Mke wangu anapitia wakati mgumu sana hadi nimemuonea huruma

Ukiona mkeo wanakumbushiabna na x wake ujue kuna mambo hawajamaliza. Hapo lazima watafanya kwa siri sana kiasi kwamba kugundua itakuwa ngumu.

Hapo cha msingi kama umemsamehe mpe vigezo na masharti kama siku ukimkuta ndiyo mwisho wa kupiga chini mazima
Ukihamua kuwa kwenye familia lazima uwe tayari kuvumilia, kuzikabili changamoto kama hizi, kwa kuwa alarm imeshagonga uhamuzi utakuwa rahisi sana kwangu.
 
Bwana Tears of the sun unastahili noble prize ya changamoto ya ndoa
 
Subiri kuchapiwa Tena utarudia hapa
Ulimwengu wa sasa ni neema tu ya Mungu, tunakutana nao ukubwani ujui mangapi kafanya nyuma kabla yako heri usiyasikie.

Mfano hawa wanachuo wanaoishi pamoja kinyumba zaidi ya miaka 3 chuoni kupika na kupakua,ex anamjua wife kuliko wewe,kipi kinawazuia kupeana maana hana cha kumringia,mtu maadamu akikuzalia watoto mengine usihoji,utakufa siku si zako.
 
Huyu jamaa kwa namna alivyopambana na suala lake hili, hakika nimepata somo kidogo.
 
Chance ya kurudia ni kubwa hawana uwezo wa kumshinda shetani, kuzini ni ujinga wa mind tu eti kuchepuka kutamu kumbe ni mind tu.
 
Kitu wanaume wengi tunakosea kwenye mahusiano. Unatakiwa umpe mwanamke masharti na vigezo.
Ajue kabisa akifanya kosa hili adhabu yake ni hii.

Ila kiukweli 100% ukishajua mkeo analiwa tena X wake kuna upendo hutoweka. Utamchukulia kawaida halafu moyoni utakuwa na hasira. Siku akikiudhi unaweza hata kumtukana hata mbele za watu.

Sidhani km unaweza kupata muda wa kukaa na mkeo mkapiga story na mkacheka pamoja.
Najua alikuwa na huyo jamaa amepiga hata km ni sana. Shida inakuja unagongewa mara ya pili.
Mtaishi ila ule upendo haupo tena.
Huyu jamaa kwa namna alivyopambana na suala lake hili, hakika nimepata somo kidogo.
 
Uko sahihi, ila kwa jinsi alivyopambana amejitahidi
 
Ni kweli ila raha ya ndoa mfurahi, mcheke na mpendane. Unakuwa na mwenza wako, unamtania, mnacheka hata wakati mwingine mnacheza muziki pamoja ila vinapotea pindi usaliti unapoingia.
Hapo mtaishi ila ule upendo haupo ukikumbuka usaliti wake unapata hasira.
Akikosea unaweza kufikiri anafanya makusudi.
Uko sahihi, ila kwa jinsi alivyopambana amejitahidi
 
Tusubiri kikao cha mwisho alichosema tutajua maamuzi yake ya mwisho
 
Kwa hapo ww ndo unapitia magum mkuu.... Huyo bi dada anakuigizia tu
Unajua mwanamke hadi ameamua kulala na mwanaume mwingine yeye ndio amechochea hilo swala sio huyo mchepuko
Mwanamke wa namna kama hyo haupaswi kabisa kumsamehe kirahis unaweza pia kutokumsamehe kabisa
Atakuja afanye tukio kubwa na anaweza hata shawishiwa kukumaliza na akafanya hivo kwa sabb sio mwaminifu na hana sifa ya kuitwa mke.
BROTHER RUN
 
Kuna watu wanakuona mjinga kwasababu wao ni wajinga zaidi yako. Lakini ibakie TU kwamba, nyumba zinasiri nyingi sana.
 
Mke kucheat na ex wake ni jambo kubwa Sana, wanaume walio kamili na wanawake makini wanaelewa maana yake., Hilo sio kosa la kusamehe kabisa.
 
Umeandika vizuri kama vile wewe huchepukagi. Au ndio mkuki kwa nguruwe ila kwa binadamu mchungu.

Ukiona mwanamke amechepuka ujue wewe mwanaume ndio tatizo. Hata ukimwacha ukioa mwingine atachepuka tu maana wewe tatizo lako utakuwa hujalijua na kulitatua.
 
Vipi wewe mwanaume ukichepuka yeye afanyeje?
 
Ngoja aje akugeuzie kibao aje akupige na kitu kizito unamuonea huruma mwanamke bora umruhusu aondoke kwanza akija kunywa sumu humo ndani ndo utajua hujui.
 
Mkuu hongera sana kwa namna unavyo lishughulikia hilo tatizo Mungu akuongoze ulimalize salama. Uwe unatuletea update kuna vitu tunajifunza wengine kupitia wewe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…