamehe kilaini kwake Ni zaidi ya adhabu.. ..harudii anahisi huo Ni mtego..

Lakini kwani wewe hujawahi kuwa na chepuko?! Pengine ndio unarejeshewa maumivu unayowapa wenzio..


Sent from my TECNO CD6 using JamiiForums mobile app
Hadi nimehisi bora ningechukua maamuzi mengine, maana ni kama nimemharibu saiklojia.
 
Ni hatari sana kuendelea kuishi na mwenza mwenye tabia ya uzinzi......

Narudia tena ni hatari sana kuendelea kuishi na mwenza mwenye tabia ya mzinzi.......

Narudia tena no hatari sana kuendelea kuishi na mwenza mwenye tabia ya uzinzi.....

WORD IS ENOUGH FOR THE WISE.....
 
Back
Top Bottom