Mke wangu anapitia wakati mgumu sana hadi nimemuonea huruma

Mke wangu anapitia wakati mgumu sana hadi nimemuonea huruma

Dah! Mkuu kama ulimpora Uyo ex -wake yakupasa kuvumilia tuu. Ukioa mtaa wako jaribu kuhamisha makazi kidogo ya kuishi mfano Dar to Shinyanga🤣🤣

Hapo utamfanya mkeo abadili fikra zake zote na kuwa na future na wewe ingawa haimaanishi kuwa hatachepuka tena. Possibility ya kufanya hivyo ni ndogo sana kuliko mtaani kwao.
 
Mke ana wame wawili
Mume mkolezo na mume mpauko 😂😂.
Kaka umepigwa igizo wazi wazi
 
Umeandika vizuri kama vile wewe huchepukagi. Au ndio mkuki kwa nguruwe ila kwa binadamu mchungu.

Ukiona mwanamke amechepuka ujue wewe mwanaume ndio tatizo. Hata ukimwacha ukioa mwingine atachepuka tu maana wewe tatizo lako utakuwa hujalijua na kulitatua.
kutofautiana kwa mtazamo kusiwe sababu ya kuhukumiana. Nahisi ulikuwa na uwezo wa kutoa maoni yako kwa maudhui ya uzi wa mtoa mada na sio kujaribu kuhukumu wachangiaji pia.

Kujibu swali lako tu, mimi sichepuki, kwa vile kila ulikekutana nae alikuchepekia haimaniishi wanaume wote wachepukaji.
 
Kuachana hao ni ngumu. Sisi tunakuombea yaishe salama kama mdau wetu humu.
 
Mke wangu anatarajiwa kuruhusiwa Kutoka hospitalini hapo kesho kwa mujibu wa daktari alivyosema leo. Jana nilimpeleka mtu wa saiklojia, hili ajarabu kuirudisha saiklojia yake sawa. Baada ya kurusiwa Kutoka hospitalini tutakuwa na kikao Pande zote mbili (wazazi wangu na wazazi wake), Hiki kikako kikimalizika salama, maamuzi yangu ya mwisho yatategemeana na kikao hicho (Mengine yaliyoendelea siwezi kuyaandika, lakini nisema kwamba bado hili suala ntalishughulikia na kulimaliza salama)

Nimependa sana unavyompigania mkeo, kukosea kupo na huyo dada itakua kapata funzo.

Mungu aitunze ndoa yenu
 
Tatizo kubwa lilianza pale nilipogundua anachepuka na ex wake. Baada ya kuligundua hilo sikutaka kuchukua hatua za shari sana papo kwa papo, bali nilichukua hatua ambazo mpaka leo anashindwa kuelewa afanyeje, sasa imefikia hatua muda wote ni analia tu, saikolojia hayupo sawa na kama anataka kuchanganyikiwa hivi.

Baada ya kugundua kwamba anachepuka nilichukua maamuzi yafuatayo

1. Siku hiyo hiyo niliyogundua sikutaka kumuuliza kama ni kweli au siyo kweli kwa sababu nilishajihakikishia kwa asilimia 100.

2. Sikula Chakula chake, nilifika naingia jikoni na kuandaa Chakula mwenyewe (hii imeendelea hadi leo)

3. Najitahidi sana niwahi kurudi nyumbani tofauti na siku za nyuma.

4. Tukilala kitandani mimi nageukia mzungu wa nne.

5. Tangia siku hiyo sijawahi kumuomba unyumba(japo anaweka mazingira ya jambo hili kila siku)

6. Akiniuliza namjibu kidogo halafu naendelea na utaratibu wangu.

7. Kila kitu najifanyia hadi nguo chafu zote za kwangu nakusanya na kufua mwenyewe nikipata nafasi(Ninapokuta amezifua narudia kufua)

8. Simtukani wala kumuongelesha vibaya bali nafanya mambo yangu ndani ya nyumba kivyangu.

9. Baada ya kuona hivyo, akasema anataka akaonane na Mama yake(ilikuwa Ijumaa usiku, nikampatia nauli muda huo huo na kumwambia asubuhi na mapema aende, ghafla akasema ameahirisha hadi sasa yupo)

10. Nimeacha kuchangia naye kitu chochote ndani ya nyumba isipokuwa sehemu ya kulala tu(kitandani na penyewe mzungu wa nne au nalala sebuleni wakati mwingine).

Sasa leo ni siku ya 6 tangia nimeanza kuishi hivyo na mke, mke wangu amenyongonyea ghafla, amekonda, amekuwa mtu wa mawazo na wasiwasi muda wote.

Katika kipindi hiki chote alijua sababu ya mimi kuishi hivyo ni yeye kuchepuka, hii ni baada ya jana jioni kuniita Chumbani na kusema anajutia sana kufanya vile na hatarudia, jambo baya zaidi akasema ameshafikiria mara mbili kunywa Sumu, anaona hana thamani tena kwangu, Dah [emoji24][emoji24] nilimwonea huruma sana na nikaamua kumsamehe tuendelee na maisha lakini naona hali haijabadilika kwake yaani ni mtu wa mawazo na wasiwasi muda wote, kiufupi anapitia wakati mgumu sana.

Wito kwa wanaume na wanawake hasa wanaoishi pamoja kama mke na mume kwa namna yoyote ile, kupigana siyo adhabu tosha ya kusuruhisha migogoro, mimi huyu mwanamke nimempa adhabu hiyo lakini naona imemnyoosha kweli kweli japo naona kabisa imemuharibu kisaikolojia kabisa.
Hiyo adhabu uliyompa usingemsamehe angekufa,hio adhabu iskie tu kwa jirani.
 
Nimesoma comment nyingi za wanaume wenzangu wakiona adhabu uliyotoa no ndogo na kwao adhabu tosha ilikua kumuacha mkeo.

Huo ni upuuzi na usifuate ushauri wa vijiweni huo. Binadamu ni wakosefu na tunastahili msamaha . Bora amani irejee.

Hawa wanaume ndo wanaotongoza wake zetu kila siku makazini, njiani au wakiwa kwenye biashara. Wako tayari kuwa spoil wake zetu Ili watulize nyege zao ila gafla demu akiwapa walichokua wanakitaka wanaanza kumuona demu hafai.

Huo ni ukichaa na ubinafsi. Yaani naimagine ambavyo kazini tunavyowatoleaga macho wake wa watu na kuwalazimisha japo aflirt na wewe tu ujisikie vizuri , Leo huku JF tunajifanya kuwapandishia vioo mademu waliokamatwa wame cheat .

Kanuni ni ile Ile ya YESU ikiwa kati yenu Kuna mtu hajawahi fanya dhambi na awe wa kwanza kumpiga jiwe mwanamke huyu !!!

Maombi yangu siku zote kama ilivyo kwa wanaume wengi Mungu amlinde mke wangu awe na hofu na aniondolee mtihani huu wa kuzalauliwa na wanaume wasiojua msamaha maana yake Nini.

Mungu azidi kukubariki una hekima sana
 
Tatizo kubwa lilianza pale nilipogundua anachepuka na ex wake. Baada ya kuligundua hilo sikutaka kuchukua hatua za shari sana papo kwa papo, bali nilichukua hatua ambazo mpaka leo anashindwa kuelewa afanyeje, sasa imefikia hatua muda wote ni analia tu, saikolojia hayupo sawa na kama anataka kuchanganyikiwa hivi.

Baada ya kugundua kwamba anachepuka nilichukua maamuzi yafuatayo

1. Siku hiyo hiyo niliyogundua sikutaka kumuuliza kama ni kweli au siyo kweli kwa sababu nilishajihakikishia kwa asilimia 100.

2. Sikula Chakula chake, nilifika naingia jikoni na kuandaa Chakula mwenyewe (hii imeendelea hadi leo)

3. Najitahidi sana niwahi kurudi nyumbani tofauti na siku za nyuma.

4. Tukilala kitandani mimi nageukia mzungu wa nne.

5. Tangia siku hiyo sijawahi kumuomba unyumba(japo anaweka mazingira ya jambo hili kila siku)

6. Akiniuliza namjibu kidogo halafu naendelea na utaratibu wangu.

7. Kila kitu najifanyia hadi nguo chafu zote za kwangu nakusanya na kufua mwenyewe nikipata nafasi(Ninapokuta amezifua narudia kufua)

8. Simtukani wala kumuongelesha vibaya bali nafanya mambo yangu ndani ya nyumba kivyangu.

9. Baada ya kuona hivyo, akasema anataka akaonane na Mama yake(ilikuwa Ijumaa usiku, nikampatia nauli muda huo huo na kumwambia asubuhi na mapema aende, ghafla akasema ameahirisha hadi sasa yupo)

10. Nimeacha kuchangia naye kitu chochote ndani ya nyumba isipokuwa sehemu ya kulala tu(kitandani na penyewe mzungu wa nne au nalala sebuleni wakati mwingine).

Sasa leo ni siku ya 6 tangia nimeanza kuishi hivyo na mke, mke wangu amenyongonyea ghafla, amekonda, amekuwa mtu wa mawazo na wasiwasi muda wote.

Katika kipindi hiki chote alijua sababu ya mimi kuishi hivyo ni yeye kuchepuka, hii ni baada ya jana jioni kuniita Chumbani na kusema anajutia sana kufanya vile na hatarudia, jambo baya zaidi akasema ameshafikiria mara mbili kunywa Sumu, anaona hana thamani tena kwangu, Dah [emoji24][emoji24] nilimwonea huruma sana na nikaamua kumsamehe tuendelee na maisha lakini naona hali haijabadilika kwake yaani ni mtu wa mawazo na wasiwasi muda wote, kiufupi anapitia wakati mgumu sana.

Wito kwa wanaume na wanawake hasa wanaoishi pamoja kama mke na mume kwa namna yoyote ile, kupigana siyo adhabu tosha ya kusuruhisha migogoro, mimi huyu mwanamke nimempa adhabu hiyo lakini naona imemnyoosha kweli kweli japo naona kabisa imemuharibu kisaikolojia kabisa.
Ukweli ni kwamba wewe umejipa adhabu kupitia kosa lake na umejiumiza kisaikolojia.
 
Mm nilioa kabisa, yaan hata mwez haikupita nimekuja kugundua ana kijana wa kawaida sana, kweli nilijiuliza maswali mengi sana ambayo yalikosa majibu, yaan mnatoka kufunga ndoa, harusi mtu haoni hata uchungu wa gharama zote???.

TUKAYAONGEA YAKAISHA
Hapa kwanza nilikosa amani kabisa, yaan hata ile furaha ya ndoa ilinisha, pili nililibeba kwa lengo la sikutaka kuonekana ndoa yangu imedumu kwa mwezi mmoja, hivyo nililibeba angalau nisogeze siku huku nikiendelea kufanya tafiti.

Huwez amin amerudia jambo lilelile, nikaona hapa sasa hakuna jipya na angarau kidogo nimesogeza siku nikampiga taraka akafie mbele
 
Malaya ni malaya hutuna jinsi wanaume alisilimia kubwa wake zetu wana umalaya fulani wa siri ndo maana migogoro na talaka kila siku
 
Hahaha jamaa anachapiwa utamu wake halafu anazila kula, anafua nguo zake mwenyewe, anapika mwenyewe mbaya zaidi analala mzungu wanne akili za kijinga kabisa
Halafu anajipongeza eti ametoa adhabu kwa mwanamke hata wiki haijaisha ana conclude kuwa mkeo anajutia na amekuwa na stress

Jiuulize baada ya kukataa haki yako kwa huo muda vipi siku aliyokupa, je alikupa kwa kiwango kisicho cha kawaida au bado alikuwa na huzuni

Fanya analysis kwa hiyo siku aliyokupa kama aliifurahia basi huyo hajajutia

Sent from my SM-A037F using JamiiForums mobile app
 
Its a soft approach but doesn't mean it works.

Mwanamke akishacheat ina maana either haridhiki na wewe au ana tamaa zake za asili (zipo kwenye damu DNA) za kupenda kujaribu shaft na ladha tofauti tofauti.

Kwa hiyo iwe ni kutoridhika au tamaa zake za asili (DNA) either way hizo hazinaga dawa mzee baba.

Unune, ujifulie nguo, ujipikie, usisex,umpige mpaka apasuke, upeleke case kwa wazazi hata umsemee kwa viongozi wa dini none of them is going to work.

Mwanaume usiwe na uoga eti ndoa ikivunjika jamii itakuonaje au sijui eti watoto wataishije, kwa awaida hivyo vitu kwenye jamii vinamuathiri sana mwanamke na sio mwanaume.
Ukiona mwanamke hajali hayo yote na akaccheat bro you'e the walking dead asipokugeuza zuzu basi atakuua iwe directly kwa sumu au indirectly kwa ngoma, presha na visukari.

Acha hizo dhana za kizamani kwenye ulimwengu wa sasa, mwanamke akicheat na ukajihakikishia kwa asilimia mia piga chini haraka iwezekanavyo, ikiwezekana hata usimwambie sababu ya kumuacha fukuza tu.
 
suluhisho ungemwambia amletebex wake mmpige threesome ndo umsamehee
 
Kama huja muoa unamtesa bure.
Muoe kwanza ndio mambo mengine yaendelee.

Unaweza dhani kachepuka hiyo siku tu kumbe umemkamata siku hiyo.
 
Back
Top Bottom